Bilionea Charlie Munger aliwahi kunukuliwa akisema, hakuna rubani makini, hata awe na kipaji na uzoefu kiasi gani, ambaye atapuuza nguvu ya orodha ya mambo ya kuzingatia.Kwenye kila kazi unayofanya, hakikisha unakuwa na nguvu ya orodha ya mambo ya kuzingatia.Ukiwa na orodha ya mambo ya kuzingatia, itakua kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Huwezi ukasahau, kwa sababu …
Hiki Ndiyo Chanzo Cha Hekima
Rafiki, Baba wa falsafa, mwanafalsa Socrates aliwahi kunukuliwa akisema, hekima pekee niliyonayo ni kwamba sijui kitu. Socrates ni mtu ambaye alikuwa anachukuliwa ni mtu mwenye hekima.Mtu anayejua lakini watu walishangaa pale alipoulizwa hekima yake na majibu aliyotoa. Pata picha, unaenda kwa mtaalamu wa kitu fulani halafu anakuambia, yeye anachojua ni kwamba hajui kitu utajisikiaje? Kujua …
Hii Ndiyo Dhambi Ambayo Hupati Raha Wakati Wa Kuifanya
Rafiki, Kuna watu huwa wanajisikia raha pale wanapoona wengine wakipitia magumu.Na hiyo ndiyo inakuwa furaha yao kuu. Na waswahili wanasema, Dua la kuku, halimpati mwewe.Ukiwa unawaombea wengine wapate mabaya, mabaya hayo hayawapati na huenda yakakurudia wewe mwenyewe. Dhambi ambayo watu wengi huwa hawapati raha wakati wa kuifanya ni wivu. Tukirejea kwa mtu mwenye hekima kutoka …
Continue reading "Hii Ndiyo Dhambi Ambayo Hupati Raha Wakati Wa Kuifanya"
Kitu Ambacho Kila Mwajiri Huwa Anapenda
Kiasili kila mmoja wetu ni mwajiriwa, kama umeajiriwa utawajibika kwa bosi wako na kama umejiajiri utawajibika kwa mteja wako.Kila mtu anawajibika kwa mtu. Hakuna ambaye hawajibiki kwenye haya maisha. Iwe umejiajiri au umeajiriwa. Kitu ambacho kila mwajiri huwa anapenda sana ni mtu ambaye anaweza kutatua matatizo na siyo anayesababisha matatizo. Kama umeajiriwa, jitahidi sana kupunguza …
Sheria Tatu Za Kazi
Kama unataka kufanikiwa kwenye kazi au biashara unapaswa kufuata sheria ambazo zitakuongoza. Ukiwa na sheria, wewe ni kuzizingatia na ili kupata matokeo mazuri. Sheria tatu za kazi kadiri ya hekima ya Bilionea Charlie Munger ni kama ifuatavyo; Moja, usiuze kitu ambacho wewe mwenyewe haupo tayari kukinunua. Mbili, usimfanyie kazi mtu ambaye humheshimu na kumkubali. 3. …
Jinsi Sheria Ya Louis Vincenti Inavyofanya Kazi Kwenye Maisha
Kwenye maisha huwa tuna mambo mengi. Na tunaongea na watu wengi kiasi kwamba hatuwezi kukumbuka kila ambacho tunaongea na mtu. Kwa kuwa tuna mambo mengi, hatuwezi kukumbuka kila kitu, hapo ndipo sheria ya Louis Vincenti. Tunaendelea na hekima za Charlie Munger, Munger anasema kwamba, sema ukweli na hutahitaji kukumbuka uongo wako. Kumbuka sheria ya Louis …
Continue reading "Jinsi Sheria Ya Louis Vincenti Inavyofanya Kazi Kwenye Maisha"
Hii Ndiyo Silaha Bora Ya Kuishi Maisha Ya Uzee
Mpendwa rafiki yangu nikupendaye, Watu huwa wanajua kwamba, wakifika uzeeni ndiyo wataishi maisha mazuri. Siyo, kama ukiwa mzee ndiyo utaanza kuishi maisha mazuri. Maisha mazuri ya uzeeni unapaswa kuanza kuyaishi sasa.Kila kitu kwenye maisha kinaanza sasa. Ni kila kitu unachotaka kwenye uzee wako, anza kukiandaa sasa hivi. Kama kwa sasa maisha yako yanakupiga, usifikirie ukiwa …
Continue reading "Hii Ndiyo Silaha Bora Ya Kuishi Maisha Ya Uzee"
Usiupoteze Mwaka Huu Kwa Namna Hii
Tunakaribia kuumaliza mwaka huu na kuingia mwaka mpya 2024. Mwaka huu ulikuwa na mipango na mawazo mazuri mengi.Yako ambayo uliyafanyia kazi na ambayo hujayafanyia kazi. Kila mwaka lazima ufanye kitu cha ushindi, usiache mwaka uishe bila kupata kitu cha ushindi. "Kila mwaka unaopita ambao hujaharibu moja ya mawazo yako pendwa ni mwaka ambao umeupoteza" Kama …
“Nimefanikiwa Kwa Sababu Hii”
Siku moja Bilionea Charlie Munger aliwahi kuulizwa kwa nini amefanikiwa, na jibu lake nilikuwa moja tu, Na alijibu hivi,"Nimefanikiwa kwa sababu nina uzingatiaji mkubwa kuliko wengine "Ukiangalia hiyo sentensi yake na wewe ukijaribu kwenye maisha yako, lazima utafanikiwa. Kwa sababu kwenye kila eneo la maisha yako, inakutaka wewe kuzingatia mambo fulani ili ufanikiwe.Kwenye eneo la …
Kama Unataka Kufanikiwa Tulia Hapa
Kila mtu anapenda kufanikiwa.Na kama kwenye maisha yako umeshajaribu vitu vingi na ukajikuta umejipata kwenye kitu fulani, shukuru Mungu na tulia hapo. Chochote kile ambacho kinafanya kazi vizuri kwako kirudie tena kukifanya.Kirudie kwa sababu kinakupa matokeo mazuri.Kitu ambacho kinakupa matokeo mazuri, endelea kukitumia na tulia hapo. Hakuna mtu ambaye anaweza kutabiri kwa usahihi kila wakati,Huwezi …