Kama Tatizo Lako Linatatuliwa Na Fedha Basi Jua Tatizo Lako Ni Hili Hapa

Ukichunguza matatizo mengi tuliyonayo chanzo kimoja ni fedha. Hata matatizo mengi uliyonayo siyo kwamba ni matatizo makubwa sana bali kuna kitu kinachangia wewe kuwa hivyo.Kumbe basi, matatizo mengi watu waliyonayo yanasabishwa na ukosefu wa fedha. Kama una matatizo, halafu tatizo lako linaweza kutatuliwa na fedha basi wewe huna tatizo hapo, Bali tatizo lako ni fedha …

Haya Ndiyo Mambo Mawili Yanayoweza Kutokea Katika Maisha Yako

Heri ya mwezi agasti, Unapopata muda wa kujitathimini katika kile unachofanya kila siku mambo hayawezi kwenda kama vile ulivyopanga au vile unavyotaka wewe. Hivyo basi, katika maisha yetu pale mambo yanapokwenda ndivyo sivyo hata usijilaumu sana bali pokea na shukuru jifunze kwa kile kilichotokea. Wakati mwingine huwa tunajiaandaa na ushindi ,tunapanga mambo yetu kama vile …

Njia Ya Kufikia Malengo Yako Ya Kifedha

Katika saikolojia ya mauzo, mwandishi Brian Tracy ameshirikisha mbinu nyingi za kufanikiwa kimauzo.Kila mmoja kuna kitu anauza hata kama huna biashara kuna kitu unauza ndiyo maana unayaendesha maisha yako kwa mfano, unaweza kusema mimi siyo mfanyabiashara hivyo basi sina haja ya kujifunza mauzo, hapana unatakiwa kujifunza mauzo kika siku kwani mauzo ndiyo yanamfanya kila mtu …

Njia Rahisi Ya Kupunguza Matatizo

Huwa tunafikiri kuwa tunaweza kumaliza matatizo yetu, hapana hatuwezi kumaliza matatizo yetu kama tunaendelea kuishi hapa duniani. Kuepuka matatizo ya duniani ni kuondoka duniani ila kama unaishi changamoto ni sehemu ya maisha kama vile unavyokula kila siku huli mara moja na kusema huli milele bali kila siku. Hutatui changamoto moja na kusema umemaliza changamoto zote, …

Pale Mtu Anapokushinda Mwache Awe Hivi

Kuna wakati unajikuta unachoka pale unapokuwa unamsaidia mtu kuwa katika mstari na yeye wala haelekei. Wako ambao tuko nao katika mahusiano ya kindugu wamekuwa ni watu ambao hawaambiliki kabisa. Unakuwa mpatanishi sana wa kusuluhisha lakini inafikia mahali kibinadamu unachoka. Inapotokea kupishana kauli na mtu, mkaombana msamaha nyie kwa nyie, akawa hataki, mkamshirikisha mtu mwingine mpaka …

Jinsi Ya Kupata Utulivu Wa Akili

Mara nyingi huwa tunatengeneza tabia kisha tabia zinatutengeneza sisi, siyo tu tabia bali pia hata matatizo huwa tunatengeneza sisi wenyewe hata furaha pia. Kwa mfano, watu wakijua kesho kuna sherehe ya kitu fulani basi watatengeneza furaha ya sherehe hiyo na kweli katika tukio hilo utawakuta watu wanafurahi kweli. Ila ikitangazwa kesho ni siku ya kutoa …

Usitake Usichokuwa Nacho

Na shida yetu kubwa sisi binadamu iko hapa, tunapenda kutamani au kutaka vile ambavyo hatuna na matokeo yake tunakuja kusahau hata vile ambavyo tunavyo. Tunaweza kuwa na kile ambacho tunacho, lakini hatukitumii vizuri sana badala yake tunajikuta tunatamani vile ambavyo hatuna. Ulichonacho kinatosha kama ukifikiria vya kutosha. Badala ya kuangalia vile ambavyo huna hebu anza …

Hii Ndiyo Dhambi Unayopaswa Kuacha Kuitenda

Ukichunguza ndani ya mioyo yetu, utakutana watu wengi wana dhambi moja ambayo inawamaliza watu wengi katika zama hizi. Na dhambi hiyo siyo nyingine bali ni kulalamika. Tumekuwa ni watu wa kuwalalamikia wengine hata kama makosa ni ya kwetu kabisa tunakataa kukubali kukosa na tunatafuta ni nani ambaye tunaweza kumsingizia. Binadamu tunayo asili ya ukaidi, hii …

Tarajia Mazuri Lakini Tegemea Hiki

Hakuna mtu mwenye uhakika wa kitu chochote katika maisha yake zaidi ya kifo. Tunapanga mipango mingi lakini hatuna uhakika wa kufanikiwa mipango tuliyopanga. Falsafa ya ustoa inatualika sisi sote kama binadamu tupange mambo makubwa lakini tutarajie kinyume chake pia. Yaani chochote tunachokipanga tujiandae na matokeo yoyote yale. Umepanga kupata mazuri sawa, tegemea na kinyume cha …

Jiandae Kuishi Maisha Haya

Hivi ulishawahi kujiuliza maisha yako yatakuwaje kama usipokuwa na kile ambacho unacho sasa? Vipi cheo au wadhifa ulionao sasa ukinyang'nywa ghafla itakuwaje? Ulishawahi kujiandaa kuishi maisha ya kinyume cha kile unachoishi sasa? Yaani kama kwa sasa una kazi je ulishawahi kuishi maisha ambayo kama mtu ambaye hana kazi? Umejiandaaje na yale maisha ambayo hukuyategemea kuyaishi? …

Design a site like this with WordPress.com
Get started