Furaha Ya Kweli Inatoka Hapa

Shabaha ya kila mmoja wetu hapa duniani ni kuwa na furaha. Wengi tunajikuta tukifanya hiki au kile ili tupate furaha. Tunajiambia tukiwa na vitu fulani basi tutakua na furaha lakini kitu kama hicho hakiji kutokea kwenye maisha. Tumekuwa ni watu wa kukimbizana na vitu kuanzia mwanzo wa mwaka mpaka mwisho wa mwaka. Tumekuwa tunakimbizana na …

Kuna Sababu Mtu Kufanya au Kutokufanya Kitu

Kwenye maisha unapaswa kujua saikolojia ya watu. Usipojua saikolojia ya watu utapata shida, lakini utakapoijua wala hawatakusumbua. Watu wanafanya kitu au kutokufanya kitu kwa kuu mbili;Moja, hawajui. Ukiona mtu anashindwa kufanya kitu sababu ya kwanza huenda ikawa hajui. Kabla hujamlaumu na kumgombeza kaa chini muulize je, unajua unachopaswa kufanya? Wakati mwingine mpaka unaona mtu anafanya …

Kitu Muhimu Cha Kufanyia Kazi Kwenye Mauzo.

Kama tulivyojifunza kwenye kitabu cha CHUO CHA MAUZO, kwamba mauzo ndiyo moyo wa biashara. Na ushindi mkubwa kwenye mauzo ni pale mteja anapotengana na fedha zake. Mteja anapokuja kwenye kile unachouza, punguza chenga nyingi na hakikisha unafunga goli la haraka ili upate ushindi. Chenga hazina maana kama hujapata ushindi. Usiogope kuuza, pale unapogundua maumivu ya …

Njaa Inayowasumbua Watu Wengi

Watu wana njaa ya kusifiwa. Ni kawaida yetu sisi binadamu kupenda kusifiwa. Kila mtu anapenda kusifiwa, kama utaweza kuwasifia watu kwa kile wanachofanya au walichofanya utaweza kujenga ushawishi na kukubaliana nao.Kwa kila mtu unayekutana naye, tafuta kitu cha kumsifia. Maisha ni mauzo, hivyo wewe kama muuzaji unatakiwa kuwasifia wateja wako. Wasifie watu wako wa karibu, …

Njia Rahisi Ya Kupata Matokeo Ya Tofauti

Njia hiyo ni kufanya kitu cha tofauti. Wanasema, ujinga ni kufanya kitu kile kile halafu unategemea kupata matokeo ya tofauti. Ili upate matokeo ya tofauti kanuni ni moja tu, fanya kitu cha tofauti. Kwa mfano, hujawahi kujifanyia tathmini ya kujua kama unaenda mbele au la, fanya kitu cha tofauti kwa kujifanyia tathmini. Hujawahi kutabasamu, fanya …

Unafanya Nini Kwenye Biashara Yako?

Rafiki yangu nikupendaye, Uko kwenye biashara kwa lengo kutoa thamani kubwa kwa wengine kupitia kile unachofanya. Na uhai wa biashara yako ni MAUZO. Kwa sababu mauzo ndiyo yanayoleta fedha kwenye biashara na fedha ndiyo damu ya biashara bila fedha biashara haiwezi kwenda mbele. Chochote ambacho hakikui huwa kinakufa. Hivyo, kama kile unachofanya kwenye kazi au …

Ni Heshima Gani Unaipata Kwenye Umasikini?

Kifupi, hakuna heshima yoyote kwenye umasikini zaidi ya kupata fedhea tu. Umasikini ni adui yetu, tunapaswa kupambana naye kila siku na usikubali umasikini ukupige wakati una nguvu za kufanya kazi. Na kumbuka, umasikini huwa hauanzii mfukoni, unaanzia kwenye akili. Hakuna mtu masikini duniani ila kuna akili masikini duniani. Ukitaka uheshimike na kupata heshima yako unayostahili …

Njia Ya Uhakika Ya KufikiaUbilionea

Kama unataka kuwa na uhuru wa kifedha na kufikia VIWANGO vya juu kabisa vya ubilionea basi unapaswa kufanya biashara. Kwa sababu biashara ndiyo njia ya uhakika ya kufikia ubilionea. Ila biashara siyo mchezo rahisi, ni mgumu lakini una ushindi mzuri. Kama unataka kuwa na maisha ya kawaida, endelea kufanya vitu vya kawaida ila kama unataka …

Bahati Haiji Kwa Namna Hii

Bahati haiji ukiwa umeweka mikono mifukoni. Bahati inakuja pale unapokuwa umekaa kwenye mchakato wa kuyafanyia kazi kitu fulani. Hakuna mbadala wa kazi. Lazima ufanye kazi ili uweze kukutana na bahati yako.Bahati inatengenezwa, je, umekaa katika mchakato wa kutengeneza bahati yako? Bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi. Kumbe basi, ili ukutane na bahati, lazima uwe …

Usiruhusu Vitu Hivi Kuwa Ndani Yako

Kama binadamu huwa tunapitia mengi kwenye maisha yetu ya kila siku. Kuna watu watakuchukia na kutamani uanguke. Lakini hupaswi kuwachukia na kuwawekea vinyongo. Bali, wasamehe na watakie mema. Ili usiruhusu chuki au hasira kuwa ndani yako.Chuki na hasira ikikaa ndani yako utakua na maisha shida.Maisha yako ni mafupi sana kuhangaika na mambo yasiyokuwa na maana. …

Design a site like this with WordPress.com
Get started