Haijalishi unafanya kazi ofisini, kiwandani, dukani au wito wowote ule uliochagua kuishi unahitaji kuwa na uvumilivu.
Popote pale ulipo unapaswa kuwa na uvumilivu.
Bila uvumilivu sijui kama kuna mtu angeweza kufanikiwa na kile ambacho anacho sasa. Karibu mafanikio yote uliyonayo umefanikiwa kwa sababu ulikuwa na uvumilivu.
Kuanza na kumaliza kitu inahitaji ung’ang’anizi na uvumilivu ndiyo maana siyo wote wanakuwa na uvumilivu wa kumaliza. Mafanikio yako mwisho sasa mara nyingi watu huwa wanaishia njiani bila ya kuyafikia malengo yao.
Usiwe mtu kuwa kutaka mafanikio ya haraka. Hata kama unaweka kazi kweli huwezi kuyaona mabadiliko kwa siku moja. Fanya kazi yako na jipe muda kuiachia na asili nayo ifanye kazi yake.
Uvumilivu ni uwekezaji mzuri kuelekea kwenye mafanikio. Unatakiwa kuwa mvumilivu na bosi, mteja, usawa, vitendea kazi, masomo yako nakadhalika.
Mfanyakazi mzuri hata kama ana kitendea kazi kibaya atajaribu na kujitahidi kufanya kazi nzuri. Naomba ukawe mfanyakazi mzuri hata kama kile ulichonacho siyo kizuri jitahidi ukazalishe kazi nzuri.
Mfanyakazi mbaya hata akiwa na vitendea kazi vizuri, hatozalisha kazi nzuri bado ataendelea kulaumu vitendea kazi kwa kufanya kazi mbaya.
Kila mmoja wetu anahitaji uvumilivu kwenye kile anachofanya. Ukikosa leo usikate tamaa jua pia kuna kesho.
Kama unataka kuweka mwili wako kwenye hali nzuri basi jitahidi sana kuishi uvumilivu kwa sababu HAKUNA kitu ambacho utaweza kukipata kwenye maisha yako bila kuwa na uvumilivu.
Unahitaji uvumilivu na wale watu wako wa karibu, ndugu, jamaa, rafiki, mwenza wako nk. Ukikosa uvumilivu utashindwa kuhusiana na watu. Unapaswa kuwaelewa watu kuwa inahitaji uvumilivu kuishi na watu na usipokuwa mvumilivu utakuwa ni mtu wa msongo wa mawazo kila siku.
Hatua ya kuchukua leo; jifunze kuwa mvumilivu. Wavumilie wengine kwa sababu hata wewe wanakuvumilia.
Kila kitu huwa kinabadilika, jaribu kutoa muda kwenye uwekezaji wowote ule uliofanya au unaofanya.
Usikubali kuishia njiani, vumilia mapito unayopitia kwani hakuna tatizo linalodumu milele. Ili uweze kuona mafanikio kwenye eneo lolote la maisha yako unapaswa kuwa mvumilivu.
Muhimu;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504