Hii Ndiyo Njia Bora Ya Kuaminika Na Wengine

Kama unataka kuuza kitu chochote kwa wengine hakikisha kwanza umejenga uaminifu. Watu wanapenda kununua sehemu ambayo ina uhakika. Na uhakika unajengwa mahali ambapo kuna uaminifu wa hali ya juu. Je nawezaje kujenga hali ya kuaminika kwa wengine? Jawabu; Anza kujiamini wewe mwenyewe kwanza. Ukitaka watu wakuamini na wewe hujiamini, mfano mzuri, kama mtu anauza kitu, …

Maisha Chanya Hayaletwi Na Akili Hii

Mchezo mzima uko katika akili ya binadamu. Mambo yote tunayoyaona kwa nje basi yalianzia ndani ya akili. Akili ikiyumba na maisha yako yatayumba pia. Akili ikinenepa na mwili wako pia utanenepa. Maisha mazuri yanaletwa na akili chanya. Akili hasi kamwe haiwezi kukupa wewe maisha chanya. Watu huwa hawaamini hili lakini ona ushuhuda katika maisha yako …

Hii Ndiyo Akaunti Unayopaswa Kuilinda Kuliko Zote

Najua kila mtu ana akaunti, wako ambao wana akaunti za akiba, uwekezaji, kazi , biashara na akaunti nyingine zinazofanana na hizo. Leo ninakwenda kinyume na akaunti zote duniani na kukuambia akaunti moja muhimu ambayo huwa hauipi uzito kama akaunti nyingine. Licha ya kuwa akaunti muhimu kuliko zote lakini watu wanaichukulia poa tu. Tuko hapa duniani …

Hawa Ndiyo Mabingwa Wa Kuapa Na Kugeuka Duniani

Taaluma mbalimbali, miito mbalimbali kama vile ndoa watu huwa wanakula kiapo. Viongozi serikalini wanapopewa nyadhifa fulani huwa wanaapa. Kila mtu kadiri ya imani yake, anashika kama ni Qouran, Biblia ana apa kuwa atakua mwaminifu kutokana na cheo alichopewa.Watawa nao hivyo hivyo wanakiri nadhiri zao.Wanandoa nao huwa wanakiri na kula kiapo kuwa wataishi kwa uaminifu na …

Njia Moja Ya Kuepuka Kukosa Fedha Kabisa Katika Maisha Yako

Ni kawaida watu wengi huwa wanalala huku wakifikiria kesho watakula nini au watapataje hela ya kula. Hebu jiulize inakuwaje mtu anakua hana kabisa hela? Liko jawabu rahisi sana kwanini mtu anakua hana hela kabisa. Jibu ni moja tu hana thamani anayoitoa. Msingi wa fedha ni kutoa thamani, sasa kama huna thamani unayotoa maana yake huna …

Huyu Ndiye Mtu Ambaye Huwezi Kumdanganya

Yuko mtu ambaye anakujua vizuri kuliko hata watu wengine na mtu huyo siyo mwingine bali ni wewe mwenyewe. Utaweza kuwadanganya watu wote lakini ukweli ni kwamba huwezi kujidanganya wewe mwenyewe. Ukiangalia maisha yako, jinsi unavyoishi ndiyo utajua kama unawadanganya watu au la. Je hayo ndiyo maisha yako halisi? Kama siyo kwanini unaendelea kuishi maisha ambayo …

Hii Ndiyo Hatua Ya Mtu Anayetaka Kufanya Kitu

Siku zote mtu anayetaka kufanya kitu huwa anakua hana sababu za kutaka kufanya bali;Anafanya tu. Kwa mfano, mtu anayetishia anataka kujinyonga huyo basi hataki kujinyonga bali anatishia tu ili aweze kupata kile anachotaka. Watu wengi huwa wanawatishia wale watu wao wa karibu kuwa wanataka kufanya kitu fulani basi wale wa karibu wanawaomba wasifanye hivyo halafu …

Bado Hujaamua Kukipata Kitu Hiki Ndiyo Maana Hukipati

Mtu mmoja alikuwa anasoma gazeti nyumbani kwake, mara akatokea mgeni akamuuliza vipi mbona mbwa wako analia hivyo? Akamjibu, amekalia msumari, yule mgeni akamwambia kwanini sasa usimtoe?Akamjibu, kama ingekuwa msumari umemchoma vizuri angetoka hapo alipo asingeendelea kulia. Hii ni hadithi fupi, lakini ina funzo ndani yake. Hii iko hata katika maisha yetu ya kawaida wako watu …

Jinsi Ya Kuwa Na Nguvu Ya Akili

Utakua mkali sana pale mtu anapokuja kuuchezea au kuushika mwili wako bila ridhaa yako. Je utakua tayari kuuanika mwili wako na watu wauchezee vile wanavyotaka? Kama huwezi kufanya hivyo, kwanini sasa unaruhusu watu waichezee akili yako vile wanavyotaka? Umekuwa ni mteja wa kila habari, huchagui wala kuchuja kile kinachoingia akili kwako. Akili yako ndiyo kiwanda …

Haya Ndiyo Mafanikio Unayopaswa Kuwa Nayo

Iko wazi kila mtu ana ndoto yake hapa duniani. Lakini cha kuchangaza wako watu ambao wala hawana ndoto. Kuna binadamu wengine wako kama vile wanyama wanachojua wao ni kula tu. Wako ambao wanaishi ili wale na wako ambao wanakula ili waishi. Vipi ile ndoto yako uliyokuwa nayo kwa sasa umefikia wapi? Nasikitika kuwa ndoto za …

Design a site like this with WordPress.com
Get started