Dunia yetu inahitaji watu makini sana karibu kila eneo la maisha yetu tunahitaji watu makini.
Watu wasipokuwa makini mambo mengi yataathirika.
Kama hakuna watu makini basi kuna wazembe na hawa wazembe ndiyo wanaoleta madhara katika maisha yetu.
Leo tunakwenda kujifunza jinsi ya kuwa makini kwenye kila eneo la maisha yetu.
Ipo njia rahisi sana ya sisi kuwa makini kwenye vile tunavyofanya. Na njia hiyo ni kuwa mwangalifu.
Ukitaka kuishi miaka mingi hapa duniani basi kuwa mwangalifu kwenye kila eneo la maisha yako.
Kuwa mwangalifu kwenye eneo la kiroho. Hapa zingatia yale yanayohusiana na mambo yote ya kiroho.
Kuwa mwangalifu kuyaishi.
Kuwa mwangalifu katika eneo la akili. Hakikisha kila kinachoingia ndani ya akili yako ni bora kwa akili yako.
Usikubali kutumia akili yako kama choo, kila habari unaingiza bali kuwa mtu wa kuchuja, siyo kila kitu ni cha kuruhusu kuingia akilini mwako.
Ipo hivi, yako mambo ambayo ukiruhusu yaingie akilini mwako yanakuharibia kabisa na mengine yanakujenga. Kuwa mtu wa kuingiza habari chanya tu, acha kuingiza habari hasi zinazokutia hofu kubwa.
Kuwa mwangalifu na mwili wako. Mwili wako ni nyumba unayoishi lakini pia ni hekalu.
Jitunze kwa kula vizuri chakula chenye kuupa mwili nguvu.
Siyo kila kitu ni chakuweka tumboni, kuwa mwangalifu na kile unachokula.
Fanya mazoezi kwa afya ya mwili wako. Watu wengi siku hizi wanajiua kwa ulaji wao wenyewe.
Ndiyo maana rai yangu Mimi leo kwako ni kuwa mwangalifu.
Kuwa mwangalifu na fedha zako. Hakikisha unafanya kazi vizuri kwa kutoa thamani ili uweze kulipwa vizuri.
Fedha yoyote unayopata unatakiwa kujilipa kwanza wewe mwenyewe iwe ni kwenye kazi au biashara jilipe asilia kumi na zaidi kama uchumi unaruhusu.
Kuwa mwangalifu na hisia, tunashuhudia watu wanaoshindwa kudhibiti hisia zao wanapelekea hata kudhuru maisha ya watu wengine.
Usitawaliwe na hisia kwani ni madhara makubwa ambayo unaweza kuyasababisha na baadaye ukaja kujuta.
Kuwa mwangalifu katika mahusiano yako na utayafurahia mahusiano yako.
Mtu yeyote ambaye siyo mwangalifu kwenye eneo lolote la maisha yake ni rahisi kupoteza kile ambacho anacho.
Hatua ya kuchukua leo; Popote pale ulipo haijalishi unafanya nini jitahidi kuwa mwangalifu.
Ukiwa mwangalifu utayafaidi maisha yako lakini usipokuwa makini utayapoteza maisha yako.
Kwahiyo, njia ya uhakika ya kuishi muda mrefu ni wewe kuwa mwangalifu kwenye kila eneo la maisha yako.
Kwa kutumia mbinu hii utaweza kuwa na maisha bora sana.
Usipokuwa mwangalifu utaiacha dunia mapema hivyo jitahidi kuwa mwangalifu kwenye kila eneo la maisha yako.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo jiunge na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Jiunge na mfumo wetu wa kupokea makala zaidi kwa njia ya email. Jaza fomu unayoiona hapo juu palipoadikwa makala kwa email na kisha bonyeza subscribe.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl.Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante sana.