Sisi binadamu tumetawaliwa sana na miili yetu. Tunaisikiliza miili yetu na inatuongoza kuamua mambo. Miili yetu kiasili haipendi bughudha, hivyo inapokutana na kitu ambacho kitautesa mwili unapeleka taarifa katika akili ya kukata jambo fulani. Tunatakiwa kuamua mambo yetu kwa njia ya kufikiri na siyo kuupa mwili nafasi, anayeusikiliza mwili wake atakuwa mtumwa wa wengine. Unajua …
Umekubali Mwenyewe Iwe Hivyo
Mara nyingi kile kitu ambacho ni muhimu sana katika maisha yetu huwa tunakipa uzito sana. Lakini kama siyo muhimu tunatengeneza mazingira ya kukichukulia poa. Umekubali mwenyewe kuwa hivyo ulivyo leo. Kwa mfano, kama unasafiri bila hata ya kuweka alamu lazima utaamka tu muda muafaka ili usiachwe na gari na muda mwingine unajikuta hata usingizi huna …
Usiende Kubishana Siku Hii Ya Leo
Usiende kupoteza nguvu zako bure katika kubishania mambo ambayo yako nje ya uwezo wako. Kubishana ni kupoteza nguvu na muda wako. Tumia muda wako kufanya kazi ambayo inakupatia kipato na mambo mengine achana nayo. Unapokuta watu wakibishana juu ya mpira, siasa, udaku wewe nenda kafanye kazi inayofanya maisha yaende. Badala ya kubishania mambo ambayo hayakuingizii …
Jinsi Ya Kujitofautisha Na Wafanyabiashara Wengine
Kufanya kile ambacho kila mtu anafanya hapo unakuwa umejijengea mazingira ya kuchukuliwa poa. Kama wote mnafanya biashara moja, na mteja akija kwako na akienda kwa mwingine anapata huduma hiyo hiyo hapo unakuwa bado huna thamani. Ili kujitofautisha na wafanyabiashara wengine unatakiwa kwenda hatua ya ziada. Unatakiwa kufanya kile ambacho watu wengine hawafanyi. Jijengee kutoa huduma …
Continue reading "Jinsi Ya Kujitofautisha Na Wafanyabiashara Wengine"
Hivi Ndivyo Vitu Saba Unavyopaswa Kuvilinda Kwenye Karne Hii 21
Viko vitu vingi sana ambavyo tunapaswa kuvilinda katika maisha yetu. kazi yetu kubwa katika maisha yetu ni kutengeneza, kukuza na kisha kukitunza. Haifai kutengeneza na kisha kuacha, hapana unapswa kutunza na kukuza kile ambacho umekianzisha au kukitengeneza ndani yako. Leo nakwenda kukushirikisha vitu saba unavyopaswa kuvilinda kwenye maisha yako na vitu hivyo ni kama ifuatavyo; …
Continue reading "Hivi Ndivyo Vitu Saba Unavyopaswa Kuvilinda Kwenye Karne Hii 21"
Kabla Hujapata mtu Sahihi Utapitia Hali Hii
Usiwaonee watu wote waliofanikiwa katika jambo fulani kuwa walifanikiwa kirahisi. Hapana, hakuna aliyefanikiwa kirahisi kwenye jambo lolote hata lile ambalo unaliona wewe ni rahisi. Kwa mfano, kila siku umeshajijengea imani kwamba ukiingia katika mtandao huu wa Kessy Deo lazima utakutana na kitu kipya. Ila mpaka unakuja kuiona makala imekwenda hewani kuna mchakato mkubwa sana umefanyika. …
Continue reading "Kabla Hujapata mtu Sahihi Utapitia Hali Hii"
Hii Ndiyo Tahajudi (meditation) Bora Kabisa
Asubuhi tunapoamka miili yetu inakuwa iko fuli chaji. Kama vile ilivyo simu, inapofika jioni betri zinakuwa zimeisha hii ni kutokana na kutumika kwa simu ndani ya siku nzima. Miili yetu inapokuwa imechoka inahitaji kupumzika na watu huwa wanapoona wamechoka wanakuwa wananunua vitu vya kuchangamsha mwili kama vile vilevi, kinywaji cha eneji cha kuongeza nguvu.Hii inakuwa …
Continue reading "Hii Ndiyo Tahajudi (meditation) Bora Kabisa"
Hiki Ndicho Kinachokufanya Wewe Ukose Kupata Bahati Yako
Kila binadamu ana bahati yake. Na wanasema kuwa, bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi. Kumbe basi, huwezi kuweka mikono mifukoni nakusubiria bahati yako ije bali, unatakiwa upambane kupata bahati yako. Kabla ya kuzaliwa kwetu, tulishabarikiwa na kitendo cha wewe kuzaliwa kibaiolojia wewe ni mshindi na umezaliwa kushinda.Ndiyo maana kila siku nakusihi sana uweze kujinenea …
Continue reading "Hiki Ndicho Kinachokufanya Wewe Ukose Kupata Bahati Yako"
Unaweza Kuweka Juhudi Lakini Huwezi Kuamua Hiki
Katika maisha unapaswa kujua kuwa kuna mambo ambayo yako ndani ya uwezo wetu na kuna mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu.Na hapa ndiyo falsafa ya ustoa inapoingia. Unaweza kuweka juhudi katika maisha yako, unaweza kufanya kila unachoweza lakini huwezi kuamua matokeo gani yatokee. Bahati huwa ina nafasi ya mwisho katika maisha yetu. Tunapaswa kuweka …
Continue reading "Unaweza Kuweka Juhudi Lakini Huwezi Kuamua Hiki"
Sababu Kuu Moja Kwanini Watu Hawapendi Kuweka Akiba
Kila mmoja wetu anajua umuhimu wa kuweka akiba katika maisha yake. Hakuna mtu anayejua kesho yake itakuwaje. Hakuna anayeamka na kujua leo ataenda kukutana na changamoto gani. Tunakutana na changamoto nyingi sana lakini ukiangalia changamoto zetu kama huna fedha unakuwa unaongeza matatizo zaidi. Na wote tunajua kuwa ukiwa na fedha utaweza kutatua matatizo yako mengi …
Continue reading "Sababu Kuu Moja Kwanini Watu Hawapendi Kuweka Akiba"