Design a site like this with WordPress.com
Get started

Bado Hujaamua Kukipata Kitu Hiki Ndiyo Maana Hukipati

Mtu mmoja alikuwa anasoma gazeti nyumbani kwake, mara akatokea mgeni akamuuliza vipi mbona mbwa wako analia hivyo?

Akamjibu, amekalia msumari, yule mgeni akamwambia kwanini sasa usimtoe?
Akamjibu, kama ingekuwa msumari umemchoma vizuri angetoka hapo alipo asingeendelea kulia.

Hii ni hadithi fupi, lakini ina funzo ndani yake.

Hii iko hata katika maisha yetu ya kawaida wako watu wanalalamika kila siku kuwa kuna vitu vinawachosha au wamechoka kuishi maisha yasiyokuwa na viwango lakini cha ajabu hawachukui hatua wanaendelea kulalamika tu.

Kama kweli hali uliyonayo huipendi, ina kukera huwezi kuendelea kuivumilia kwa gharama yoyote ile. Utatafuta namna yoyote uitoe.

Vipi kama mtu akija kukuziba pua sasa hivi, utaendelea kumuangalia tu wakati ukikosa pumzi? Lazima utachukua hatua ili uweze kupata pumzi.

Pale tunapoona jambo ni la muhimu huwa tunakua hatuna sababu. Kwa mfano, umezama kwenye maji halafu akatokea mtu anauza vifaa vya uogeleaji utakua na muda wa kubishana naye juu ya bei? Utakachoangalia wewe ni kuokoa uhai wako utachukua mara moja.

Hii ni mifano halisi ambayo tuko nayo katika maisha yetu. Lengo langu ni kukuambia kuwa kama kweli kuna kitu unakitaka na ni muhimu kwenye maisha yako utapambana mpaka ukipate.

Wale ambao hawajapata kile wanachotaka jawabu ni rahisi tu bado hawajajitoa sadaka na hawajaamua kupata kile wanachotaka.

Kama jambo ni muhimu utalifanya tu na kama siyo muhimu utatafuta sababu za kutofanya. Chukulia mfano hata wewe mwenyewe unafanya yale ambayo ni muhimu kama unaona siyo muhimu utatafuta sababu za kutokufanya.

Hatua ya kuchukua leo; Amua kupata kile unachotaka na utakipata kwa gharama yoyote ile.
Dunia inakupa kile unachotafuta kama ukijitoa kweli.

Kwahiyo, angalia juhudi unazoweka je zitakufikisha kule unakotaka kufika?
Kama haziwezi, basi badilisha gia inayoendana na kasi unayotaka.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz

Asante Sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: