Mtu Mwenye Akili Huwa Anafanya Vitu Kwa Namna Hii

Mtu ambaye akili yake haiko sawa huwa anafanya vitu kwa kutokuwa na sababu. Chochote kile ambacho kinamjia kwenye akili yake yeye anafanya tu bila hata kufikiri. Lakini kwa kuwa wewe ni mtu mwenye akili timamu basi kuwa na sababu za msingi pale unapotaka kufanya jambo. Usifanye kwa sababu ya hisia, bali fanya kwa sababu unayo …

Ukipata Fedha Ni Kama Vile Umenunua Dawa Mpya Ya Meno

Natumaini kila mmoja huwa anatumia dawa ya meno. Ukiwa na dawa ya meno mpya unakuwa unajiachia kutumia vile unavyotaka na unaamini kuwa haitoisha na ikianza kuisha ndiyo umakini wa kutumia dawa unaanza. Hiyo hali iko hata katika fedha, tukipata fedha tunatumia vibaya mpaka pale inapoisha ndiyo tunakuja kushtuka na akili inarudi hivi imekuwaje mpaka hela …

Njoo Na Kitu Hiki Ambacho Watu Watakuwa Tayari Kulipia Pesa

Hakuna kitu kigumu kama mtu kutoa pesa yake ambayo ameipata kwa shida. Wako wako tayari kutoa fedha yao pale ambapo wanakuwa wamepata suluhisho la tatizo lao. Njoo na suluhisho ambalo watu wako tayari kulipia pesa. Kama huna fedha jiulize, je ni suluhisho gani ambalo naweza kuja nalo na watu wakawa tayari kulipia pesa? Kila mtu …

Njia Nzuri Ya Kuwavuta Watu Wako

Ni upendo. Aliyekuwa mtawala wa Ufaransa, mbabe wa kivita na jemedari wa kijeshi Napoleon Bonapart aliwahi kunukuliwa akisema, nimewavuta watu wangu kwa mabavu lakini Yesu amewavuta watu wake kwa upendo. Hapa tunapata fundisho kubwa sana, ukitaka kuwavuta watu na wakuweke moyoni wavute kwa upendo na siyo mabavu. Utafanikiwa kuwavuta kwa mabavu lakini yatakuwa hayadumu ila …

Kabla Hujakosoa Jiulize Swali Hili

Ni kawaida yetu sisi binadamu kupenda kukosoa zaidi kuliko kupongeza. Wako watu ambao wanapenda kuona mabaya tu pale mtu anapokuwa amejaribu kufanya kitu. Badala ya kupongeza yeye atakosoa kwa nini isiwe hivi. Ukitaka kujenga mahusiano yako, usiwe mtu wa kukosoa bali kuwa mtu wa kupongeza. Ukishamkosoa mtu tayari hamtaweza kukubaliana kwenye jambo lolote lile. Katika …

Jinsi Ya Kujikaanga Na Mafuta Yako mwenyewe

Kwa matokeo yoyote uliyonayo sasa huna wa kumlaumu zaidi ya wewe mwenye. Kwa sababu wewe ndiyo mpishi mkuu wa kile unachokula. Matokeo unayopata sasa yawe ni mazuri au mabaya mzalishaji ni wewe. Ukiona kwa sasa huna fedha ujue wewe ndiyo umesababisha hayo. Kama huna fedha maana yake huna thamani unayotoa au hakuna matatizo unayotatua kwani …

Unapokuwa Kwenye Kiwango Hiki Watu Watakuona Tishio

Ni asili ya binadamu kuwa mtu unapokuwa chini watu hawakuoni kama ni tishio. Ukiweka juhudi kila kitu kinawezekana. Na tabia ya watu ni kwamba ukikaa nao hawapendi kukuona ukibadilika. Sehemu yoyote ile mtu ukiwa tofauti na wengine lazima utapigwa vita. Ukiwa ni mtu ambaye umewazidi wenzako kwa kitu chochote kile, wale ambao hawana lazima watakuona …

Design a site like this with WordPress.com
Get started