Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tegemea Kupata Kitu Hiki Kutoka Kwa Mtoto Wako

Watoto wanakupa kile ambacho wewe mzazi unawapa watoto. Kama unawapa upendo basi watoto watakurudishia upendo. Baadhi ya wazazi wanalalamika kuwa watoto hawawajali pale wanapokuwa wakubwa. Kama mzazi hukumjali mtoto wako akiwa mdogo unategemea na yeye akujali ukiwa umezeeka? Kumbuka unavuna kile ulichopanda, usitegemee kuvuna kitu ambacho hujakipanda kutoka kwa mtoto. Kwa mfano, kama mzazi hujawafundisha …

Somo Muhimu Unalopaswa Kuwafundisha Watoto Wako

Mzazi ndiye mwalimu wa kwanza katika familia na malezi kwa ujumla. Lakini baadhi ya wazazi huwa wanaamini kwamba walimu mashuleni ndiyo wana jukumu hilo la kuwafundisha watoto. Kitu ambacho napenda kukujulisha wewe kama mzazi, mlezi au mzazi mtarajiwa ni kwamba wafundishe watoto wako somo muhimu la kutotoa siri za familia yako. Kwanini nasema hivyo? Wako …

Neema Tumepewa Bure, Ili Upate Baraka Unapaswa kufanya Hiki

Kila mmoja wetu amepewa neema bure kabisa lakini vipi kuhusu baraka? Baraka nayo ni nguvu ya asili inayofanya kazi ndani yetu. Baraka huwa haiji kama neema, ili upate baraka unatakiwa kufanya kazi. Baraka inapatikana kwa kufanya kazi, kwa kufanya kitu fulani ndiyo uweze kuipata. Bila kufanya kitu baraka haiwezi kukupata. Kwa mfano, tunapata baraka pale …

Wekeza Kwa Watu Hawa Muhimu Sana Kwako

Kama ikitokea umekufa leo usiku, mwajiri wako atatangaza nafasi ya kazi mwisho wa mwezi kuziba nafasi yako. Lakini familia yako, wapendwa wako na marafiki zako watakukosa daima.Usiwe bize sana kuishi maisha na kusahau kutengeneza maisha. Hayo ni maneno ya bilionea Elon Musk. Kwa hekima hiyo hapo juu, watu wanakula maisha lakini wanasahau kuwatengenezea watoto wao …

Andaa Mazingira Yako Mwenyewe Wala Usimtegemee Mtu Huyu Hapa

Sisi binadamu kiasili ni wabinafsi. Huwa tunaanza kujifikiria sisi wenyewe kwanza ndiyo tunawafikiria wengine baadaye. Wako baadhi ya wazazi wanayo dhana kwamba wanazaa watoto ili wale watoto waweze kuja kuwasaidia baadaye. Ni mawazo mazuri kweli wako ambao wanafanya hivyo na watoto walio wazaa wanakuja kuwasaidia. Lakini baadhi ya wazazi wanafikia mahali wanajuta na kusema kweli …

Huna Mkataba Wa Kuishi Naye Milele

Vitu vyote ambavyo tunafanya hatuna uhakika navyo asilimia mia moja. Kitu ambacho kwa kila mmoja ana uhakika nacho asilimia mia moja ni kifo tu. Haya mambo mengine yote hatuna uhakika nayo kwa sababu ni vitu ambavyo viko nje ya uwezo wetu. Wazazi kuwapenda watoto wao ni kitu kizuri sana. Lakini, baadhi ya wazazi wanajisahau sana …

Tengeneza Mifumo Hii Ili Watoto Wako Waje Kufaidi

Kama wewe ulianzia sifuri yaani zero. Ulikuwa huna kitu, ukapambana na kufikia mafanikio ya juu, hakikisha unalinda kile ulichopata ili kizazi chako kisije kupata shida. Nguvu zako zisiende bure, fanya kazi mara moja na achia urithi kizazi chako. Na njia nzuri ya kuachia kizazi chako urithi ni kutengeneza mfumo imara. Usiwaachie watoto wako mzigo wakuja …

Usimwadhibu Mtoto Hili Siyo Kosa Lake

Mpendwa rafiki yangu, Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hakuna mtu anayeandika barua ya kuomba kuwa na mtoto bali mtoto ni matunda ya ndoa. Kama sisi wote tulikuwa watoto, tulizaliwa hatujui kitu. hivyo vitu vingi ambavyo unajua leo ni kwa sababu umejifunza au umefundishwa. Kwa mtoto ambaye uko naye sasa kama hajui kitu hilo siyo …

Jinsi Ya Kumjengea Mtoto Wako Tabia Za Kitajiri

Mpendwa rafiki, Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hakuna aliyeandika barua ya kuomba kuzaliwa na hakuna aliyeomba au kuchagua mzazi ambaye anaye sasa bali wote tumejikuta tunao wazazi ambao leo hii tunao. Mtoto anamtegemea sana wazazi wake kumpa msingi wa maisha bora, kama mzazi hajielewi na hana ramani katika maisha yake ni wazi kwamba naye …