Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kupata Utulivu Wa Akili

Mara nyingi huwa tunatengeneza tabia kisha tabia zinatutengeneza sisi, siyo tu tabia bali pia hata matatizo huwa tunatengeneza sisi wenyewe hata furaha pia.

Kwa mfano, watu wakijua kesho kuna sherehe ya kitu fulani basi watatengeneza furaha ya sherehe hiyo na kweli katika tukio hilo utawakuta watu wanafurahi kweli.

Ila ikitangazwa kesho ni siku ya kutoa mapepo, wale ambao wanaalikwa kwenda huko wataanza kujitengenezea mapepo kiakili na mpaka inafika siku hiyo husika , mtu ameshatengeneza hofu kubwa ya kiakili kwamba yeye ana mapepo hivyo basi, hali ya kutotulia kiakili inamchanganya kirahisi hatimaye kuvurungwa.
Kwanini? Unakuwa kile unachofikiri, wewe ni kile unachofikiri muda mrefu.

Kama unataka kujenga utulivu wa akili, tafadhali jiepushe na vitu vyote vinavyokupa hofu, vinavyokupa msongo wa mawazo.

Mtu ambaye yuko kijijini ambaye hafuatilii kitu chochote kinachoendelea duniani hawezi kuwa na msongo wa mawazo kama yule ambaye yuko mjini ambaye kila habari anataka isimpite, kwa namna hii lazima atakosa utulivu wa akili.

Jitenge na vitu vinavyokupa hofu na utabaki kuwa na utulivu wa akili. Ishi tu kadiri ya asili, hebu mwangalie mtoto mdogo hana hofu kwa sababu hana taarifa za hofu alizojaza ndani yake.

Sikiliza, angalia , soma kile ambacho kinakupa au kujitengenezea mazingira ya kuleta furaha yako. Kamwe usiambatane au usisikilize vitu ambavyo vinafanya ukose utulivu wa akili.

Wakati mwingine jitoe kwenye mambo ya kidunia na rudi katika asili, pata muda wa kupumzika vizuri na utakua na utulivu wa akili kuliko kujihangaisha na kila kitu kinachopita kwenye siku yako.

Hatua ya kuchukua leo; Unapata kile unachotafuta, hivyo basi, jiondoe kwenye mazingira yanayokufanya ukose utulivu wa akili na jiweke katika mazingira yanayokupa utulivu wa akili.
Epuka habari hasi, na kuwa mtu wa vitu chanya tu vinavyokusaidia wewe kupiga hatua kubwa.

Kwahiyo, wewe ndiyo unahusika katika utulivu wa akili yako, ujivuruge au usijivuruge. Wakati mwingine ukiingia ndani katika sala, kufanya tahajudi na kujiepusha na vitu vya hofu huwezi kuwa na kuhofia chochote kile.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz  

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: