Design a site like this with WordPress.com
Get started

Endelea Kufanya Mambo Haya Yanayodumu Milele

Endelea kufanya mambo mazuri yanayodumu milele.

Katika zama tunazoishi unaweza ukafanya mambo mazuri na ukaona hakuna anayejali.

Lakini huo siyo ukweli, mambo mazuri unayofanya hata kama ni kidogo kiasi gani huwa yanagusa maisha ya wengine na huwa wengine hawayasahau.

Kwa mfano, mwandishi Robin Sharma katika kitabu chake cha Manifesto, the hero every day anatushirikisha hadithi ambayo alikuwa anafanyiwa na mama yake ambayo mpaka leo anakumbuka kwa kile kidogo ambacho mama yake alikuwa anamfanyia.

Mama yake na Robin alikuwa na utaratibu ambao mama yake alikuwa anamletea Robin chakula shuleni kipindi ambacho Robin alikuwa mtoto.

Ndani ya chakula kile alichokuwa anampelekea alikuwa anaweka ujumbe wa jinsi alivyokuwa anampenda mwanae Robin.

Kitendo kile kidogo ambacho mama yake alikuwa anamfanyia mpaka leo Robin anakikumbuka.

Hapa tunapata funzo kuwa endelea kutenda mema, mazuri unayofanya yanaendelea kujenga kumbukumbu nzuri inayodumu milele.

Hata wewe kuna kitu ambacho umezoea kumfanyia mwenzako huenda asikuambie lakini unajenga kumbukumbu nzuri inayodumu milele. Kwa mfano, kama una watoto au mtoto kila siku unapoamka na kuwaambia namna unavyowapenda hapo unakuwa unajenga kumbukumbu nzuri inayodumu milele licha ya wewe kuona ni kitu kidogo.

Endelea kuwafanyia watu wengine vitu vidogo vinavyowafanya wafurahie maisha yako.

Siku moja robina alikuwa na wazazi wake, mara wakakutana na mchezaji maarufu Mohamed Ali, Robin alikuwa na shauku ya kukutana naye na akawaomba wazazi wake wasimamishe gar ili aweze kumsalimia na kuomba wapige picha ya pamoja.

Mchezaji yule maarufu alipoombwa kupiga picha, alikuwa tayari kusimama na kupiga nao picha.

Robin alipomuuliza kwa nini ana utayari wa aina hiyo, alimjibu unahitaji kufanya vitu vidogo sana kuwafurahisha watu wengine.

Hapa tunajifunza kuwa umuhimu wa vitu tunavyowafanyia wengine huwa havisauliki. Kwa mfano, kitendo tu cha kumsalimia mtu huenda ukaona ni kidogo lakini kwa mwingine ni kitu muhimu sana.

Kuwa tayari kufanya vitu vidogo vidogo vizuri kwa wengine, kwako inaweza kuwa kawaida, lakini kwa wengine ikawa ni kitu kikubwa ambacho hawatakisahau maisha yao yote.

Hatua ya kuchukua leo; endelea kufanya yale mazuri ambayo yanawagusa watu hata kama kwako unaona ni kidogo kiasi gani.

Endelea kutenda mema, endelea kufanya kile unachofanya hata kama hakuna anayeona, hakuna anayejali lakini jua wako ambao wanajali na wananufaika na wewe.

Thamini kile ambacho watu wengine wanakufanyia, wape watu wengine kile ambacho wao wanapenda kupewa.
Watendee wengine kile ambacho wewe unapenda kutendewa.
Heshimu na thamini mchango wa kila mtu ambao wamekuwezesha kufika hapo ulipo kwa hali na mali.

Kila mtu ana msaada wake, nufaika na kila msaada wa mtu unayehusiana naye.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: