Design a site like this with WordPress.com
Get started

Epuka Kujikaanga Na Mafuta Yako Mwenyewe

Unajikaanga na mafuta yako mwenyewe pale unapokuwa unamchukia mtu bila sababu yoyote ile.

Muda mwingine hata yule unayemchukia hajui hilo yeye anaendelea na maisha yake huku wewe ukiendelea kuteseka.

Chuki ni sawa na kunywa sumu ili kumkomoa mtu mwingine kitu ambacho unaishia kujiumiza wewe mwenyewe.

Hisia ya chuki ni mbaya sana kwa sababu haina faida yoyote ile.

Haijalishi unakuwa na chuki kiasi gani, hakuna namna inaweza kumdhuru yule unayemchukia. Bali inaishia kukuumiza wewe kwa kukosa furaha na kuwa na mtazamo mbovu.

Shabaha yangu kubwa ya leo ni kukusihi wewe rafiki yangu, ondokana na kila aina ya chuki kwa kujua haina msaada wowote ule zaidi ya kujiumiza wewe mwenyewe.

Acha kuendelea kujikaanga na mafuta yako mwenyewe kwa kuwachukia watu wengine. Wapende watu na acha kuhangaika na madhaifu yao maana utajikuta unajiumiza kwa mambo yasiyokuwa na maana.

Hatua ya kuchukua leo; usiweke nguvu kubwa katika chuki kwa sababu chuki ni hisia ambayo haina msaada wowote kwako.

Tumia nguvu ulizonazo kufanya yale mambo yenye manufaa zaidi kuliko kuwachukia watu wengine.

Ukiona unamchukia mtu bila sababu ujue wewe ndiyo mwenye shida. Ondoa sumu ya chuki kwenye maisha yako na karibisha upendo utawale kwenye maisha yako.
Jipende, wapende wengine na penda kile unachofanya.

Kuwachukia watu ni kujichukia wewe mwenyewe kwani anayewachukia watu maana yake hata yeye mwenyewe hajipendi. Anayejipenda atawapenda na wengine.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: