Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usitake Usichokuwa Nacho

Na shida yetu kubwa sisi binadamu iko hapa, tunapenda kutamani au kutaka vile ambavyo hatuna na matokeo yake tunakuja kusahau hata vile ambavyo tunavyo.

Tunaweza kuwa na kile ambacho tunacho, lakini hatukitumii vizuri sana badala yake tunajikuta tunatamani vile ambavyo hatuna.

Ulichonacho kinatosha kama ukifikiria vya kutosha. Badala ya kuangalia vile ambavyo huna hebu anza kuangalia vile ambavyo unavyo umevitumiaje na kukusaidia? Waswahili wanasemaje? Fimbo ya mbali haiui nyoka, kumbe basi kile ambacho unacho sasa ndiyo kinaweza kukusaidia kama ukitumia vizuri.

Aliyekuwa mwanafalsafa wa ustoa Seneca, anatuambia kwamba hakuna mtu mwenye nguvu ya kupata kila anachotaka kuwa nacho, lakini kila mtu ana nguvu ya kutokukata kile ambacho hana na kuchagua kutumia vizuri kile ambacho anacho.

“No person has the power to have everything they want, but it’s in their power not to want what they don’t have, and to cheerfully put to good use what they do have” Seneca.

Hatua ya kuchukua leo; acha kuangalia umekosa nini, Bali angalia una nini ambacho unacho tayari mkononi cha kuweza kufanya kitu.
Angalia kile ambacho unacho kusaidia kuongeza thamani kwa wengine na hatimaye kuweza kupata kile unachotaka.

Hivyo basi, usitake usichokuwa nacho, tumia vizuri sana kile ambacho unacho kupata kile unachotaka. Kumbuka, ulichonacho kinatosha kama ukifikiria vya kutosha.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz  

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: