Design a site like this with WordPress.com
Get started

Zimebaki Siku Sita Tu Ili Tuanze Semina Ya Kuanza Mwaka 2022 Kiushindi, Karibu Ushiriki Semina

Maisha yetu ni kama mpira wa miguu, unapokuwa uwanjani huwezi kujijua kama unafanya makosa lakini unapokuwa na mwalimu anayekuangalia nje au wapenzi watazamaji wanakua wanajua kwa uhakika ni wapi unakosea ukiwa uwanjani.

Hata kama uko vizuri sana kwenye kile unachofanya bado unahitaji mwalimu wako wa kukusimamia hatua kwa hatua.

Usiwaone wachezaji wenyewe viwango vya juu kabisa wanakuwa na walimu wao, wanakuwa na makocha unafikiri wao ni wajinga? Siyo wajinga wanafanya hivyo kwa sababu wanajua binadamu ili aweze kufanya jambo vizuri lazima awe na mtu anayemsukuma kufanya na kumpa usimamizi wa karibu na kumrekebisha.

Sishangai kuona watu ni rahisi kutimiza majukumu wanayopangiwa kazini na bosi kuliko majukumu binafsi. Majukumu ya bosi yataenda vizuri sana kwa sababu bosi atakusumbua kuhakikisha anapata matokeo anayotaka kuyaona, hivyo ili kuepuka usumbufu huo na wewe lazima ujitume ili usionekane mzembe.

Ila ukiwa peke yako, unapanga na unahairisha wewe mwenyewe ila ukiwa na mtu anayekusimamia na anayetaka kuona matokeo huwezi kujiamulia tu.

Kujisimamia ni kazi ngumu ambayo watu wengi hawawezi kuifanya.

Kwa kulijua hilo, nimekuandalia semina ambayo itakupa mwongozo wa namna ya kuanza mwaka wako 2022 kiushindi.

Nataka hamasa unayopata tarehe moja nikusaidie kuiendeleza, kazi yangu kwako itakuwa ni kuendelea kuchochea moto uliowasha januari mosi.

Karibu sana kwenye semina, siku ya kwanza utajifunza masomo yanayokupa hamasa, nimekuandalia viapo ambavyo ukiviapa hakika lazima utakua vizuri.

Wakati narudia kupitia masomo ya semina nilikuwa nasoma somo la nguvu ya kiapo( power of declaration) mpaka mwili ulikuwa unasisimka ni kwa jinsi gani masomo yalivyokuwa na nguvu.

Nina uhakika na wewe yatakwenda kukusaidia kutapata nguvu na hamasa ya kuendelea kujiwasha moto ndani ya mwaka 2022.

Unachotakiwa kufanya sasa ni wewe kulipia ada shilingi elfu 10. Lipia ada yako sasa kwenda namba 0717101505 au 0767101504 wasiliana na mimi ili usikose semina hii kwani ni muhimu mno.

Semina itaanza januari 3, mwaka 2022 na itamalizika januari 12.

Itakua ni semina ya siku kumi (10) na semina itafanyika ndani ya kundi la wasapu la Mimi Ni Mshindi Klabu.

Unachotakiwa kuwa nacho ni mtandao wa wasapu tu, huhitaji kusafiri bali utakuwa hapo ulipo ni wewe kutenga muda wako wa kusoma tu na kuchukua hatua.

Karibu sana rafiki yangu, mwambie na rafiki yako kwamba kuna semina ya kuanza mwaka 2022 kiushindi. Asipange kukosa kwani atanufaika na semina mpaka atashangaa mwenyewe.

Usisahau kuwasiliana na mimi kwa wasapu namba 0717101505 ili niweze kukuunganisha kwenye kundi kujihakikishia nafasi ya kushiriki semina.

Afisa Mhamasishaji Mkuu, Chief Inspiration Officer (CIO) Mwl Deogratius Kessy.

https://kessydeo.home.blog
Karibu na asante sana.

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: