Design a site like this with WordPress.com
Get started

Muda Mzuri wa Kufanya Kazi Za Kutumia Akili

Zipo kazi nyingi zinazohitaji nguvu na akili. Ziko kazi ambazo zinahitaji umakini wako wa hali ya juu sana na hizi ni kazi ambazo hazihitaji usumbufu wa aina yoyote ile.

Kwa mfano, kazi kama za kuandika ni kazi ambazo zinahitaji umakini wa hali ya juu. Unahitaji muda ambao hauna usumbufu.

Muda mzuri wa kufanya kazi zinazotumia akili yaani mental work ni asubuhi. Fanya kazi zako zinazohitaji umakini wako mapema sana kabla dunia haijaamka.

Muda mzuri ambao dunia bado imelala ni kuanzia saa 10 mpaka saa 12 asubuhi.

Muda wa kuanzia saa 10 mpaka saa 12 ni muda mzuri wa kufanya tahajudi, yaani meditation. Muda mzuri wa kusoma kitabu.

Ni muda mzuri wa kupangilia siku yako unavyotaka iwe. Unaandika mambo unayotaka kufanya na yale ambayo hupaswi kufanya ndani ya siku husika.

Kuna faida kubwa ukiishi yale unayojifunza. Watu wanakosa muda wa kujitumikia kwa sababu ya kutoamka mapema. Ukichelewa kuamka utakimbizana na muda na kwenda kuwatumikia wengine.

Muda wa alfajiri ni muda ambao akili inakuwa iko freshi kabisa. Na unakuwa na nguvu ya kutosha.

Hatua ya kuchukua leo; Jitahidi kutumia muda wa asubuhi kabla dunia haijaamka kufanya mambo yako muhimu yanayohitaji umakini wako wa hali ya juu.

Muda wa kuanzia saa 10 mpaka saa 12 asubuhi ni muda wako wa dhahabu ambao hutakiwi kusumbuliwa na mtu. Ni muda wako ambao unaweza kufanya kile unachotaka kufanya.

Dunia ikishaamka huo muda sio wako tena ni wa watu wengine. Utaenda kuwatumikia wengine ili kujihakikishia ushindi kila siku asubuhi amka mapema.

Ukishainza siku yako utakutana na mambo mengi ambayo mengine yatakukatisha tamaa au kukuharibia siku au hamasa ya kufanya kazi. Lakini ukiwa na uhakika wa kuwa umeshapata ushindi wako asubuhi hata mambo yakienda ndivyo sivyo unajua una kitu cha kujivunia.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: