Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kuwa Mkali Kwa Mtu Huyu Hapa

Rafiki yangu,

Yako mambo mengi tu unashindwa kuyatekeleza kwa sababu ya kukosa nidhamu binafsi.

Umekosa kuwa na nidhamu binafsi ndiyo maana mambo mengi huyakamilishi. Wakati unapokuwa na njaa huwa hujali kitu kingine zaidi ya kupata chakula ili ushibe. Unatakiwa kuwa na nidhamu hiyo kwenye kile ulichojiwekea kufanya yaani hutulii mpaka upate kile unachotaka kwenye maisha yako.

Nakusihi sana, uwe mkali wa wewe mwenyewe. Usikubali wewe mwenyewe ujiletee mazoea ya kijinga bali nidhamu binafsi.

Usisubiri mpaka watu wakukumbushe majukumu yako. Jikumbushe wewe mwenyewe na jitume sana.

Jitume sana kwenye kile unachotaka. Hakuna kitu kitakachokuja kwenye maisha yako bila kujituma.

Hatua ya kuchukua leo; Nenda kajitume leo mpaka upate kile unachotaka.

Kuwa mkali dhidi yako wewe mwenyewe. Weka kazi; wala usijionee huruma. Huwezi kufa kwa kufanya kazi bali utapata kile unachotaka kwenye maisha yako.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: