Tegemea Kilicho Bora

Rafiki, Maisha tuliyonayo ni matokeo ya mategemeo ambayo tumekuwa nayo siku za nyuma.Hatupati tofauti na tunachotegemea. Pale unapoamini jambo linawezekana na kulifanyia kazi ipasavyo, dunia yote itakusaidia kufanya ndoto zako, malengo yako na mipango yako kuwa kwenye uhalisia. Kupata ushindi kwenye maisha yako unapaswa kuiandaa akili yako kupata ushindi. Kama unataka kupata matokeo mazuri, andaa …

Jinsi Ya Kuongeza ushawishi Kwa Wengine

Rafiki,Tunaweza kupata tunachotaka kwenye maisha yetu kama tutaweza kuwashawishi wengine kutupa kile tunachotaka kutoka kwao.Lugha ya ushawishi ni nzuri kwa sababu, kwenye maisha hatupati tunachostahili bali tunachoshawishi. Binadamu ni watu wa sifa kiasili, kama unataka kumshawishi mtu halafu ukaanza na kumkosoa lazima atashindwa kukubaliana na wewe. Katika maisha unaweza kukutana na watu ambao wanafanya vitu …

Tabia Kuu Mbili Za Watu

Rafiki , Watu wana tabia kuu mbili, kwanza watu ni viumbe wa kijamii kwa sababu wanawapenda na kuwajali watu ambao wapo ndani ya kundi moja. Hapa ndiyo maana tunao watu wengi wanafanya vitu kama wengi wanavyofanya. Licha ya kuwa sisi ni viumbe vya kijamii unapaswa kuwa makini kwani siyo kila kinachofanywa na wengi ndiyo sahihi …

Kuwa Makini Kwenye Hili Hapa

Rafiki, Jitahidi sana kwenye maisha yako unapokuwa unaongea basi ueleweke kile unachoongea. Hakuna kitu kibaya kama unaongea halafu ujumbe haufiki. Ongea kitu unachotaka kusema, kiseme kwa lugha rahisi kiasi kwamba kila mtu anaelewa. Kila unapotaka kusema kitu na watu wajue, tafuta lugha rahisi ambayo mtu ataelewa bila shaka. Na kila mtu anapokuwa anaongea na wewe …

Wateke Watu Kwa Kuwapa Kitu Hiki

Ili binadamu atulie sehemu yoyote ile anahitaji kupata uhakika. Watu wengi ambao wanahangaika kuhusu kitu fulani, ni kwa sababu katika hali waliyonayo sasa bado hawajapata kile wanachotaka. Kama unafanya biashara, ili mteja wako atulie na umteke, unapaswa kumpatia kile anachotaka. Ukiweza kujua maumivu ya mteja wako na kisha kumtatulia maumivu yake hawezi kwenda sehemu yoyote …

Utakuja Kuimbuka Nguvu Ya Buku Baadaye

Rafiki, Katika hali ya kawaida kwa sasa kama unafanya kazi huwezi kukosa elfu moja. Na unakuwa nazo sana, unatumia kila siku zaidi hata ya elfu moja.Unawalipa watu wengine kila siku, lakini kwa miaka ya baadaye hao unaowalipa hawatakuja kukusaidia kukupa vitu bure kama huna fedha.Kitu kikubwa unachotakiwa kufanya kwenye maisha yako ni kuwekeza. Fanya uwekezaji, …

Kuwa na Ufuatiliaji Endelevu

Rafiki, Vitu vingine unavyokosa kwenye maisha yako ni kwa sababu moja tu, nayo ni kushindwa kufuatilia. Vitu vingi sana vimefichwa kwenye ufuatiliaji. Usipofuatilia kile unachotaka hupati, lakini ukifuatilia unapata.Usiwalaumu watu wengine kwa sababu ya kuwa hawakupi kile unachotaka kutoka kwao kabla hujawafuatilia. Chochote kile unachotaka kutoka kwa wengine fuatilia kwa ukaribu. Rafiki, fedha imejificha kwenye …

Kazini Kwa Huyu Kuna Kazi

Rafiki yangu nikupendaye, Asili ya binadamu ni kazi.Tumeumbwa kuzalisha ili maisha yetu yaende mbele. Na asili ya kazi ni kuchosha. Na huwa kuna tabia ya watu hupenda kusema kazi za wengine ni rahisi pale wanapolinganisha.Lakini, ukweli ni kwamba, kazini kwa kila mtu kuna kazi. Ndiyo, kazini kwako kuna kazi kama ilivyo kwa mwingine.Na hakuna kazi …

Usiwaruhusu Watoto Wako Wafanye Kitu Hiki

Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Wazazi huwa wanakuwa na upendo mkubwa na watoto wao pale wanapokuwa wanawapata kitu ambacho ni kizuri. Sina uhakika kama itakufaa lakini watoto wa zama hizi wanakua bila ya malezi bora, wazazi wanaogopa kuwaadhibu watoto kwa kuhofia kuchukiwa na watoto hao. Lakini kitu chema ambacho mzazi anaweza kufanya kwa mtoto …

Lazima Utoke Nje Ya Mazoea

Rafiki, Ili ufanikiwe kwenye maisha yako, lazima ufanye kitu kimoja nacho ni utoke nje ya mazoea. Mazoea huwa yanaleta matokeo yale yale mara zote.Lazima utoke nje ya mazoea ili upate matokeo mazuri.Lazima uende hatua ya ziada ili upate matokeo ambayo hujawahi kuyapata. Huchoki kupata matokeo yale yale kila siku? Kama unachoka basi fanya mabadiliko.Matokeo yale …

Design a site like this with WordPress.com
Get started