Asiyehusika Atoke Nje

Huwa tunajeruhiana katika mengi. Muda mwingine huwa tunawakwaza wengine pasipo hata sisi kujua kadiri ya mienendo yetu ya maisha. Kila mmoja wetu ana majeraha yake ya moyo, ambayo akikaa chini na akikumbuka mapito aliyopita anahisi kupatwa na uchungu na kupelekea kulia. Usifiche hisia pale unapohisi kupatwa na uchungu unapokumbuka mapito uliyopita. Unapohisi kulia lia kabisa …

Hii Ndiyo Faida Ya Kukutana Na Mtu Yeyote Yule

Natumaini ulishawahi kusafiri, ulishawahi kwenda kwa rafiki yako na maeneo mengi uliyotembelea hukubaki kama ulivyokuwa hapo awali. Mara nyingi pale unapokutana na mtu mwingine au unapoenda sehemu huwa unajifunza kitu cha kwenda kukifanyia kazi kwenye maisha yako. Kila mtu unayekutana naye anakuwa na kitu cha kukufundisha na hii ndiyo faida kubwa ya kukutana na mtu …

Jenga Utaratibu Huu Wa Kihistoria Kwenye Maisha Yako

Hakuna juhudi yoyote utakayoiweka na kwenda bure. Asili huwa inatabia ya kulipa juhudi ya kila mtu hata kama hujalipwa leo ila utalipwa tu. Juhudi ya mtu huwa haipotei hata siku moja hivyo endelea kuweka juhudi na iko siku dunia itakupa kile unachotaka kwenye maisha yako. Watu wengi wanaofanikiwa sana ni wale watoaji. Wale wanaotoa juhudi …

Jinsi Ya Kupunguza Uwezekano Wa Kushindwa

Hakuna mtu ambaye hashindwi katika maisha yake. Kila mtu anashindwa. Lakini anayeshindwa zaidi ni yule mtu anayeshindwa na kuishia kukatia tamaa pale pale bila kuendelea. Katika safari ya mafanikio hakuna kushindwa bali kuna kujifunza hivyo unaposhindwa unakua unajifunza. Je namna gani unavyoweza kupunguza uwezekano wa kushindwa kwenye chochote kile unachofanya? Jawabu; unaweza kupunguza uwezekano wa …

Usikubali Siku Yako Ipite Bila Kupata Ushindi Wowote Ule

Hakuna anayelala na kujua kesho yake itakuwaje, licha ya kuamini mambo yatakuwa mazuri lakini hili ni jambo ambalo liko nje kabisa ya uwezo wetu. Hatuwezi kujua leo tutakutana na changamoto gani, hivyo basi pale tu unapoamka hakikisha unajihakikishia ushindi ili siku yako isiende bure.Yako mambo mengi ambayo unaweza kujihesabia ushindi kabla hujaenda kuwatumikia wengine. Kwa …

Haya Ndiyo Madhara Ya Utoaji Wa Huduma Ya Hovyo

Kila mmoja wetu ni mtoa huduma yaani kila mtu kuna kitu anauza kwa mwingine kwa lugha rahisi.Kwa sababu sisi ni binadamu na tunaishi kwa kutegemeana. Kama ulikuwa hujui asilimia 85 ya mafanikio yako yanatoka kwa wengine na asilimia 15 tu inatoka kwako.Kwa maana hiyo basi, hata useme wewe ni jeshi la mtu mmoja ni ngumu …

Jitafakari, Je Kile Unachofanya Kitaweza Kukufisha Hapa?

Ni vema ukajitafakari mapema kama kile unachofanya kitaweza kukufikisha kule unakotaka kufika. Kila mmoja ana ndoto zake na kufanikiwa inategemea na kile unachofanya. Viko vitu vingine unavyofanya vinachangia kujirudisha nyuma. Kuna vitu kweli ukivifanya kwa hakika vitakurudisha nyuma na kuna vitu ambavyo ukivifanya vitakupeleka mbele. Ni muda wa kujipima kama kile unachofanya kweli kinakulipa? Na …

Huyu Ndiye Mwalimu Wa Vitu Vyote

Kila mtu anakuwa mgeni kwenye baadhi ya maeneo katika maisha yetu.Huwezi kuwa mwenyeji kwenye kila kitu. Kuna maeneo utakua vizuri na kuna maeneo hautakua vizuri lazima utawategemea wengine. Kila mtu anamtegemea mwingine ili maisha yake yaweze kwenda. Hakuna ambaye hamtegemei mwingine kwa sababu sisi ni viumbe vya kutegemeana. Kila ambaye alifikia kwenye ubobezi hapo mwanzo …

Njia Moja Ya Kuwa Na Maisha Mazuri Kati Njia 52

Mwandishi wa kitabu njia 52 za kuwa na maisha bora mwandishi Rolf Dobeli ametushirikisha katika kitabu chake. Kwenye kitabu cha Tano za Juma alichoandika mwandishi Makirita Amani ameweza kukichambua vizuri na hapa mimi leo ninakushirikisha njia moja ya kuwa na maisha mazuri. Njia hiyo ni, " Unachoona kwa wengine na kukitamani, siyo bora kama unavyofikiria. …

Fedha Hazina Kitu Hiki Kimoja

Fedha ni jawabu la mambo yote kadiri ya kitabu cha mhubiri. Hakuna anayeweza kubisha kwamba fedha siyo ya muhimu ni muhimu kwani inatusaidia kupata kile tunachotaka. Fedha ni zao la thamani, kadiri unavyotoa thamani zaidi na wewe kipato kinaongezeka. Yaani ukitoa thamani zaidi na fedha inaongezeka. Ni kama vile unavyotoka jasho maana yake nishati inatoka …

Design a site like this with WordPress.com
Get started