Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kushindwa Kitu Ambacho Kipo Ndani Ya Uwezo Wako

Huo ni uzembe mkubwa.

Usikubali kushindwa kwa kitu ambacho tayari unao uwezo wa kila namna kukishinda..

Unapopata nafasi yoyote ile, itumie vizuri kwa sababu usipoitumia nafasi ambayo iko ndani ya uwezo wako baadae itakuja kukutesa sana kisaikolojia.

Utaanza kujilaumu laiti ningelijua, usikubali upitie maumivu ya laiti ningelijua kwa ni fedheha kubwa kwako. Kama unaweza kushinda, shinda kweli ili baadaye usije ukajilaumu.

Kama unaweza kupata moja kwa nini usipate na mia? Kila kitu kinawezekana.

Angalia ni uzembe gani ambao unaufanya kwenye eneo la fedha na ulifanyie kazi mara moja.
Kwenye fedha hakikisha mapato yako yanakuwa makubwa kuliko matumizi yako.
Hakikisha unaweka akiba, unawekeza.

Usisubiri mpaka nguvu ziishe ndiyo uchukue hatua, fanya sasa wakati ukiwa na nguvu zako.

Angalia ni uzembe gani unaoufanya kwenye kazi au biashara na ufanyie kazi mara moja. Usikubali hata siku moja laiti ningelijua ije kukuumiza.

Futa manung’uniko yote kwenye maisha yako kwa kufanya kile kinachowezekana kwako kufanya.

Usikubali mgonjwa afie mikononi mwako kwa uzembe, pambana kwa kila namna mpaka mgonjwa apone. Usijipe sifa mbaya wakati unao uwezo wa kuzivunja.

Kwenye maisha kila kitu kinatokea kwa sababu lakini vitu vingine vinatokea kwa sababu ya uzembe. Usikubali ushindwe maisha kwa sababu ya uzembe wako ambao uko ndani ya uwezo wako.

Usikubali hata siku moja kitu unachoweza kufanya ukishindwe kwa uzembe. Epuka uzembe kwenye maisha yako kwa kuwa makini.

Bahati huwa haiji mara mbili, kila unapopata nafasi itumie vizuri sana. Kila mmoja anajua kuna kifo hivyo usiishi kizembe leo kwa kutegemea kesho kwa sababu kesho huijui ishi leo kama vile ndiyo siku yako ya mwisho hapa duniani.

Ukipewa dhamana itumie vizuri sana. Ukikabidhiwa namba cheza namba yako vizuri kwa sababu wako watu wanaokutegemea wewe kwa namba unayocheza. Unapocheza vibaya unaleta shida kwa wengine.

Hatua ya kuchukua leo; Usikubali kushindwa kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako.
Pambana kushinda kwa kila unachoweza na usifanye uzembe kwa kitu ambacho unakiweza.

Usikubali wengine wapate shida kwa sababu ya uzembe wako. Kuwa makini kwenye kila eneo la maisha yako.

Muhimu;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: