Mambo 13 Unayopaswa Kuyajua Kabla Ya Kufika Miaka 30

Mpendwa rafiki yangu, Mtu yeyote ambaye hana mwelekeo basi mwelekeo wowote humchukua, mtu mwa namna hii anakuwa hana tofauti na bendera. Mahali ambapo upepo unakwenda naye anaenda, usiwe mtu wa kuishi bila misingi sahihi ya maisha. Leo nakwenda kukushirikisha mambo 13 ambayo kila kijana anapaswa kuyajua na mambo hayo ni kama ifuatavyo. Kuwa na marafiki …

Hiki Ndiyo Kitu Kinachotusaidia Bila Hata Sisi Kujua

Natumaini imeshawahi kukutokea siku moja au mara nyingi umepanga kwenda sehemu fulani kwa muda fulani halafu likatokea jambo ambalo hata hukutegemea na ukajikuta umechelewa sehemu husika. Hiyo haitoshi, siku nyingine unajikuta unamuwaza rafiki yako au mtu fulani kabla hata hujajua la kufanya utashangaa yule mtu uliyekuwa unamuwaza anakupigia simu au kuja nyumbani uliko na unamwambia …

Sababu Kuu Moja Kwanini Unatakiwa Ujisukume Wewe Mwenyewe

Mpendwa rafiki yangu, Katika maisha yetu ya kila siku jifunze kujitegemea, tunapokuwa tunajitegemea katika mambo yetu ni ngumu watu wa nje kutuangusha. Unatakiwa kutambua kuwa jukumu la maisha yako ni lako mwenyewe hivyo usisubiri watu waje wakupambanie. Je kwanini unatakiwa ujisukume mwenyewe  au ujitume? Iko sababu kuu moja ambayo imenihamasisha siku hii ya leo nikuandikie …

Kwenye Kila Ushindi Unaoujua Wewe Kuna Kitu Hiki Cha Kujifunza

Mpendwa Rafiki yangu, Mpaka tunaona kazi yoyote imekamilika basi jua kuwa kuna mchakato mkubwa umefanyika. Mafanikio yoyote uliyopata au unayotegemea kuyapata yana mchakato wake. Watu wengi wanapenda kufurahia mafanikio lakini hawapendi kusikia mchakato wa mafanikio. Sasa kwenye kila ushindi wowote ule unaoujua wewe kuna kitu muhimu sana cha kujifunza. Kitu hiko siyo kingine bali ni …

Kitu Pekee Duniani Ambacho Hakuna Anayeweza Kukihodhi Au Kukimiliki Hata Awe Nani

Ni kawaida yetu sisi binadamu kupenda kuhodhi au kumiliki vitu mbalimbali, wapo ambao wanamiliki ardhi, nyumba na mali nyingine. Tunayo nguvu ya kumiliki vitu vyote lakini kuna kitu kimoja ambacho sisi binadamu hatuwezi kukimiliki. Aliyekuwa mwanafalsafa wa ustoa Seneca aliwahi kunukuliwa akisema, ‘’ ukweli hauwezi kuhodhiwa, yeyote anayetafuta ukweli ataupata.’’ Rafiki, kitu pekee ambacho hakuna …

Jinsi Ya Kukabiliana Na Mtu Asiyejielewa

Rafiki, Siyo kila mtu unayekutana naye anajielewa na kujitambua. Tunakutana na watu wa aina mbalimbali kuna wengine wana hekima na kuna wengine hawana kabisa hekima wala busara. Kuishi na watu ni kazi sana kwa sababu kila mtu ana mitazamo yake. Ukitaka kuishi vile watu wanavyotaka hapo utakua unaishi maisha ya kuwafurahisha watu ambayo ni kazi …

Jinsi Ya Kuwa Na Utulivu Wa Akili

Mpendwa rafiki yangu, Akili zetu zinapokuwa na amani na utulivu basi zinaweza kufanya kazi vizuri sana. Kama ukiishi bila kuwa na utulivu wa akili itakupelekea kufanya mambo ya ajabu usiyoyategemea. Tukiwa na utulivu wa ndani tutaweza kufanya kazi zetu kwa viwango vya juu sana, hivyo basi ni namna gani unaweza kuwa na utulivu wa akili? …

Haya Ndiyo Maandilizi Muhimu Unayopaswa Kuwa Kwenye Maisha Yako

Maisha ni maandalizi. Hivyo unatakiwa kujiandaa na maandalizi kwenye kila eneo la maisha yako. Isifikie mahali sasa ukaridhika na kile ulichonacho. Dunia siyo mti au jiwe kwamba halikui wala halisogei bali dunia inakuwa na kubadilika kila siku. Mambo yanabadilika kila kukicha, kama matumizi ya kifedha yanapanda na wewe unatakiwa kubadilika kuongeza kipato. Hutakiwi kukaa chini …

Huu Ndiyo Uhai Wa Kila Biashara

Rafiki, Kama unafanya biashara basi kuna eneo moja ambalo unatakiwa kulifanyia kazi kila siku ya maisha yako. Kila mtu ni mfanyabiashara kiasili kwa sababu biashara ni mfumo wa kubadilishana thamani, kama umeajiriwa kuna kitu una uza ambacho ndicho ujuzi wako. Kwa namna yoyote ile sisi wote ni wauzaji wa kitu fulani. Uhai wa biashara uko …

Huu Ndiyo Mfumo Mzuri Wa Mafanikio Wa Kuishi Kila Siku

Tumekuwa ni kama wakulima ambao wanapanda leo na kesho wanafukua hata kabla mbegu haijaota. Hebu chukulia mfano, mkulima anapanda leo mbegu ya mahindi kesho anaifukua na kutaka tena kwenda kupanda kitu kingine. Je kwa mtindo huu, unafikiri ataweza kufanikiwa kweli? Ataweza kuona hata mbegu ikichipua? Hawezi kuiona, unapopanda unatakiwa uwe na subira mbegu ikae chini …

Design a site like this with WordPress.com
Get started