Kama Unataka Kujiona Hujui Fanya Haya

Hapa duniani unatakiwa kuishi kwa akili sana. Siyo tu kuishi kwa akili bali kuishi maisha yako. Kila mmoja wetu amepewa akili na akili ndiyo kitu kilichokutofautisha wewe na mnyama. Mnyama hana akili wala Imani uliyokuwa nayo wewe. Hivyo basi, kama unataka kujiona hujui basi anza kujifananisha na wengine. Kujifananisha na wengine ni utumwa, utajiona huna …

Hiki Nacho Kinahusika Katika Safari Ya Mafanikio

Ukisikiliza hadithi nyingi za mafanikio utasikia alianza na moja kisha akawa na tatu.Ni rahisi kusimulia ila hizi hadithi nyingi za mafanikio huwa zinakosa kitu kimoja ambacho kinampata kila mmoja wetu. Wanasema bahati ni pale maandalizi yanapokutana fursa.Ni kweli wala sina pingamizi juu ya hilo. Katika safari ya mafanikio kuna kitu kikubwa huwa watu hawakisemi ambacho …

Anza Mwaka Na Fikra Mpya

Fikra zilizotengeneza tatizo mwaka jana haziwezi kukusaidia kutatua tatizo jipya mwaka mpya. Unatakiwa kuwa mtu mpya katika kila eneo la maisha yako. Uache maisha ya mazoea na mbinu ulizotumia kushindwa mwaka jana usiendelee kuzitumia mwaka huu mpya. Badilisha gia kama gia uliyotumia mwaka jana haijakusaidia. Usiendelee kung'ang'ania kitu ambacho hakina msaada kwako na weka nguvu …

Kuhesabu Baraka Ni Kushukuru

William Arthur Ward aliwahi kusema, "kujisikia kutoa shukrani na kutoitoa ni kama kufunga zawadi na kutoitoa." Rafiki yangu, Natumia nafasi hii kukushukuru kwa kuwa mshirika mkubwa wa kazi zangu za uandishi katika mwaka 2019.Bila wewe kazi zangu hazina kazi. Kushukuru ni kuomba tena. Hivyo ninakuomba tena tuendelee kuwa pamoja mwaka 2020 tuendelee kushirikishana maarifa mazuri …

Hizi Ndiyo Siku Mbili katika mwaka ambapo hakuna Kinachofanyika

Kuna siku mbili katika mwaka ambapo watu huwa wanajidanganya sana katika siku hizi.Huenda katika mwaka kila siku watu huwa wanajipa matumaini mbalimbali lakini cha kushangaza hakuna anayefanikiwa ndani ya siku hizo. Huenda hata wewe umeshajidanganya sana Katika siku hizi mbili ambazo ni Jana na kesho. Kamwe kesho haitokuja kutokea katika maisha yako. Umejipotezea mengi sana …

Unaweza Kukubali Kushindwa Lakini…

Aliyekuwa bingwa wa mchezo wa kikapu Michael Jodarn aliwahi kunukuliwa akisema " ninaweza kukubali kushindwa lakini siwezi kukubali kutokujaribu. Huwa tukishindwa mara ya kwanza ni kama vile tumepewa tiketi ya kushindwa milele.Kushindwa kwa mara ya kwanza imewafanya watu wengi sana kutokuthubutu na kujaribu tena. Kuna watu ni ving'ang'anizi wa kujaribu mpaka wapate matokeo ndiyo wataweza …

Hapa Ndiyo Mahali Ambapo Dunia Inazaliwa

Kila mmoja wetu hapa duniani amezaliwa katika familia. Ni mpango wa Mungu kila mwanadamu kuzaliwa katika familia.Na kupitia familia ndiyo mahali dunia inapozaliwa. Kupitia familia zetu, tunajipatia miito mbalimbali duniani. Familia ndiyo nyumba ya dunia ambayo kila mmoja wetu anaishi na kujifunza misingi ya dunia. Familia zetu zikiwa takatifu zinafananishwa na mbingu ndogo hapa duniani. …

Nimewashinda Maadui Zangu Kwa Kuwafanya Kuwa Marafiki Zangu

Dalai Lama enzi za uhai wake aliwahi kusema kuwa nimewashinda maadui zangu kwa kuwafanya kuwa marafiki zangu. Hii ni kauli yenye nguvu sana katika mambo ya msamaha. Moja ya mbinu nzuri ya kuwavuta maadui zetu ni kuwafanya kuwa marafiki zetu kwa njia hii tunakuwa tunawamaliza bila kutumia nguvu. Hatuwezi kumaliza chuki kwa chuki bali tunaweza …

Kuanza Upya Siyo Ujinga

Hutakiwi kujilaumu pale mambo yanapokuwa yanakwenda ndivyo sivyo. Kwa lolote tunalofanya , basi chochote kinaweza kutokea. Hakuna mkataba kuwa kila tunalofanya basi mambo yataenda kama vile tunavyotaka sisi. Huko ni kujidanganya kweli, Mambo yanaenda vile yanavyotaka yenyewe. Unapo,pokea na kupoteza shukuru na jifunze tena. Na ikibadi anza upya kwani kuanza upya siyo ujinga. Huenda ulipanga …

Kuwa Kiherehere Wa Maisha Yako

Kama kila mtu angekuwa kiherehere wa maisha yake, basi mambo yangekuwa mazuri kweli. Watu wengi siyo vinara wa kufuatilia mambo yao binafsi bali watu ni vinara kwa kufuatilia maisha ya watu wengine. Tunatumia muda na gharama kubwa katika kufuatilia mambo ya watu wengine huku ya kwetu tukiyaacha bila kuyafanyia kazi. Kabla hujaanza zoezi la kumfuatilia …

Design a site like this with WordPress.com
Get started