Kwa chochote kile ambacho unaweza kufanya sasa kifanye. Usipeleke mambo mbele kwa kuahirisha leo kwani ya mbele huyajui yatakuwaje.
Punguza mambo mapema. Kwa chochote kile utakachoweza kufanya leo fanya wala usipeleke mambo mbele kwa sababu wakati ulionao sasa ndiyo wakati muhimu na wa uhakika.
Vile ambavyo unaweza kuvikamilisha leo au sasa vikamilishe.
Kila siku tembea na moto huu nitafanya sasa kile ambacho naweza kukifanya sasa.
Angalia ni majukumu gani unayoweza kuyafanya leo na yafanye sasa. Usiamini kuhusu kesho, baadaye, mwezi ujao au mwakani kwa sababu vitu hivi viko nje ya uwezo wako. Huwezi kuviathiri kwa namna yoyote ile ndiyo maana usiwe una uhakika na mambo ambayo yako nje ya uwezo wako.
Hatua ya kuchukua leo; nenda kabadili kile ambacho unaweza kukibadili sasa. Ukipata nafasi ya kufanya kile unachopaswa kufanya, fanya na wala usisubiri wakati ujao ambao huna hata uhakika nao.
Wakati sahihi ni sasa, usisubiri kupewa ruhusa. Jipe ruhusa ya kufanya kile unachotaka lakini usivunje sheria za asili.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo