Maandalizi Bila Ufanisi

Maandalizi yoyote unayofanya kwenye maisha yako, hakikisha maandalizi hayo yana kitu kimoja muhimu ambacho ni ufanisi. Haina haja kuwa na maandalizi, halafu maandalizi hayo hayana ufanisi. Jitahidi sana unapojiandaa unakuwa na maandalizi yenye ufanisi. Na tunaposema ufanisi, maana yake viwango vimezingatiwa na ubora. Kwa maandalizi yoyote yale, jiandae vizuri na usifanye kitu juu na kushindwa …

Haya Ndiyo Makosa Mazuri

Kila mtu anakosea kwenye maisha yake. Na makosa mazuri ni yale ya kufanya kuliko kuliko kutokufanya. Ni bora kufanya kile unachopaswa kufanya kuliko kutokufanya. Unapofanya na ukakosea, kuna vitu utakavyojifunza na ukaviboresha zaidi. Ukifanya na ukakosea, hutaweza kurudia makosa hayo hayo wakati mwingine. Lakini, utafanya vizuri na kwa usahihi ili usirudie makosa. Usiogope kukosea, fanya …

Hii Ni Kwa Ajili Ya Waajiri Na Waajiriwa

Kama umeajiriwa unapaswa kufanya uwekezaji. Na watu wengi huwa wanasubiria wakishamaliza kustaafu au wakimaliza mkataba wa kazi basi wapewe fedha yao. Changamoto moja ni kwamba, hela za kwenye mifuko ya pesheni siyo za uhakika. Ni fedha ambazo ziko nje ya uwezo. Hata ukishastaafu, huenda usipate kwa muda unaotaka wewe. Na unakuwa unashida kweli, lakini huna …

Jinsi Ya Kukabiliana Na Hali Pale Mambo Yanapoenda Vibaya

Ni wazi kabisa mambo hayawezi kwenda kama vile unavyotaka wewe. Dunia haiwezi kwenda kadiri ya matakwa yako. Dunia inaenda kadiri ya vile inavyotaka. Mambo yanatokea kama yalivyopangwa kutokea. Unawezaje kukubaliana na mambo pale yanapokwenda vibaya? Jibu, ni wewe kutokwenda vibaya kama mambo yalivyoenda. Kumbuka, mambo yameenda vibaya usikubali na hayo mambo yakuendeshe na wewe uwende …

Huwa Anakuja Kukusaidia Ukiwa Unaumwa?

Wakati ukiwa unaumwa au kupitia magumu fulani kwenye maisha yako, watu wako wa karibu ndiyo wanakuwa watu wako wa kwanza kukusaidia kupitia kile unachopitia. Mtu mmoja katika familia akiumwa, basi familia nzima inakuwa inaumwa kwa sababu ile furaha ambayo watu walikuwa nayo inakuwa imepotea kabisa. Waheshimu sana watu ambao mnahusiana kama familia kwa sababu familia …

Sheria Za Kuwa Na Maisha Marefu Na Ya Mafanikio

Bilionea na mwekezaji Charlie's Munger ambaye kwa sasa ana miaka 99. Aliulizwa na mwandishi aseme siri za kuwa na maisha marefu na ya mafanikio.Moja ni usiwe na wivu. Wivu ni hali ya kujiona wewe una stahili kuliko mwingine.Ukiishi maisha ya wivu, hutaweza kufurahia maisha yako. Waache watu waishi vile wanavyotaka wao na wewe ishi vile …

Fanya Unachopaswa Kufanya

Kila mtu anajua kile anachopaswa kufanya kwenye maisha yake. Lakini je, ni wangapi wanafanya? Wewe mwenyewe unajua kile unachopaswa kufanya lakini hufanyi, unafikiri ni kwa nini hufanyi? Watu wanajua wanachopaswa kufanya lakini wengi wamekuwa na sababu nyingi za kutokufanya. Mfano mzuri wa jua, jua kazi yake ni kuwaka na linafanya hivyo kila siku bila kukumbushwa. …

Kuwa Mtu Unayeaminika

Kwenye maisha yako, kuwa mtu ambaye unategemewa na utajenga ushawishi mkubwa sana. Jihusishe na watu ambao wanaaminika tu. Ili uweze kuwa na maisha mazuri na marefu, unapaswa kujihusisha na watu ambao ni waaminifu na wanaoaminika. Ukishajenga tabia ya kuaminika, utawafanya watu wajenge utegemezi kwako. Watu wanapokuwa wanakutegemea maana yake unakuwa mtu ambaye una thamani kubwa. …

Hakustahili

Kama una ndoto kubwa halafu kuna mtu anakwenda kinyume na ndoto zako kwenye safari hii ya mafanikio makubwa, basi mtu huyo hakustahili. Unatakiwa kuwa na watu ambao watakuunga mkono kwenye kile unachofanya na siyo watu ambao wanakuwa wanakuvuruga.Usiogope kumpoteza mtu yeyote pale ambapo mtu huyo anakwenda kinyume na misingi yako uliyojiwekea. Rafiki yako ni yule …

Design a site like this with WordPress.com
Get started