Design a site like this with WordPress.com
Get started

Haya Ndiyo Mafanikio Unayopaswa Kuwa Nayo

Iko wazi kila mtu ana ndoto yake hapa duniani. Lakini cha kuchangaza wako watu ambao wala hawana ndoto.

Kuna binadamu wengine wako kama vile wanyama wanachojua wao ni kula tu. Wako ambao wanaishi ili wale na wako ambao wanakula ili waishi.

Vipi ile ndoto yako uliyokuwa nayo kwa sasa umefikia wapi?

Nasikitika kuwa ndoto za watu wengi zinazimika kama vile mshumaa unavyozimika katika upepo.

Ipo siri moja ambayo watu wengi bado hawajaifahamu ambayo ni kusikiliza sauti yao ya ndani.

Unajua mafanikio yako makubwa ni yale ambayo unasikiliza sauti yako ya ndani inataka nini ndiyo maana hata ukifanikiwa unakua huna lile ridhiko la moyo yaani unaona kile ambacho ulikua unakitaka bado hujakipata unajiona kama vile ni mpweke fulani licha ya kuwa na Mafanikio kwa nje lakini ndani bado unaona nafsi yako haiko huru.

Hii ni dalili ya mtu ambaye bado hajaisikiliza sauti yake ya ndani.

Kwa kulitambua hilo, mwaka 2017
nilikaa chini na kuandika kitabu kiitwacho Ongea Lugha Yako, Sauti Yako Ya Ndani Ndiyo Mafanikio Yako.

Kitabu hiki kitakusaidia namna ya kujua nini kusudi lako hapa duniani.

Kujua namna ya kuishi maisha yenye maana kwa mifano halisi.

Kitakusaida kupata mwongozo sahihi wa namna ya kusikiliza sauti yako ya ndani ili uweze kupata mafanikio katika maisha yako.
Kwa mifano halisi ya watu waliofanya makubwa duniani kitabu hiki kitakusadia.

Katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona, ndiyo wakati sahihi wa kukaa chini na kusikiliza sauti yako ya ndani. Usipojua kuisikiliza sauti yako ya ndani hutoweza kuongea lugha yako.

Sasa ili haya yote yapate kibali kwako nakualika uweze kusoma kitabu cha Ongea Lugha Yako, Sauti Yako Ya Ndani Ndiyo Mafanikio Yako.

Huna wakati mwingine wa kuongea lugha yako zaidi ya huu, kadiri ya Seneca lugha ya ukweli huwa siku zote ni rahisi na sasa jipatie nakala ya kitabu hiki uone jinsi ilivyo rahisi kusikiliza sauti yako ya ndani hapa duniani.

Kushindwa kuongea lugha yako na kusikiliza sauti yako ya ndani imesababisha hata watu kushindwa kutambua wito wao sahihi. Siyo tu wito hata kufanya kazi wasizozipenda hii yote ni kwa sababu ya kushindwa kuongea lugha yako kwa kutokusikiliza sauti yako ya ndani.

Yako mengi ambayo tunafanya lakini wala hatuyafurahii tunapingana kabisa na sauti zetu za ndani.

Jinsi ya kupata kitabu hiki cha Ongea Lugha Yako, Sauti Yako Ya Ndani Ndiyo Mafanikio Yako

Kwanza kitabu hiki kipo katika mfumo wa nakala tete, na bei yake ni shilingi elfu Kumi tu.

Lakini utakipata kitabu hiki kwa bei rahisi ya ofa ya shilingi elfu Tano tu (5000/=).

Unachotakiwa kufanya ni kutuma malipo ya shilingi elfu Tano tu kwenda namba 0717101505 au 0767101504 majina yatakuja Deogratius Kessy

Baada ya kutuma nitumie email yako na jina la kitabu kisha kitabu kitakufikia hapo ulipo.

Kitabu hiki utakisomea kwenye simu yako, kompyuta yako au hata tablet yako.

Kitabu hiki utakua unatembea nacho kwenye simu yako pale tu utakapopata muda unafungua unasoma huna tena sababu ya kupoteza muda wako.

Hatua ya kuchukua leo: Hakikisha unapata kitabu hiki cha Ongea Lugha Yako Sauti Yako Ya Ndani Ndiyo Mafanikio Yako kwa bei punguzo shilingi elfu 5000/= na mwisho wa ofa hii ni tarehe 3 May 2020.
Hivyo usisubiri mpaka tarehe 3 May ndiyo uchukue hatua, linalowezekana leo lisingoje kesho.

Kwahiyo, mafanikio yako makubwa yako ndani yako na ili uweze kuyajua jifunze kuongea lugha yako na kusikiliza sauti yako ya ndani.

Makala hii imeandikwa na;
Mwl. Deogratius Kessy ambaye ni mwalimu, mwandishi na mjasiriamali.

deokessy.dk@gmail.com, 0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog
Asante sana na Karibu sana rafiki yangu.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: