Kwa chochote kile unachopenda kufanya sasa unaweza kukigeuza kuwa sehemu yako ya mafanikio. Unaweza kukigeuza kuwa sehemu ya dunia kukujua wewe kupitia kile unachofanya. Kuwa sehemu ya kutoa thamani kwa wengine na kufanya makubwa sana. Kama unakipaji, usife njaa kitumie kukuingizia fedha. Au chochote unachopendelea kukifuatilia, angalia ni namna gani unaweza kuongeza thamani kwa wengine …
Lazima Sababu Itokee
Hakuna jambo ambalo litatokea kwenye maisha yako bila sababu. Kwa mfano, ukichukua jiwe na kuliweka ndani haliwezi kuondoka hapo mpaka mtu aje alihamishe. Ili upate matokeo fulani kwenye maisha yako, lazima kuwe na sababu yaani kisababishi. Sheria ya sababu na matokeo(laws of cause and effects) ndiyo inayoendesha dunia. Hakuna kinachotokea bila sababu. Kwa mfano, hakuna …
Rafiki Wa Kweli
Kwenye maisha ukitaka kufika haraka, basi nenda peke yako.Na ukitaka kufika mbali, nenda na wenzako. Kwa maana hiyo basi, tunahitaji marafiki sana au kifupi tunahitaji watu wa kushirikiana nao ili tuweze kufika mbali. Lakini watu wa kushirikiana nao wamekuwa changamoto kubwa kwetu. Kazi zipo lakini watu wa kufanya nao kazi ndiyo shida. Kuna mtu mmoja …
Ushindani Wa Kijinga Kwenye Biashara
Kila mtu anataka kuuza zaidi kwenye biashara yake. Na pale mtu anapoona hauzi huwa anafikiria namna ya kuweza kufanya ili aweze kupata wateja. Sasa ujinga ambao wanafanya wafanyabiashara wengi pale ambao anaona hauzi ni kushusha bei.Watu wengi siku hizi wanajiita vunja bei wakiwa na imani kwamba wakipunguza bei watapata wateja wengi zaidi. Kama una biashara, …
Unachotakiwa Kujua Ni Hiki Hapa
Bilionea na mshirika mwenza wa Warren Buffett Bilionea Charlie Munger aliwahi kunukuliwa akisema,Ninachotaka kujua ni wapi nikienda nitakufa ili niepuke kwenda sehemu hiyo. Rafiki yangu nikupendaye, tafsiri rahisi ni kwamba jua ni mambo gani ukiyafanya utakufa na kisha acha kufanya kitu hicho. Kwenye kila eneo la maisha yetu kuna vifo. Vifo siyo tu vya binadamu …
Vitu Vitakavyokusaidia Kuendesha Biashara Yenye Mafanikio
Ni muhimu sana kuingia kwenye biashara unayoipenda na una uzoefu nao. Lakini lipo kosa la watu wengi ambalo wanakuwa wanafanya pale wanapokuwa wanafanya kitu wanachopenda. Kosa ambalo linawagharimu watu wengi ni kujua kile ambacho wanafanya zaidi kuliko kujua biashara yenyewe. Kwa mfano, kama mtu anajua na anapenda kupika chapati basi anaanzisha biashara ya chapati na …
Continue reading "Vitu Vitakavyokusaidia Kuendesha Biashara Yenye Mafanikio"
Jamii Isikuvuruge Kwa Tafsiri Zake
Jamii ina tafsiri mbaya pale unapoonekana unapenda sana kile unachofanya. Jamii inatafsiri mbaya pale unaoonekana unapenda sana fedha. Kifupi, jamii ina kisirani na mtu yeyote ambaye yupo tofauti. Jamii inawapenda watu ambao ni wa kawaida. Kwa sababu, jamii haitaki kuonekana wao ni wazembe kwa kushindwa kufanya makubwa hivyo kazi yao kubwa ni kuwafanya watu wajione …
Hiki Ndiyo Kitaamua Mafanikio Yako
Hakuna kitu kingine kitakachoamua mafanikio yako, zaidi ya mtazamo wako. Mtazamo wako utaamua mafanikio yako. Mtazamo wako ndiyo picha yako ya akili yako. Jinsi unavyoona vitu, ndivyo mambo yako yanavyokuwa.Ukiwa na mtazamo hasi au chanya na vitu vitakuja hivyo hivyo. Mafanikio yako yatatokana na kile unachoona iwe unaona uwezekano au unaona changamoto. Watu wengi wanafungwa …
Hata Wewe Ni Kikwazo
Huwa mtu anaposhindwa kwenye jambo lolote lile, huwa anatafuta sababu za kwa nini ameshindwa.Ni kawaida ya binadamu kutopenda kukubali kosa au kile alichofanya.Mara nyingi kitu kikitokea huwa tunatafuta sababu nani wa kumlaumu au kutafuta sababu nzuri ambazo zitaturidhisha ili kukwepa kukiri makosa yetu binafsi. Kuna vikwazo vya aina mbili kwenye maisha yetu. Moja ni vikwazo …
Elimu Ya Biashara
Rafiki yangu nikupendaye, Kitu kimoja unachotakiwa kujua ni kwamba, elimu ya biashara haijakamilika kama hakuna vitendo. Hata kama ungesoma vitabu vingi kiasi gani. Ukahudhuria kila aina ya mafunzo kuhusu biashara.Kumbuka, elimu yako ya biashara haijakamilika kama hujajifunza kwa vitendo. Siyo tu kwenye biashara bali pia kwenye kitu chochote kile. Elimu haifanyi kazi kama hakuna vitendo. …