Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Rahisi Ya Kupunguza Matatizo

Huwa tunafikiri kuwa tunaweza kumaliza matatizo yetu, hapana hatuwezi kumaliza matatizo yetu kama tunaendelea kuishi hapa duniani.

Kuepuka matatizo ya duniani ni kuondoka duniani ila kama unaishi changamoto ni sehemu ya maisha kama vile unavyokula kila siku huli mara moja na kusema huli milele bali kila siku. Hutatui changamoto moja na kusema umemaliza changamoto zote, bali changamoto ni kama mtihani, ukimaliza wa darasa moja lazima utafanya wa darasa lingine ili upige hatua zaidi.

Sasa ipi ni njia rahisi ya kupunguza matatizo?
Njia rahisi ya kupunguza matatizo ni kufikiria mitazamo chanya tu. Unajua wakati mwingine mitazamo hasi au mawazo hasi ni sumu, mawazo hasi tunayokuwa nayo huwa tunajitengenezea sumu sisi wenyewe kiakili, kimwili na kiroho.

Usiwe mtu wa kufikiria mitazamo hasi, bali kuwa mtu wa kufikiri mambo mazuri tu, yaani unajitoa katika mazingira ambayo unajua yanaweza kukupa matatizo.

Wewe ni kile unachofikiri, sasa kama ni hivyo kwanini usiwe unafikiri kile unachotaka? Huoni ukiwa unafikiri mambo chanya itakusaidia kupunguza matatizo?

Kuwa mtu wa kupambana na yale ambayo yako ndani ya uwezo wako. Yale ambayo yako nje ya uwezo wako yatakuletea shida tu. Na hii ni moja ya njia ya kukufanya kuwa na utulivu wa akili.

Sisi binadamu tunayo tabia ya kutengeneza matatizo sisi wenyewe kisha matatizo yanatutengeneza. Kuwa mtu wa kupotezea maana ukisema ukomae na vitu ambavyo havina maana vitakuondoa kwenye uwepo wako.

Hatua ya kuchukua leo; Acha kufikiri vitu hasi, fikiri mambo chanya nayo yatakusaidia kukupunguzia matatizo.
Wewe ni kile unachofikiri, sasa unapofikiria chanya ni rahisi kufanikiwa na kupunguza matatizo yasiyokuwa ya lazima.

Fanya kile ambacho kinakupa furaha, angalia, sikiliza wimbo unaopenda ila siyo za huzuni bali za furaha. Kikubwa fanya kile unachopenda kitakuchochea kuwa mtu mwenye furaha na kupunguza matatizo, maisha yetu ni mafupi, ukijipa shida sana utakufa bila kufurahia kile ambacho unacho.

Kwahiyo, jitoe kwenye vitu ambavyo vinakupa msongo wa mawazo, lakini pia iruhusu akili yako kufikiri vitu chanya, kuwa na hisia za upendo badala ya kuwa na hisia za hofu maana hisia za hofu zinaa vitu kama wivu, chuki, hasira na hivi hupelekea matatizo kwa mtu.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz  

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: