Ukishindwa Hakikisha Huna Sababu

Kama ukifeli mtihani kwa sababu hukusoma, itakuuma sana kwa nini sijasoma huenda ningesoma hata ningefaulu.Lakini, ikitokea unafeli mtihani na ulikuwa umesoma wala haitokuuma kwa sababu ulishafanya yaliyo ndani ya uwezo wako. Au kwa mfano, una mgonjwa anaumwa, ukienda kumuona kabla hajafariki haikuumi sana lakini ukijua mgonjwa amefariki na ulipaswa kwenda kumuona itakuuma sana.Vivyo hivyo katika …

Jinsi Ya Kujenga Afya Ya Roho

Huwezi kuwa binadamu kamili kama hujaweza kukamilika katika maeneo haya, afya ya akili, roho na mwili.Afya ya akili, roho na mwili ni muhimu sana kwa mtu kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake. Hata watu wengi wenye shida ya akili, huwa haamini kama wana shida ya akili. Na shida ya akili inaanzia pale unapokuwa unakosa afya …

Kama Huna Tabia Hizi Mafanikio Makubwa Hayakuhusu

Kila kitu kwenye maisha yetu huwa kinajengwa na tabia. Watu wengi mambo tunayofanya kila siku yanatokana na tabia ambazo tumejijengea huko nyuma. Watu hawafanyi kitu kama siyo tabia yao. Vitu vingi ambavyo unafanya ni kwa sababu ni tabia yako kufanya ndiyo maana unafanya hivyo. Huwa tunatengeneza tabia, kisha tabia zinatutengeneza. Ili uweze kufika au kufanya …

Vitu Viwili vya Msingi Kwenye Utajiri

Huwa tunakwama kwa sababu ya kufanya vitu vipya kila siku siku kwenye eneo la fedha. Kwenye maisha pia kwa ujumla tunakwama kwa kufanya vitu vipya kila siku huku tukisahau kufanya vitu vya msingi kabisa.Na Utajiri haupo kwa kufanya vitu vingi sana kwenye fedha. Bali utajiri kwenye fedha ni kufanya vitu vya msingi kila siku kwa …

Hakuna Mtu Mvivu Duniani

Ni kweli kiasili watu ni wavivu. Wanajua kile wanachopaswa kufanya lakini hawafanyi hivyo. Ukimchukua mtu mvivu na kumtumbukiza kwenye kina kirefu cha maji, uvivu wake wote unaondoka, hataendelea kuutukuza uvivu wake, bali atajitahidi kupambana kuhakikisha anajiokoa. Kwa mfano huo hapo juu, tunaona kwamba ni kweli hakuna mtu mvivu. Watu wanaamua wao wenyewe kuwa hivyo walivyo.Yule …

Njia Ya Hovyo Ya Mauzo

Wauzaji wengi sana wanadhani ili waweze kuuza sana na kukubalika na wateja basi wanatakiwa kupunguza bei. Kupunguza bei ni njia ya hovyo ya muuzaji bora kuwahi kutokea. Kwa sababu kadiri unavyokuwa unapunguza bei, ndivyo na wewe unavyojinyima nafasi ya kupata faida. Faida kwenye biashara ndiyo tunda tamu. Faida ndiyo itakusaidia wewe kuendesha maisha yako. Kama …

Ujuaji Umekufikisha Wapi?

Kama unajua kweli kwa nini hufanyi? Je, hufanyi kwa sababu ni uzembe? Uvivu au ujinga? Kama unajua kwa nini hufanyi? Je, huo ujuaji wako umekufikisha wapi? Ukijaribu kuongea na watu wengi kila mtu ni mjuaji, wako ambao wanawashawishi watu wao wa karibu kuwa watu fulani lakini wao hawafanyi. Kwa mfano, mtu anawahamasisha wenzake kuwekeza kwenye …

Tumia Nguvu Zako Vizuri

Kama ingekuwa kufanya kazi kwa bidii tu inakutosha kuwa tajiri basi watu wengi wangeshakuwa matajiri. Watu wengi sana wanajituma lakini miaka nenda, rudi lakini bado wako pale pale.Unaweza kujiuliza ni kwa nini lakini sababu ni kwamba ni kushindwa kutumia nguvu vizuri. Chukulia Simba, Simba ni mwindaji bora kuwahi kutokea lakini hata siku moja huwezi kumkuta …

Tengeneza Hadithi Yako

Rafiki yangu nikupendaye, Chochote kile ambacho unafanya sasa ni kama vile unaitengeneza hadithi yako. Kila mtu ana hadithi yake hapa duniani.Je, uko hapa duniani kutengeneza hadithi ya aina gani? Hadithi ni hadithi, je wewe umeamua kutengeneza hadithi ya aina gani kwenye maisha yako?Unatengeneza hadithi ya kushindwa au kushinda? Tengeneza historia ya maisha yako, jitume kwa …

Paka Anapaswa Kuwa Kwenye Chumba Muda Wote

Katika hali ya kawaida kila mmoja wetu anamfahamu paka, huwa paka akikaa ndani ya chumba ambapo kuna panya, panya huwa hawaonekani wanajificha na kutulia ili wasionekane.Ili panya asitawale, paka anapaswa kuwa ndani ya chumba muda wote. Hii ina maana gani kwetu? Kuna hali ambayo huwa inatokea katika maisha yetu ya kila siku, kama kiongozi akiwepo …

Design a site like this with WordPress.com
Get started