Kushiriki Kikamilifu Na Kutaka Kuonekana

Kwenye matukio ambayo watu wengi wanashiriki, wengi wanakuwepo kwa madhumuni mawili.Moja, mwingine anashiriki kwenye jambo ili tu apate kuonekana kwamba ameshiriki.Na mwingine anashiriki kwenye jambo kikamilifu. Kushiriki kikamilifu maana yake akili yako yote inakuwa pale na kutekeleza yale yanayopaswa kufanywa kadiri ya mahitaji ya tukio. Kwa mfano, kuhudhuria nyumba za ibada, wako ambao wanaenda nyumba …

Maisha Ni Mahusiano

Ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote lile, unahitaji watu watakaokuwezesha kufanikisha jambo lako. Watu ambao watakuja kwenye jambo lako lolote lile, ni wale ambao umehusiana nao. Kwa mfano, unaenda kwenye harusi, send off ambayo tayari una mahusiano na wale ambao mnahusiana nao. Vitu vingi ambavyo vinatupita ni vile ambavyo hatuna mahusiano navyo. Kama unahusiana na …

Haya Ndiyo Mawazo Unayopaswa Kuyafikiria

Kila siku unapaswa kufikiria mawazo ya kujenga.Na kile unachofikiri ndiyo kinaamua ni nini utafanya. Kila unachofikiri kila mara ndiyo kitaamua ni wapi utakapoishia na maisha yako. Hii ndiyo sababu kubwa kwa nini ni muhimu sana wewe kushirikiana na watu wenye mawazo ya mafanikio. Tengeneza timu ambayo mtashirikiana na kusaidiana, utajitengenezea uhakika wa kufanikiwa. Maandalizi makubwa …

Vunja Tabia Mbaya

Ukivunja tamaa, unaweza kuondokana na tabia mbaya.Unafikiri nini kinachowafanya watu wengi kuendelea na tabia mbaya? Kinachowafanya watu wengi kuendelea na tabia mbaya ni kushindwa kuzuia tamaa zao, hasa pale zinapokuja kwa nguvu kubwa. Pale unaposalimu amri kwa tamaa zako ndiyo kitu kinachofanya tabia mbaya kuendelea kuwepo. Vunja tabia zinazokupelekea kwenye uraibu. Uraibu wa kukupeleka kwenye …

Wakikupa Hela, Watakupangia Hiki

Hapa duniani kila binadamu yuko katika maslahi yake binafsi.Watu huwa wanaangalia wanapata nini kwanza ndiyo wafanye kitu. Ni asili ya kila binadamu kuwa mbinafsi. Anaangalia kwanza yeye atapata nini. Ukiona mtu anafanya kitu, jua kuna maslahi binafsi anapata. Kwenye maisha unapaswa kuwa makini, watu wakikupa hela, basi watakupangia cha kufanya. Unakuwa mtumwa kwa watu hao. …

Usimkatie Mtu Tamaa

Kwenye maisha huwa tunawakatia tamaa watu wengi ambao tunahusiana nao. Tunawakatia tamaa na kuona kama vile wamefikia mwisho.Kuwakatia watu tamaa maana yake ni kama kuwawekea nukta kwamba hawawezi tena kuendelea. Tumegeuka kuwa miungu watu wa kuwawekea watu ukomo.Tunaona watu hawawezi kumbe wanaweza.Yako maeneo mengi ambayo tumewakatia watu tamaa kwenye maisha yao. Tunaona hawawezi tena.Kila mtu …

Njia Nzuri Ya Kutopuuzwa

Kila mtu anapenda kufanya kitu na kuonekana yuko vizuri. Ni jambo zuri kufanya kitu na kuonekana uko vizuri. Kama unataka usipuuzwe kwenye kitu chochote kile, kwanza fanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Ukiwa bora, hakuna atakayekupuuza hata siku moja.Mtu ambaye anafanya vitu vyake hovyo hovyo, mara nyingi huwa anapuuzwa. Na kitu kingine ni …

Ufukara Siyo Kilema

Kwenye maisha kuna vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako na kuna vitu ambavyo viko nje ya uwezo wako.Kuzaliwa masikini siyo kosa lako ila kufa masikini ndiyo kosa lako. Kama umezaliwa masikini, unapaswa kupambana kiasi kwamba ile hali ya umasikini iondoke kwako.Laana ya umasikini inaondolewa na kitu kimoja tu, nacho ni KAZI. Kama umasikini ni …

Kabla Ya Kutaka Kuongea, Jiulize Swali Hili Hapa

Mwanaidi Plato aliwahi kunukuliwa akisema, werevu huongea kwa sababu wana kitu cha kuongeza. Ila wapumbavu huongea kwa sababu inabidi waseme kitu. Wakati wowote ule unapotaka kuongea, jiulize swali hili,Jiulize je, una kitu cha kuongea au na wewe unataka usikike tu kwamba umeongea? Kwa kufanya hivyo, itakusaidia kujizuia kuongea mambo ambayo siyo ya muhimu. Kama huna …

Njia Bora Kabisa Ya Kuwaadhibu Wale Wenye Chuki Na Wewe

Ni kawaida ya binadamu kuchukiwa. Hakuna mtu ambaye hachukiwi kwa sababu kila anayeenda hatua ya ziada wale ambao hawapendi maendeleo yao lazima watawaonea wivu. Watu hawapendi kuonekana wameshindwa, watu hawapendi kuonekana wao ni wavivu au wazembe. Kinachotokea ni kwamba, kukufanya wewe usifikie ndoto zako ili muwe sawa. Wapo watu ambao watakuchukia kwa sababu ya mafanikio …

Design a site like this with WordPress.com
Get started