Kama kuna ujuzi ambao unataka kujifunza kwenye maisha yako, basi jifunze sayansi na sanaa ya kuuza. Kwa nini? Kwa sababu kuuza ndiyo msingi wa kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako. Kwenye maisha yako kila kitu ni mauzo. Unauza kwenye ajira, unaunza kwenye mahusiano, unauza kwenye biashara.Kama unataka kuwa kiongozi bora jua jinsi ya kuuza …
Kitu Cha Kujifunza Kutoka Kwa Muuza Samaki Aina Ya Nguru
Yamaguchi ni muuzaji wa samaki mwenye mafanikio makubwa sana. Analala masaa matatu tu kwa siku na anahudumia migahawa zaidi ya elfu moja Yukitaka Yamaguchi ni raia wa Japan ambaye ameanza kuuza samaki tokea mwaka 1980. Anaitwa mfalme wa samaki na mtu akiitwa mfalme maana yake amebobea kweli kwenye kitu hicho. Kitu kikubwa nilichojifunza kutoka kwa …
Continue reading "Kitu Cha Kujifunza Kutoka Kwa Muuza Samaki Aina Ya Nguru"
Mtu Akikupa Ahadi Fanya Hivi
Watu wengi tumekuwa tukipewa ahadi na watu mbalimbali, tunapewa ahadi na watu lakini ahadi hizo huwa hazitekelezwi. Kwa nini kwa sababu hakuna ufuatiliaji.Ili ahadi zikamilike lazima zifuatiliwe. Watu huwa wanafanya pale wanapofuatiliwa. Kama unataka mtu akupe fedha, unatakiwa kumfuatilia. Mteja akikuambia nitakutafuta, usisubiri mpaka aje kukutafuta bali mfuatilie kwenye ahadi yake. Kama unataka kupata fedha, …
Ukishajua Kile Unachotaka
Hicho pekee ndiyo kinapaswa kuwa kipaumbele kwako.Komaa nacho mpaka ukipate. Sema hapana kwa yote ambayo hayana mchango kwako.Utashawishiwa na vitu vingi ambavyo havihusiani na unachotaka, lazima uwe na nidhamu ya kusema hapana na kuweka umakini wako wote kwenye kile unachotaka.Haijalishi wazazi wako, ndugu zako, wafanyakazi wenzako na hata jamii inasema na kufanya nini, jua hakuna …
Omba Msaada Kwenye Hili
Tuko hapa duniani kwa ajili ya kusaidiana. Unafanya hicho unachofanya kila siku kwa ajili ya kusaidia wengine. Wajibu wetu mkubwa ni kusaidia, kupitia kusaidia wengine na sisi ndiyo tunapata. Kujitegemea siyo kujitosheleza. Tunategemeana kama vile viungo vya mwili. Hivyo, kwenye maisha usiogope kuomba msaada pale ambapo unahitaji msaada. Kuomba msaada siyo kushindwa au hujui. Huwezi …
Jinsi Ya Kuilinda Siku Yako
Pale unapoamka salama kwenye siku yako inakuwa ni siku nyingine bora na ya kipekee kwako kwenda kufanya makubwa. Kustahilishwa kuiona siku yako ni bahati hivyo hutakiwi kuiharibu siku hiyo kwa namna yoyote ile , unapaswa kuilinda kwa ajili ya uzalishaji tu na si vinginevyo. Ili uweze kuilinda siku yako unapaswa kuwa na orodha ya mambo …
Kinachokupoteza Ni Hiki
Kinachokupoteza ni kujilinganisha na watu wa nje. Unataka kuishi kama mtu ambaye tayari ameyapatia maisha, unataka kuishi kama mtu ambaye yuko katika nchi zilizoendelea na wakati wewe uko katika nchi zinazoendelea.Kwa mfano, kwenye kazi unataka kufanya kidogo huku ukiwa na matarajio ya mfano makubwa. Unajilinganisha na mabilionea ambao wakati wanaanza walikuwa hawaishi maisha ya anasa, …
Ni Tatizo Lako
Kama hujisikii vizuri hilo ni tatizo lako binafsi.Wala usimtafute mtu wa kumlaumu, hakuna anayeharibu siku yako ila wewe mwenyewe. Wewe ndiye unayechagua ufikirie nini, uangalie nini, uambatane na nani na ufanye nini. Hakuna anayeharibu maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe. Kwa mfano, kama unachagua kufikiria vitu vinavyokufanya ujisikie vibaya unamlaumu nani? Kama umechagua kusikiliza na kuangalia …
Kitendawili, Hakisimami,Kikisimama Msiba
Tegua kitendawili hiki,Hakisimami, na kikisimama msiba, jibu lake nini? Huku ukiendelea kufikiria jibu, ngoja na mimi nikupe jibu,Jibu lake ni moyo. Kwa nini moyo? Kwa sababu moyo ndiyo kiungo pekee katika mwili wa binadamu huwa hakijawahi kusimama kufanya kazi yake. Kama moyo ukisimama maana yake wewe hauna maisha.Moyo ukisimama unaleta msiba . Sina uhakika kama …
Usimsahau Kumjali Mtu Huyu Hapa
Kazi ndiyo rafiki wa kweli hilo halina ubishi. Na fedha ndiyo jawabu la mambo yote, na hili halihitaji mjadala. Tunaalikwa kuwasaidia wengine, ni kweli kabisa lakini huwezi kusaidia kama wewe mwenyewe huna cha kutoa. Njia rahisi ya kusaidia masikini ni wewe kuwa tajiri. Kama unataka kusaidia watu, kipengele cha kwanza ni wewe kuwa bora. Kama …