Iko wazi na siyo siri. Ukitaka ugomvi na watu ni pale wanapojua wewe unapata hela zaidi kuliko wao. Hakuna mtu anayependa kukuona wewe ukipata hela. Wako wachache sana watafurahia kukuona wewe ukipata hela nyingi lakini wengine utawakera na watakuchukia.
Hakuna mtu anayependa kukuona wewe ukipata hela kwa mfano, ukiwa umeajiriwa na ukawa na miradi yako ya pembeni inayokuingizia hela watu wataanza kukuchukia bila sababu, wengine watasema kwa sasa wewe hufanyi kazi inayokupasa ufanye bali unajali sana biashara zako tu.
Ukitaka chuki na watu wajue unapiga hela sana iwe kwenye mshahara au kipato chochote kile halali. Kwa kuwa umeshajua ukweli huu kuwa watu hawapendi kukuona ukipata hela unatakiwa kuwa makini sana.
Usiwaambie watu juu ya mambo yako ya kifedha. Labda mtu ambaye ni mtu muhimu kwako yule unayemwamini ambaye anakufuatilia kila mwezi kwa taarifa za maendeleo yako kama vile mwalimu au kocha wako.
Hata kama unapata sana hela iwe ni siri yako usitafute kununua matatizo ya lazima. Watu wakishajua unapata sana hela watakuanzishia visa vya kila aina. Hata wale ambao wamekupangishia eneo la biashara watakupandishia kodi au watataka kukufukuza eneo hilo ili wafanye kile ambacho wewe unafanya na hata wakijaribu hawataweza kwa sababu wewe ni wewe na hawajui umebeba nini ndani yako na wala hawajui unatumia maarifa gani kukufanya kuwa bora. Kwenye chochote kile wanachofanya watu wako watu ambao wamefanikiwa kwenye eneo hilo na wako ambao hawajafanikiwa kwenye eneo hilo.
Hakuna mtu ambaye anayependa kukuona wewe ukipata hela lazima watakuwekea vikwazo. Kwa mfano, ni watu wachache sana wanapenda kukuona wewe ukipata hela lakini siyo wote.
Kwa mfano, ukipata hela nyingi kwa wakati mmoja serikali itakuchunguza lakini ukiwa huna hela haikuchunguzi sasa hapo ndiyo utaweza kukubaliana na mimi kwamba HAKUNA mtu anayependa kukuona wewe ukipata hela nyingi.
Kwa kuwa watu hawapendi kukuona ukipata hela na wewe ndiyo ubweteke usipambane hapana, endelea kuweka kazi zaidi ili uzipate zaidi.
Hata kwenye vitabu vya maandiko matakatifu vinasema kuwa fedha ni ulinzi. Ukiwa nayo itakuwezesha kufanya kile unachotaka.
Usiwaogope watu wanaoua mwili bali mwogope Mungu anayeua roho na mwili. Kila siku pambania maisha yako kuwa bora sana kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kukupuuza kwa sababu uko vizuri.
Falsafa ni moja tu, wasaidie wengine kupata kile wanachotaka na wewe utapata kile unachotaka kwenye maisha yako.
Yaani pale unapofikiria nitapate, jiulize kwanza umetoaje? Kadiri unavyotoa ndivyo unavyopokea zaidi.
Acha mazoea kabisa na fanya vitu vyako kwa viwango. Kwa yoyote yule anayekutana na kazi yako ajivunie tena kufanya kazi na wewe. Kile unachotoa kiwe msaada kwa wale unaowalenga, usifanye tu ili mradi umefanya bali fanya kwa sababu unataka kiende kumpa mtu suluhisho kwenye kile kinachomsumbua.
Hatua ya kuchukua leo; watu wasijue zaidi juu ya njia zako za kuingiza hela.
Naomba maeneo haya yawe ni siri kwako eneo la familia, afya na fedha. Watu wakishajua miongoni mwa maeneo hayo hapo juu wataweza kukusumbua, kadiri unavyofanikiwa ndivyo unavyopaswa kuwa makini maana siyo watu wote wanapenda kukuona ukipata hela nyingi.
Mwezi huu ukawe mwezi wa kukusanya fedha nyingi, katoe thamani kubwa ili uweze kupata matokeo makubwa.
Ukawe bora kwenye kile unachofanya kiasi kwamba hakuna anayeweza kukupuuza.
Kumbuka kupitia mchakato wako kila siku, kwa sababu mchakato ndiyo zawadi na mchakato ndiyo kazi yenyewe. Bila mchakato hakuna matokeo.
Pambana na mchakato kwa sababu iko ndani ya uwezo wako na matokeo yako nje ya uwezo wetu.
Muhimu;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504