Kuna wakati unajikuta unachoka pale unapokuwa unamsaidia mtu kuwa katika mstari na yeye wala haelekei. Wako ambao tuko nao katika mahusiano ya kindugu wamekuwa ni watu ambao hawaambiliki kabisa.
Unakuwa mpatanishi sana wa kusuluhisha lakini inafikia mahali kibinadamu unachoka. Inapotokea kupishana kauli na mtu, mkaombana msamaha nyie kwa nyie, akawa hataki, mkamshirikisha mtu mwingine mpaka mkafikia hatua ya juu kabisa na hataki kusamehe wewe wala usijusumbue kama tayari umeshatimiza wajibu wako.
Pale mtu anapokushinda mwache awe mtu wa mataifa, iachie asili ipambane naye kama unaona umefikia mwisho na mtu hataki kubadilika.
Kadiri ya mienendo yetu ya maisha wakati mwingine tunajikuta kuwa kero kwa kuwakwaza wengine. Usipoteze muda mwingi kumbadilisha mtu kwani watu wanaamua kubadilika pale wanapotaka wenyewe na kadiri unapomfosi mtu kubadilika ndiyo anazidisha ile tabia ambayo huipendi kutoka kwake.
Asili ina namna yake ya kuwabadilisha watu, hivyo kama mtu amekushinda kaa pembeni mwachie Mungu au asili itamrekebisha.
Hatua ya kuchukua leo; siyo lazima kupambana na kila kitu, ukiona kitu au mtu amekushinda baada ya kutimiza wajibu wako jiweke pembeni na iachie asili ipambane naye kwani asili ina namna yake ya kuwabadilisha watu.
Kwahiyo, kubadilisha watu ni kazi ngumu ambayo hutoiweza, kazi yako kubwa ni wewe kuishi kikamilifu kila siku, kuishi vile ambavyo unapaswa kuishi hata wale wanaotaka kubadilika watajifunza kutoka kwako.
Wakati mwingine maisha yetu ni vitabu, hivyo kuwa mtu wa kusoma vema yale ambayo ni mazuri kutoka kwa mtu na kile ambacho hakikusaidi achana nacho wewe pambana na vile ambavyo viko ndani ya uwezo wako.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana
©Kessy Deo