Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kinachokufanya Usiende Mbele Ni Hiki Hapa

Hakuna kitu kingine zaidi ya kutochukua hatua.

Hakuna mtu asiyejua ili afanikiwe anapaswa kufanya nini. Hakuna asiyejua ili afanikiwe kiroho, kiakili au kimwili anatakiwa kufanya nini.

Watu wanajua kile wanachopaswa kufanya lakini shida iko kwenye kutokuchukua hatua. Wako watu wana kiri kabisa baada ya kuanza kuchukua hatua kwa nidhamu sasa wanaona mabadiliko chanya kwenye maisha yao, lakini mwanzoni walikuwa tu wanachukulia poa kile wanachojifunza.

Ukitaka faida ya mawazo yako, maarifa unayopata, matunda ya kile unachotaka kufanya ni kuchukua hatua mara moja.

Bila kuchukua hatua kwenye yale tunayotaka hatuwezi kuyapata. Kama unasoma kitabu, usiishie tu kusoma bali hakikisha unaondoka na kitu cha kwenda kufanyia kazi. Hata unaposoma hakikisha ukitoka hapa unakwenda kufanyia kazi kile ulichojifunza.

Ndani yako una utajiri wa kutosha shida yako, hutaki kuanza kuutumia utajiri huo ulioko ndani yako.

Utapata elimu ya kila aina lakini kama hutotumia elimu hiyo kwenye vitendo hutapiga hatua. Kama watu wanafundishwa mazuri kila siku kwa nini sasa hawayatumii mazuri hayo? Tatizo watu wanajua wanatakiwa kufanya nini ila shida ni uvivu wa kutokuchukua hatua.

Acha uvivu, ujinga na uzembe chukua hatua kwenye yale uliyojifunza. Njia nzuri ya kujaribu kama umeelewa kile ulichojifunza ni kukifanyia kazi.

Hatua ya kuchukua leo; ujumbe wangu mkubwa kwako leo ni fanyia kazi yale yote unayojifunza.

Kuwa mwanafunzi wa kufanyia kazi kile unachojifunza. Zawadi ya kile unachojifunza ni kuchukua hatua.

Usipofanyia kazi kile ulichojifunza unakuwa huna tofauti na yule mtu ambaye hajajifunza. Na unajua kusoma halafu husomi unakuwa huna tofauti na yule mtu asiyejua kusoma. Usikubali kufa bila kufanyia kazi yale yote unayojifunza. Jifunze kila siku na fanyia kazi kila siku.

Muhimu;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: