Shughuli Na Maeneo Unayopaswa Kuyapa Kipaumbele

Kila mmoja wetu anajua ni maeneo gani yuko vizuri sana na maeneo gani hayuko vizuri. Kwa kulijua hilo, tunapaswa kuyapa kipaumbele yale maeneo ambayo yanafanya vizuri sana. Shughuli na maeneo unayopaswa kuyapa kipaumbele sana ni yale yanayokupa furaha. Shughuli na maeneo yanayokupa furaha ndiyo unayopaswa kuyapa kipaumbele zaidi. Usiendelee kujisumbua na mambo mengi. Tulia na …

Linda Vitu Hivi Viwili Ili Kupata Ufanisi

Watu wote duniani tuko sawa na kinachotufanya tuwe sawa ni masaa 24 kwa siku tuliyopewa. Lakini, ndani ya hayo masaa 24, kuna ambao wanafanikiwa kufanya makubwa na wako ambao wanashindwa kufanikiwa. Ili uweze kuwa na ufanisi kwenye siku yako, zingatia mambo haya mawili. Linda akili yako. Usiingize uchafu kwenye akili yako. Kumbuka, unatoa kile unachoingiza. …

Badili Mtazamo Huu Kama Unataka Kufanikiwa Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako

Watu wengi wamekuwa na mtazamo mbaya sana ambao unawafanya wasifanikiwe. Kwa mfano, wana mtazamo wa kuchukua au kupewa zaidi kuliko wanavyotoa. Kwa chochote kile ambacho watu wanafanya huwa wanajiandaa na kujiangalia kwanza wao wananufaikaje. Watu hawajali wanawanufaishaje wengine. Kwa mfano, kwa hali kama hii ndiyo maana ukiritimba, rushwa na ufisadi unaendelea kuwepo sehemu nyingi kwa …

Jiulize Swali Hili Kila Wakati

Tuko katika zama za mambo mengi ukilinganisha na muda tulionao. Usipokuwa na misingi sahihi inayokuongoza utajikuta una hangaika na kila kitu, kila kitu kinakuwa ni kipaumbele kwako. Hebu fikiria kwa jinsi mambo yalivyokuwa mengi, na muda ni mdogo kila kitu ukikifanya ni kipaumbele kwako utaweza kufanikisha hata kimoja? Lazima uchague machache na muhimu zaidi na …

Zimebaki Siku Sita Tu Ili Tuanze Semina Ya Kuanza Mwaka 2022 Kiushindi, Karibu Ushiriki Semina

Maisha yetu ni kama mpira wa miguu, unapokuwa uwanjani huwezi kujijua kama unafanya makosa lakini unapokuwa na mwalimu anayekuangalia nje au wapenzi watazamaji wanakua wanajua kwa uhakika ni wapi unakosea ukiwa uwanjani. Hata kama uko vizuri sana kwenye kile unachofanya bado unahitaji mwalimu wako wa kukusimamia hatua kwa hatua. Usiwaone wachezaji wenyewe viwango vya juu …

Haya Ndiyo Maisha Ambayo Hayahitaji Kazi Kuhubiri

Maisha halisi unayoishi hayahitaji kazi kuhubiri. Matendo yako yanajidhihirisha yenyewe. Huhitaji kuwaambia watu kuwa wewe ni mtu mwema, bali maisha yako yatashuhudia kile kilichopo ndani yako. Huhitaji kuwaambia watu wewe ni mtu ambaye uko vizuri sana kwenye kitu fulani, bali watu watakujua tu kupitia kile unachofanya. Huwezi kuhubiri vizuri kile ambacho wewe mwenyewe hukiishi. Unakuwa …

Epuka Kujikaanga Na Mafuta Yako Mwenyewe

Unajikaanga na mafuta yako mwenyewe pale unapokuwa unamchukia mtu bila sababu yoyote ile. Muda mwingine hata yule unayemchukia hajui hilo yeye anaendelea na maisha yake huku wewe ukiendelea kuteseka. Chuki ni sawa na kunywa sumu ili kumkomoa mtu mwingine kitu ambacho unaishia kujiumiza wewe mwenyewe. Hisia ya chuki ni mbaya sana kwa sababu haina faida …

Heri Ya Sikuu Ya Krismasi

Rafiki yangu, ukawe na sikukuu njema, itumie siku hii ya leo kujitafakari. Pia, sikuachi hivi hivi rafiki yangu, nimekuandalia zawadi ya Krismasi ambayo zawadi hiyo ni vitabu viwili vilivyochapwa. Moja ni kitabu cha Ijue Njaa Ya Wanandoa bei yake ni elfu 15. Mbili ni kitabu cha Kwanini Msamaha Why Forgiveness bei yake ni elfu 10. …

Acha Kurusha Mawe Gizani

Kwa sababu hujui nani litampata. Mtenda wa jambo huwa hakumbuki sana kuliko yule anayetendewa. Kumbe basi, unapofanya jambo lolote lile, kumbuka yule anayepokea ndiyo anaona uzito wake. Ndiyo maana unatakiwa kufanya mambo ambayo ni chanya sana kwa sababu unapofanya mambo hasi ni kama unarusha mawe gizani unaweza ukampiga hata mtu ambaye hana hatia yoyote ile. …

Endelea Kufanya Mambo Haya Yanayodumu Milele

Endelea kufanya mambo mazuri yanayodumu milele. Katika zama tunazoishi unaweza ukafanya mambo mazuri na ukaona hakuna anayejali. Lakini huo siyo ukweli, mambo mazuri unayofanya hata kama ni kidogo kiasi gani huwa yanagusa maisha ya wengine na huwa wengine hawayasahau. Kwa mfano, mwandishi Robin Sharma katika kitabu chake cha Manifesto, the hero every day anatushirikisha hadithi …

Design a site like this with WordPress.com
Get started