Omba Msaada Kwenye Hili

Tuko hapa duniani kwa ajili ya kusaidiana. Unafanya hicho unachofanya kila siku kwa ajili ya kusaidia wengine. Wajibu wetu mkubwa ni kusaidia, kupitia kusaidia wengine na sisi ndiyo tunapata. Kujitegemea siyo kujitosheleza. Tunategemeana kama vile viungo vya mwili. Hivyo, kwenye maisha usiogope kuomba msaada pale ambapo unahitaji msaada. Kuomba msaada siyo kushindwa au hujui. Huwezi …

Jinsi Ya Kuilinda Siku Yako

Pale unapoamka salama kwenye siku yako inakuwa ni siku nyingine bora na ya kipekee kwako kwenda kufanya makubwa. Kustahilishwa kuiona siku yako ni bahati hivyo hutakiwi kuiharibu siku hiyo kwa namna yoyote ile , unapaswa kuilinda kwa ajili ya uzalishaji tu na si vinginevyo. Ili uweze kuilinda siku yako unapaswa kuwa na orodha ya mambo …

Kinachokupoteza Ni Hiki

Kinachokupoteza ni kujilinganisha na watu wa nje. Unataka kuishi kama mtu ambaye tayari ameyapatia maisha, unataka kuishi kama mtu ambaye yuko katika nchi zilizoendelea na wakati wewe uko katika nchi zinazoendelea.Kwa mfano, kwenye kazi unataka kufanya kidogo huku ukiwa na matarajio ya mfano makubwa. Unajilinganisha na mabilionea ambao wakati wanaanza walikuwa hawaishi maisha ya anasa, …

Ni Tatizo Lako

Kama hujisikii vizuri hilo ni tatizo lako binafsi.Wala usimtafute mtu wa kumlaumu, hakuna anayeharibu siku yako ila wewe mwenyewe. Wewe ndiye unayechagua ufikirie nini, uangalie nini, uambatane na nani na ufanye nini. Hakuna anayeharibu maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe. Kwa mfano, kama unachagua kufikiria vitu vinavyokufanya ujisikie vibaya unamlaumu nani? Kama umechagua kusikiliza na kuangalia …

Kitendawili, Hakisimami,Kikisimama Msiba

Tegua kitendawili hiki,Hakisimami, na kikisimama msiba, jibu lake nini? Huku ukiendelea kufikiria jibu, ngoja na mimi nikupe jibu,Jibu lake ni moyo. Kwa nini moyo? Kwa sababu moyo ndiyo kiungo pekee katika mwili wa binadamu huwa hakijawahi kusimama kufanya kazi yake. Kama moyo ukisimama maana yake wewe hauna maisha.Moyo ukisimama unaleta msiba . Sina uhakika kama …

Usimsahau Kumjali Mtu Huyu Hapa

Kazi ndiyo rafiki wa kweli hilo halina ubishi. Na fedha ndiyo jawabu la mambo yote, na hili halihitaji mjadala. Tunaalikwa kuwasaidia wengine, ni kweli kabisa lakini huwezi kusaidia kama wewe mwenyewe huna cha kutoa. Njia rahisi ya kusaidia masikini ni wewe kuwa tajiri. Kama unataka kusaidia watu, kipengele cha kwanza ni wewe kuwa bora. Kama …

Ni Kujiandaa Kuumia

Kuchagua kazi yoyote ile kwa kigezo cha kipato ni kujiandaa kuumia, kwa sababu kazi nyingi hazitakupa kipato kinachoendana na juhudi unazopaswa kuweka kwenye kazi hiyo. Sina uhakika kama itakufaa lakini kitu cha kwanza unachopaswa kutumia kufanya maamuzi ya kazi ni mapenzi na kujali. Ikiwa unafanya kile unachopenda na unakijali kwa sababu kina maana kwako hata …

Usitafute Usalama Kwenye Maisha

Timu yoyote inayocheza uwanjani kwa lengo tu la kujilinda mara nyingi huwa inashindwa kabla hata mchezo haujaisha. Kiasili sisi binadamu tuko kwenye mwendo, hutakiwi kusimama, hutakiwi kuridhika unatakiwa kukua kila siku. Kwenye maisha hakuna kusimama, ni aidha uende mbele au urudi nyuma. Hivyo basi, maboresho yanatakiwa kuwa kila siku. Isifikie mahali unasema kwa sasa nimeshafika …

Usinunue Matatizo Ya Watu

Ukikaa na watu na kuwasikiliza kwa nini maisha yao yamekuwa hivyo yalivyo unaweza ukaamini ni kweli na kuwaonea huruma. Watu wengi bado hawajajitambua wanajua jukumu la maisha yao siyo lao bali ni la watu wengine na hapo ndipo matatizo yanapoanzia.Unaposema maisha magumu, magumu ukimaanisha nini? Kama hufanyi kazi, huishi misingi ya fedha unafikiri maisha hayatakuwa …

Msingi Mkuu Wa Fedha

Changamoto zote za kifedha zinaanzia kwenye mapato, matumizi na bajeti. Utaweza kuhangaika sana kwenye fedha, ukamtafuta mtu akuombee au unaweza kujiona huna bahati kwa sababu ya yale unayopitia kwenye fedha. Lakini msingi wa kwanza wa fedha ni kuishi chini ya kipato. Ukiona una shida kwenye fedha, anzia kwenye matumizi. Kwenye eneo la matumizi ndiyo linamaliza …

Design a site like this with WordPress.com
Get started