Wakati ukiwa unaumwa au kupitia magumu fulani kwenye maisha yako, watu wako wa karibu ndiyo wanakuwa watu wako wa kwanza kukusaidia kupitia kile unachopitia. Mtu mmoja katika familia akiumwa, basi familia nzima inakuwa inaumwa kwa sababu ile furaha ambayo watu walikuwa nayo inakuwa imepotea kabisa. Waheshimu sana watu ambao mnahusiana kama familia kwa sababu familia …
Sheria Za Kuwa Na Maisha Marefu Na Ya Mafanikio
Bilionea na mwekezaji Charlie's Munger ambaye kwa sasa ana miaka 99. Aliulizwa na mwandishi aseme siri za kuwa na maisha marefu na ya mafanikio.Moja ni usiwe na wivu. Wivu ni hali ya kujiona wewe una stahili kuliko mwingine.Ukiishi maisha ya wivu, hutaweza kufurahia maisha yako. Waache watu waishi vile wanavyotaka wao na wewe ishi vile …
Continue reading "Sheria Za Kuwa Na Maisha Marefu Na Ya Mafanikio"
Fanya Unachopaswa Kufanya
Kila mtu anajua kile anachopaswa kufanya kwenye maisha yake. Lakini je, ni wangapi wanafanya? Wewe mwenyewe unajua kile unachopaswa kufanya lakini hufanyi, unafikiri ni kwa nini hufanyi? Watu wanajua wanachopaswa kufanya lakini wengi wamekuwa na sababu nyingi za kutokufanya. Mfano mzuri wa jua, jua kazi yake ni kuwaka na linafanya hivyo kila siku bila kukumbushwa. …
Kuwa Mtu Unayeaminika
Kwenye maisha yako, kuwa mtu ambaye unategemewa na utajenga ushawishi mkubwa sana. Jihusishe na watu ambao wanaaminika tu. Ili uweze kuwa na maisha mazuri na marefu, unapaswa kujihusisha na watu ambao ni waaminifu na wanaoaminika. Ukishajenga tabia ya kuaminika, utawafanya watu wajenge utegemezi kwako. Watu wanapokuwa wanakutegemea maana yake unakuwa mtu ambaye una thamani kubwa. …
Hakustahili
Kama una ndoto kubwa halafu kuna mtu anakwenda kinyume na ndoto zako kwenye safari hii ya mafanikio makubwa, basi mtu huyo hakustahili. Unatakiwa kuwa na watu ambao watakuunga mkono kwenye kile unachofanya na siyo watu ambao wanakuwa wanakuvuruga.Usiogope kumpoteza mtu yeyote pale ambapo mtu huyo anakwenda kinyume na misingi yako uliyojiwekea. Rafiki yako ni yule …
Shida Yoyote Kwenye Maisha Inasababishwa Na Vitu Hivi Vitatu
Kadiri ya mfanyabiashara, mwekezaji na mwandishi Kevin O'Leary anasema kwenye maisha kuna wanaume, wanawake na fedha. Mwandishi anasema, shida yoyote kwenye maisha, inatokana na vitu hivyo vitatu. Kama husumbuliwi na mwanamke, basi mwanaume anakusumbua. Na kama kwa mwanamke na mwanaume uko vizuri basi fedha itakua inakusumbua. Kila mmoja wetu ana shida kwenye mahusiano yake au …
Continue reading "Shida Yoyote Kwenye Maisha Inasababishwa Na Vitu Hivi Vitatu"
Hii Ndiyo Safari Ya Kwanza Kwenye Kupata Fedha
Safari ya kwanza ya kupata fedha nyingi ni kuamua kwanza kiasi gani cha fedha unachotaka, muda utakaotumia kupata fedha hizo . Lakini pia, unapaswa kujua ni nini unapaswa kutoa ili kupata fedha hizo unazotaka. Kama unataka kuwa na fedha nyingi, unahitaji kuwa na mpango thabiti wa kupata fedha hizo na ujue kiasi gani cha fedha …
Continue reading "Hii Ndiyo Safari Ya Kwanza Kwenye Kupata Fedha"
Anza Na Wewe Kwanza
Kama kuna watu hawakupi kile ambacho wewe unataka kwenye maisha yako, anza kwanza wewe mwenyewe kujipa kitu hicho ambacho unataka kutoka kwao. Kwa mfano, kama unataka upendo kutoka kwa wengine, anza kwanza kujipenda wewe mwenyewe, penda kile unachofanya na kisha wapende wengine na utashangaa vile unavyotaka vitakuja vyenyewe. Kama watu hawakuamini, huna haja ya kuwalazimisha …
Sababu Ya Kuwa Na Maisha Magumu
Maisha tayari ni magumu kiasili, sasa lakini watu wanayafanya maisha kuwa magumu zaidi. Na maisha yanakuwa magumu pale ambapo watu hawafanyi kile wanachopaswa kufanya. Kama kila mtu angekuwa anafanya kila anachopaswa kufanya maisha yasingekuwa magumu. Kama kila mmoja wetu, akifanya kile anachopaswa kufanya, tutafanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi kwa kila mmoja wetu. Ukifanya …
Usinunue Matatizo Mengine
Rafiki yangu nikupendaye, Matatizo uliyonayo, tayari yanakutosha hivyo usinunue mengine. Muda uliokuwa nao kufanya vitu vya msingi ni mdogo mno. Ukisema uhangaike na kila kitu kwenye hii dunia basi utakufa haraka. Ukisema uhangaike na matatizo ya kila mtu hutaweza kuyamaliza. Kwanza matatizo ya watu, huwa yanamalizwa na watu wenyewe.Unaweza kuwa mtu wa huruma sana kusikiliza …