Dalili Za Kushindwa Vibaya Kwenye Biashara

Kama umeamua kufanya kazi au biashara fanya biashara kweli. Toa thamani kubwa na mtu anufaike na huduma yako. Chochote kile ulichoamua kukifanya hujaamua kufanya kwa sababu yako binafsi. Unafanya kwa ajili ya wengine. Hakuna kitu ambacho kinawachosha wateja kama huduma mbovu. Dalili ya kwanza biashara kufa ni pale mtu anapotoa huduma mbovu. Kutoa huduma mbovu …

Kinachokufunga Ndiyo Hiki Hapa

Unaweza kumtafuta mchawi kwenye maisha yako pale unapoona mambo yako hayaendi vile unavyotaka. Kila ukigusa unaona matokeo ya tofauti. Lakini kinachokufunga usiweze kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako ni imani. Watu wana imani za ajabu zinazowafunga wasione mbele wala nyuma. Imani ina nguvu kubwa sana kwenye maisha yetu. Tusipobadilisha imani zetu hatuwezi kubadilisha maisha yetu.Imani …

Jinsi Ya Kupata Wasaidizi Wazuri Kwenye Biashara Yako

Rafiki yangu nikupendaye, Maisha ni kujifunza. Na kadiri unavyojifunza kila siku ndivyo unavyopata maarifa ya kufanya maisha yako kuwa bora kabisa. Watu wengi wanapata changamoto ya kupata wasaidizi wa kufanya nao kazi. Yule ambaye hajawahi kuajiri anaweza kusema hakuna kazi. Lakini, habari njema ni kwamba, kazi ziko nyingi changamoto ni watu sahihi na bora wa …

Kila Siku Weka Elfu Tatu

Kinachopelekea watu wengi kukopa hela ndogo ndogo ni kwa sababu ya kukosa akiba. Matatizo ya watu kukopa hela ndogo ndogo huwa yanakuwa ni chini ya milioni moja. Kama mtu ukiamua kuwa na akiba ya milioni moja ya dharura huwezi kukimbilia kukopa hovyo. Na wengine hawawezi kuishi bila kukopa. Wasipokopa wanakuwa kama vile wana "arosto"ndani yao. …

Ukikosa Ulichokipenda, Penda Hiki Hapa

Jana niliona gari moja aina ya Costa ikiwa imebeba abiria ndani wakielekea sehemu fulani.Nyuma waliandika ujumbe mmoja, ujumbe huo ulinitafakarisha sana nikasema leo nitakushirikisha rafiki yangu. Ujumbe huo ulikuwa unasema,Ukikosa ulichokipenda, penda ulichonacho. Mara nyingi watu huwa wanateseka kwa vitu ambavyo hawana. Ukiona watu wengi wanateseka, siyo kwa ajili ya vile ambavyo wanavyo, bali vile …

Acha Kuhangaika Na Mambo Mapya

Tunayafanya maisha yetu kuwa magumu kwa sababu ya kuhangaika na vitu vipya kila siku. Tuliyokuwa nayo, bado hatujaweza kuyafanya vizuri kiasi kwamba tuende tukahangaike na vitu vipya. Hii inakuwa kama akili za mkulima kichaa. Mkulima kichaa ni yule ambaye anapanda mbegu leo kesho anaenda kufukua na kuangalia kama imeota. Kama haijaota anaenda tena kupanda sehemu …

Mambo Ni Yale Yale

Ndiyo, mambo ni yale yale lakini kinacholeta utofauti ni ufanyaji.Wako ambao wanafanya kwa kawaida na wanapata matokeo ya kawaida.Na wako ambao wanafanya kwa utofauti na kupata matokeo mazuri zaidi. Vyombo unavyotumia nyumbani siyo vipya kila siku. Ni vile vile, vinatumika, vinaoshwa na hivyo ndivyo ilivyo kwenye kukaa kwenye mchakato. Mambo ni yale yale. Unaweza kuona …

Mradi Mkuu Wa Biashara Yako

Kama unafanya biashara na wewe ndiyo mmiliki wa biashara hiyo, wewe ndiyo mradi mkuu kwenye biashara yako. Ili biashara yako ikue, unapaswa kujifunza zaidi. Achana na mazoea, na kila siku weka kazi ya kujifunza ili kuwa bora sana.Kama wewe ndiyo mradi mkuu kwenye biashara yako, unapaswa kuwa kioo kwa wengine wanaokuangalia. Unapaswa kuijua biashara yako …

Njaa Inayowasumbua Watu Wengi Zama Hizi

Tunaishi kwenye zama ambazo hazina utulivu wa akili. Kwa sababu, watu wako bize na mitando ya kijamii inawafanya watu kushindwa kuwajibika vizuri kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yao. Kutokana na ubize ambao watu wanakuwa wanao, wanakuwa wanatengeneza njaa kwenye maeneo mengine ya maisha yao. Njaa inayowasumbua watu wengi zama hizi, ni njaa ya kusikilizwa. Tukianza …

Kitu Ambacho Watu Wengi Hawana

Watu wengi wamekosa kitu kinachoitwa ustaarabu. Watu wengi hawana ustaarabu ndiyo maana mtu anaweza kumfanyia mwingine kitu ambacho siyo sahihi. Kama mtu una ustaarabu, huwezi kufanya kitu ambacho siyo sahihi. Kukosekana kwa ustaarabu kwenye jamii, hupelekea watu kuwa na maisha ya hovyo. Jamii imekuwa siyo ya kuaminika na watu wamekuwa ni janja janja. Watu hawana …

Design a site like this with WordPress.com
Get started