Rafiki,
Siyo kila mtu unayekutana naye anajielewa na kujitambua. Tunakutana na watu wa aina mbalimbali kuna wengine wana hekima na kuna wengine hawana kabisa hekima wala busara. Kuishi na watu ni kazi sana kwa sababu kila mtu ana mitazamo yake.
Ukitaka kuishi vile watu wanavyotaka hapo utakua unaishi maisha ya kuwafurahisha watu ambayo ni kazi ngumu hutokuja kuiweza. Ukitaka kumfurahisha kila mtu maana yake umejiandaa kushindwa kwani hakuna kila mtu ambaye atakubaliana na wewe kwenye kila kitu na huwezi kumpa kila mtu kile anachotaka.
Je ni namni gani sasa unaweza kuishi na watu wasiojielewa, wasiokuwa na busara, hekima, misongo ya mawazo na mengine yanayohusiana na wewe?
Unatakiwa kuwa makini sana kwa sababu kuna watu wana matatizo yao,hivyo huwa wanatafuta mtu wa kumuuzia matatizo yao, wanataka wewe uwe kama wao. Sasa njia moja ya kukabiliana na mtu ambaye unaona hajielewi kwenye maisha yake ni wewe kutokua kama yeye.
Kwa mfano, mtu akikujibu majibu ya hovyo hutakiwi kumjibu na unakaa kimya na kumpuuzia. Mtu akikunyamazia kwa sababu mligombana hutakiwi kuwa kama yeye, kama yeye anaishi kwa kinyongo wewe usiwe na kinyongo msalime na muoneshe upendo.
Unatakiwa kuwa kinyume kabisa na adui yako kama mtu anakuchukua wewe usimchukie bali muoneshe upendo, unapokuwa unamuonesha upendo atakuwa anajiuliza maswali mengi, iweje mtu huyu mimi namfanyia ubaya na yeye ananifanyia upendo? Taratibu na yeye ataanza kubadilika, lakini ukisema uwe na wewe unamrudishia ubaya hutoweza kumsaidia kamwe.
SOMA; Kisasi Kizuri Kwa Adui Yako
Ukitaka kumsaidia masikini njia rahisi ni wewe kutokua masikini. Badilika wewe, anza kuwa vizuri kimaisha ndiyo utaweza kumsaidia yule ambaye hajiwezi, jiandae kwanza wewe mwenyewe kabla hujawaandaa wengine.
Anza kujipenda wewe kabla hujawapenda wengine, utawezaje kusema unapenda wengine halafu wewe mwenyewe hujipendi? Utaweza kuwahamasisha watu kama wewe unafanya tofauti na wale unaowahamasisha.
Hatua ya kuchukua leo; nenda kinyume na vile watu wanavyoishi, usiishi mazoea bali kuwa kinyume usiwe kama wao na usiishii kadiri ya mkumbo wa jamii bali ishi maisha yako.
Hivyo basi, kila unachoishi lazima kikusaidie,kile unachokiamini lazima kikusaidia na ukiona havikusaidii huenda unaishi nadharia kuliko vitendo.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl, Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com
Asante Sana