Design a site like this with WordPress.com
Get started

Zifahamu Aina Mbili (02) Za Wateja Katika Biashara Yako au Huduma Unayotoa

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni imani yangu kuwa uko salama kabisa huku ukiendelea kutimiza kusudi la maisha yako hapa duniani. Hongera rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo hivyo basi, nakusihi sana itendee haki siku hii ya leo usikubali siku ipite bila kufanya kitu cha maana kwani muda ukiondoka haurudi tena.

whatsapp-image-2016-09-30-at-16-29-22BONYEZA HAPA KUPATA KITABU HIKI

Mpendwa msomaji napenda kutumia nafasi kukualika tena katika makala yetu ya leo ambapo leo tutajifunza aina mbili za wateja katika biashara yako. Hivyo, mpendwa msomaji karibu sana pia, nakusihi sana uweze kusafiri pamoja na mimi mpaka mwisho wa somo letu la leo.

Ili biashara yako ikue na iitwe biashara inahitaji kitu kimoja ambacho ni muhimu sana nacho ni wateja. Biashara au huduma unayotoa kama hakuna wateja basi hufanyi biashara hivyo biashara ili iweze kuwa biashara lazima iwe na kiungo muhimu nacho ni wateja.

Kitu kinachotengeneza eneo la masoko katika baishara ni wateja. Je ni aina gani ya wateja ndio malengo mahususi ya somo letu la leo karibu tuendelee kujifunza wote kwa pamoja. Kuna aina mbili za wateja wanaotengeneza eneo la masoko katika biashara nao ni;

Wa kwanza ni wateja muhimu. Wateja muhimu ni wale wanaonunua kile unachouza.  Kama katika huduma yako una wateja muhimu basi hao ndio wateja wa mfano kwako. Hawa ndio wateja wanaokuamini kutokana na huduma unayotoa na kununua huduma hiyo. Huyu mteja muhimu ndio unapaswa kumpatia huduma bora ili aendelee kujenga uaminifu na wewe kila siku kupitia huduma unayotoa.

SOMA; Jambo Muhimu La Kuzingatia Pale Unapotoa Huduma Kwa Mteja

Wa pili ni wateja.wateja wanaweza wakawa wengi lakini siyo wote watanunua kile unachouza. Wateja unaweza kuwanao na unawaona ni wengi lakini siyo wote watanunua kile unachouza. Kwahiyo, mteja muhimu ndio ufunguo wa mauzo kwenye biashara yako. Unatakiwa kuweka nguvu zako kwa wateja muhimu ambao wanathamini na kuamini ile huduma unayompatia.

Hatua ya kuchukua leo. Je biashara yako ina wateja au wateja muhimu. Watumie wateja muhimu na ongeza thamani kwa wateja wako ili waendelee kuwa pamoja na wewe. Wapatie huduma bora na wewe mwenyewe jitahidi kuwa bora. Huduma yako haiwezi kuwa bora kama mtoa huduma hauko bora.

Kwahiyo, kama kampuni inazalisha bidhaa  inatakiwa kuzingatia pia katika eneo la masoko. Masoko ndio kitu kinachoendesha biashara unayofanya. Ni muhimu sana kuwa na wateja muhimu kuliko kuwa na wateja wasio kuwa na tija kwenye biashara yako.

SOMA; Mambo 20 Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Start With Why

Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Pia, Hakikisha unapenda ukurasa wetu wa facebook kwa maarifa zaidi.

 

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: