Siku moja Mt Fransisco wa Assis alimwambia ndugu twende tukahubiri ijili. Walitembea mpaka vijini sasa yule ndugu aliyekuwa naye akamwambia, mbona hatuhubiri injili tunapita tu? Fransisco akamjibu akamwambia ndugu kupita kwetu tu, tunahubiri injili.
Rafiki, jinsi tu unavyovaa unahubiri injili ya Mungu. Je, unavaaje?
Jinsi tu unavyoishi maisha yako unahubiri injili. Je, maisha yako unaishije?
Namna unavyofanya kazi unahubiri injili pia. Je, unafanyaje kazi zako?
Ushuhuda wa kile tunachofanya unajidhihirisha kwa namna tunavyoishi maisha yetu.
Angalia kile unachofanya unakifanya unakifanya kwa mapenzi ya nani? Ya Mungu au ya mwanadamu?
Shauku yako ya kutenda kutoka ndani ya moyo inajionesha yenyewe kupitia matendo yako kama unafanya ili binadamu akuone au Mungu akuone.
Hatua ya kuchukua leo; Kwa chochote kile unachofanya sasa, kifanye kwa ubora wa hali ya juu kwani unapofanya vizuri au vibaya jua unahubiri injili ya kile kilichopo ndani yako.
Maisha unayoishi yawe na utukufu kwako na kwa wengine. Kile unachofanya kiwe baraka kwa wengine.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante Sana
©Kessy Deo