Unataka Maisha Au Mafanikio?

Kama unataka mafanikio makubwa, basi pambana na elimu binafsi. Ila kama unataka kuwa na maisha ya kawaida basi elimu ya darasani inatosha kukupa maisha. Ukiendelea kutegemea elimu ya darasani, itakutesa, ili maisha yasikutese usitegemee tu elimu ya darasani bali jiongeze kwa kutafuta maarifa binafsi. Elimu ya darasani itakuwezesha kupata kazi ya kawaida, ambayo itakupa maisha …

Hii Ndiyo Adhabu Mbaya Kuliko Zote Duniani

Ni bora mtu achukue fimbo akuadhibu kuliko akuadhibu kwa njia ya kupuuzwa. Kupuuzwa ni adhabu mbaya kuwahi kutokea. Ni adhabu ambayo inakuwa inakunyanya kiakili. Ukishakuwa mtu wa kawaida kwenye maisha yako, dunia lazima itakupuuza. Ukiwa kawaida kwenye ndoa yako, mke au mume atakupuuza. Jitahidi kuwa mtu ambaye unaenda hatua ya ziada ili usipuuzwe na mwenza …

Watu Huwa Wanathamini Kitu Hiki

Kitu chochote ambacho huwa kinapatikana kiurahisi watu huwa hawakithamini hata siku moja. Kama kitu kinapatikana kiurahisi watu wanakuwa hawakipi umakini tu kitu hicho kwa sababu wanajua wakitaka watakipata. Watu Huwa wanathamini kile ambacho hakipatikani kwa urahisi. Watu wanapenda uhaba, kile ambacho ni adimu watu wanakithamini sana na kukipambania. Jifunze kujiongeza thamani kwenye maisha yako. Kuwa …

Kama Kuna Kitu Hukipendi Kibadili Wewe Siyo Mti

Mwanafalsafa Jim Rhon aliwahi kunukuliwa akisema, kama hupendi jinsi vitu vilivyo, vibadili, wewe siyo mti. Kwenye jamii yetu watu wanalalamika, watu wanapokosa kitu njia pekee ya kujifariji ni kulalamika. Badala ya kuchukua hatua, wao kulalamika ndiyo njia kwao. Kama maisha yako unayoishi huyapendi, yabadilishe wewe siyo mti badala ya kutumia muda wako kulalamika.Kama ni kazi …

Usipolipa Uzito Litapita

Mambo mengi ambayo unayapa uzito ndiyo huwa yanatokea kweli maisha yako.Yale ambayo huyapi uzito, yanapita tu yenyewe. Chochote ambacho unakipa umakini kwenye maisha yako ndiyo huwa kinatokea kweli. Kumbe, hata zile changamoto ambazo huwa tunazipuuzia huwa hazitusumbui. Jambo lolote ambalo hulipi uzito kwenye maisha yako huwa linapita lenyewe. Binadamu tumeumbiwa kusahau, laiti kama kila kitu …

Kifo Cha Mafanikio

Kile ambacho kimezoeleka kufanyika ndiyo kifo cha mafanikio. Kama unafanya kile ambacho kila mtu anafanya, kwa mtindo ule ule halafu unategemea kupata matokeo tofauti tegemea kupata anguko hapo.Watu wengi wanaoleta mazoea wanayazika mafanikio yao mapema.Watu wengi wanaoshindwa huwa wanafanya vitu vinavyofanana, lakini wanaofanikiwa wanaofanikiwa vitu vya tofauti. Watu wanatofautiana kwenye masaa ya kufanya, namna wanavyoendesha …

Jifunze Ujuzi Huu Kwenye Maisha Yako

Kama kuna ujuzi ambao unataka kujifunza kwenye maisha yako, basi jifunze sayansi na sanaa ya kuuza. Kwa nini? Kwa sababu kuuza ndiyo msingi wa kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako. Kwenye maisha yako kila kitu ni mauzo. Unauza kwenye ajira, unaunza kwenye mahusiano, unauza kwenye biashara.Kama unataka kuwa kiongozi bora jua jinsi ya  kuuza …

Kitu Cha Kujifunza Kutoka Kwa Muuza Samaki Aina Ya Nguru

Yamaguchi ni muuzaji wa samaki mwenye mafanikio makubwa sana. Analala masaa matatu tu kwa siku na anahudumia migahawa zaidi ya elfu moja Yukitaka Yamaguchi ni raia wa Japan ambaye ameanza kuuza samaki tokea mwaka 1980. Anaitwa mfalme wa samaki na mtu akiitwa mfalme maana yake amebobea kweli kwenye kitu hicho. Kitu kikubwa nilichojifunza kutoka kwa …

Mtu Akikupa Ahadi Fanya Hivi

Watu wengi tumekuwa tukipewa ahadi na watu mbalimbali, tunapewa ahadi na watu lakini ahadi hizo huwa hazitekelezwi. Kwa nini kwa sababu hakuna ufuatiliaji.Ili ahadi zikamilike lazima zifuatiliwe. Watu huwa wanafanya pale wanapofuatiliwa. Kama unataka mtu akupe fedha, unatakiwa kumfuatilia. Mteja akikuambia nitakutafuta, usisubiri mpaka aje kukutafuta bali mfuatilie kwenye ahadi yake. Kama unataka kupata fedha, …

Ukishajua Kile Unachotaka

Hicho pekee ndiyo kinapaswa kuwa kipaumbele kwako.Komaa nacho mpaka ukipate. Sema hapana kwa yote ambayo hayana mchango kwako.Utashawishiwa na vitu vingi ambavyo havihusiani na unachotaka, lazima uwe na nidhamu ya kusema hapana na kuweka umakini wako wote kwenye kile unachotaka.Haijalishi wazazi wako, ndugu zako, wafanyakazi wenzako na hata jamii inasema na kufanya nini, jua hakuna …

Design a site like this with WordPress.com
Get started