Ukichunguza ndani ya mioyo yetu, utakutana watu wengi wana dhambi moja ambayo inawamaliza watu wengi katika zama hizi.
Na dhambi hiyo siyo nyingine bali ni kulalamika. Tumekuwa ni watu wa kuwalalamikia wengine hata kama makosa ni ya kwetu kabisa tunakataa kukubali kukosa na tunatafuta ni nani ambaye tunaweza kumsingizia.
Binadamu tunayo asili ya ukaidi, hii tunaiona hata kwa Adam na Hawa, alipoulizwa kwanini umekula tunda akajibu si huyu mwanamke uliyenipa, Hapa tunaona namna anavyojitetea kama yeye hastahili kosa bali mwenzake ndiyo anastahili kosa.
Ifikie mahali tuwe watu wa kukubali makosa yetu tunayofanya na kuacha kulalamika au kuwalalamikia wengine kama ndiyo wanahusika na makosa yetu.
Kwanini watu wengi wanalalamika? Watu wengi wanalalamika kwa sababu ya kukosa fadhila ya kushukuru. Ukiwa ni mtu wa kutoshukuru kwa kila jambo kila kitu unatakiona hakipo sawa kwako.
Mtu anakosa shukurani kwa kile ambacho anacho, anaanza kujilinganisha na wengine na matokeo yake anajiona hafai na hapo ndiyo anazidi kutafuta watu ambao wamesababisha yeye awe hivyo alivyo.
Hivi ni nani akitafuta mtu wa kumlaumu kwa maisha yake yeye kuwa hivyo yalivyo au mambo kumuendea vibaya atamkosa? Jibu ni hakuna.
Sasa basi, kuanzia leo jiambie kuwa jukumu la maisha yako ni lako mwenyewe, mambo yaende vizuri au vibaya hakuna mtu mwingine wakuwajibika isipokuwa wewe mwenyewe.
Pambana na hali na shika hatamu ya maisha yako kwani wewe ndiyo unawajibika kwa asilimia zote juu ya maisha yako.
Acha tabia ya kulalamika na kuwa mtu wa kushukuru. Unaposhukuru unakuwa unaona makuu mengi anayokutendea Mungu lakini ukiwa ni mtu wa kulaumu utaona uhaba mwingi katika maisha yako na hujakamilika lakini kushukuru unaona utele.
Hatua ya kuchukua leo; Kushukuru ni kuomba tena, badala ya kuwa mlalamikaji kuwa mtu wa kushukuru kwa kile ambacho unacho, kwa matokeo yoyote yale bila kumlaumu yeyote. Kinachokuja mbele yako uwe umekosea au hujakosea jua hilo ni lako wajibika nalo.
Kwahiyo, utamaduni wa kulalamika unazaa wavivu wengi, watu wanashidwa kufanya kazi na kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yao huku wakitumia muda mwingi kwenye kulalamika.
Ni nani aliyefanikiwa kwa njia ya kulalamika? Hakuna, usiwe hata mtu wa kulalamikia kifo, kwani ni nani aliyekuambia mtu ataondoka hapa duniani akiwa hai? Kila anayeondoka hapa duniani anaondoka akiwa amekufa hivyo tukipokee kifo kama asili ya kila mwanadamu na siyo kulalamika.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana
©Kessy Deo