Kwa sababu sisi binadamu ni wavivu kiasili. Usipokuwa na mtu anayekuwajibisha ni vigumu kuchukua hatua. Kama unaona nidhamu binafsi bado ni tatizo tafuta mtu ambaye atakuwajibisha yaani accountability partner. Mtu ambaye unamweshimu na wala hutoweza kumwangusha hata kidogo. Wakati mwingine unaweza kumpa kiasi fulani cha fedha kwamba akae na hizo fedha usipofanya kitu fulani basi …
Category Archives: HAMASA
Kinachokufanya Usiende Mbele Ni Hiki Hapa
Hakuna kitu kingine zaidi ya kutochukua hatua. Hakuna mtu asiyejua ili afanikiwe anapaswa kufanya nini. Hakuna asiyejua ili afanikiwe kiroho, kiakili au kimwili anatakiwa kufanya nini. Watu wanajua kile wanachopaswa kufanya lakini shida iko kwenye kutokuchukua hatua. Wako watu wana kiri kabisa baada ya kuanza kuchukua hatua kwa nidhamu sasa wanaona mabadiliko chanya kwenye maisha …
Continue reading “Kinachokufanya Usiende Mbele Ni Hiki Hapa”
Ulinzi Kamili Ni…
Asubuhi njema rafiki yangu, ukawe na maadhimisho mazuri ya sabasaba leo jitakari biashara gani ya familia utakayoiachia familia yako hata ukifa badala ya kuwaachia familia yako CV ambayo itasomwa kwenye mbele ya jeneza lako huku ikiwa haiwezi kuwasaidia wale uliowaacha kulipa bili. Tengeneza njia kwenye kizazi chako ili kisije kupata shida baadaye. Unayo nafasi sasa …
Hakuna Biashara Inayojiendesha Kwa Hasara
” ujinga ni kufanya kitu kwa mtindo ule ule huku ukitegemea kupata matokeo tofauti.” Usifanye kwa mazoea, fanya kwa kusudi. Jipime kwenye kila unalofanya je,kuna faida unayopata au hasara? Ukiona ni hasara acha kwa sababu hakuna biashara inavyojiendesha kwa hasara bali faida. Mwl. Deogratius Kessy
Kuwa Mkali Kwa Mtu Huyu Hapa
Rafiki yangu, Yako mambo mengi tu unashindwa kuyatekeleza kwa sababu ya kukosa nidhamu binafsi. Umekosa kuwa na nidhamu binafsi ndiyo maana mambo mengi huyakamilishi. Wakati unapokuwa na njaa huwa hujali kitu kingine zaidi ya kupata chakula ili ushibe. Unatakiwa kuwa na nidhamu hiyo kwenye kile ulichojiwekea kufanya yaani hutulii mpaka upate kile unachotaka kwenye maisha …
Ukipata Nafasi Hii Itumie Vizuri
Kwa chochote kile ambacho unaweza kufanya sasa kifanye. Usipeleke mambo mbele kwa kuahirisha leo kwani ya mbele huyajui yatakuwaje. Punguza mambo mapema. Kwa chochote kile utakachoweza kufanya leo fanya wala usipeleke mambo mbele kwa sababu wakati ulionao sasa ndiyo wakati muhimu na wa uhakika. Vile ambavyo unaweza kuvikamilisha leo au sasa vikamilishe.Kila siku tembea na …
Hii Ndiyo Njia Nzuri Ya Kuhubiri Injili
Siku moja Mt Fransisco wa Assis alimwambia ndugu twende tukahubiri ijili. Walitembea mpaka vijini sasa yule ndugu aliyekuwa naye akamwambia, mbona hatuhubiri injili tunapita tu? Fransisco akamjibu akamwambia ndugu kupita kwetu tu, tunahubiri injili. Rafiki, jinsi tu unavyovaa unahubiri injili ya Mungu. Je, unavaaje? Jinsi tu unavyoishi maisha yako unahubiri injili. Je, maisha yako unaishije? …
Huyu Hapa Anaona Juhudi Zako
Asili inaona juhudi zako. Na kawaida asili huwa haipendi deni la mtu. Inamlipa mtu kadiri ya thamani anayoitoa. Mungu anaona juhudi zako unazoweka katika kile unachofanya. Hivyo basi, hawezi kukuacha, endelea kumtegemea na kuweka kazi.Weka kazi na sala kwenye kile unachofanya na utafanikiwa ni suala la muda tu. Endelea kuweka bidii kwenye kile unachofanya kwa …
Hili Ndiyo Eneo Zuri La Kuwa Mbishi
Kwenye ubishi hakuna mtu ambaye anakubali kushindwa. Mtabishana lakini kila mtu atabaki kuwa katika kile anachoamini. Mabishano yako mengi, wako ambao wanabishania siasa, mpira wa miguu, na mengine ambayo sijayaorodhesha hapa. Unapobishana unakua unapoteza nguvu kubwa ambazo ungezielekeza kwenye uzalishaji ungekuwa mbali. Leo ninataka nikupe kazi ya kwenda kuwa mbishi kwenye eneo moja muhimu sana …
Jinsi Ya Kupata Kile Unachotaka Kwenye Maisha Yako
Mpendwa rafiki yangu, Ukitaka kushindwa katika maisha basi ishi bila kujua kile unachotaka. Kanuni moja ya mafanikio ni kwanza jua kile unachotaka. Ni nani kati yetu anaweza kwenda dukani kununua mahitaji halafu anafika pale hajui kile anachotaka? Hivi kama hujui kile unachotaka dunia itakusaidiaje? Kama huulizi utajibiwaje? Kama huna unachoomba utapewa nini sasa? Kama hujui …
Continue reading “Jinsi Ya Kupata Kile Unachotaka Kwenye Maisha Yako”