Ukitaka kufanya kitu kwenye maisha yako lazima uanze kidogo ili ujifunze. Watu wengi WANASHINDWA haraka mbele ya safari kwa sababu walianzia juu. Ukianzia chini hata ukianguka hutoumia kuliko ukianzia juu. Kwa mfano, mtu anayetaka kufuga kuku akianza na kuku 10 hata akianguka hatoumia sana. Kuku 10 watampa uzoefu mkubwa sana kwenye maisha ya ufugaji. Lakini, …
Huyu Ndiyo Muuzaji
Kila mtu ni muuzaji.Muuzaji ni yule anayemshawishi mwenzake. Kitendo cha wewe kuweza kumshawishi mwenzako kukubaliana na wewe huo ni uuzaji. Siyo lazima anunue bidhaa, ila hata kukubaliana na wewe tu kimawazo ni uuzaji.Uuzaji ni kitendo cha kubadilishana imani. Kifupi, uuzaji ni mbadilishano wa imani, mmoja anamshawishi mtu ili aweze kukubaliana na kile anachokiamini.Ukisema wewe siyo …
Usiangalie Changamoto Unazopitia
Kwenye maisha hakuna eneo ambalo unaweza kwenda na unakuta hakuna changamoto. Au ulishawahi kuona nyumba gani iliyobandika bango mlango lenye ujumbe huu hapae. HAPA HAKUNA MATATIZO.?binafsi sijawahi kuliona hilo bango. Hii ina maana gani kwetu? Ina maana kwamba, hakuna sehemu ambayo ni salama hapa duniani. Kila sehemu ambayo unafikiria ukifanya kazi ndiyo utakutana na bango …
Huwezi Kukimbia Mchakato
Warren Buffett amewahi kusema huwezi kupata mtoto ndani ya mwezi mmoja kwa kuigawa mimba moja kwa wanawake 9. Mimba lazima ichukue miezi 9 kukamilika kuwa mtoto. Ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote lile, unapaswa kukaa kwenye mchakato wa kile unachotaka. Usikimbilie matokeo kabla hujakaa kwenye mchakato. Kama tulivyooona kutoka kwa Warren Buffett, huwezi kurahisha kazi …
Kwa Sababu Ya Tabia
Vitu vyote watu ambavyo huwa unaona watu wakifanya jua ni tabia. Hakuna mtu ambaye anaweza kufanya kitu ambacho ni nje ya tabia yake. Huwezi kumkuta mtu anaamka asubuhi na mapema kama siyo tabia yake, na hata akiamka mapema anaenda kufanya nini huo muda kama hana malengo makubwa? Kama mtu siyo tabia yake hawezi kufanya, kwa …
Jinsi Ya Kujua Kama Mtu Amefanya Au Hajafanya Kitu
Ukiona mtu anakuzungusha kukupa mrejesho wa kitu fulani, jua kwamba hajafanya kitu hicho. Kwa mfano, kama unapaswa kufanya tathmini yako na kuiwasilisha mahali, kama umefanya utaituma mara moja lakini kama hujafanya changamoto ndiyo inaanzia hapo. Mtu akiwa amefanikiwa kitu, atakua anatamani sana aonyeshe kazi yake.Anakuwa na hamasa ya kutaka watu wengine wajue. Sisi binadamu ndivyo …
Continue reading "Jinsi Ya Kujua Kama Mtu Amefanya Au Hajafanya Kitu"
Utawashawishi Watu Kwa Kitu Hiki
Njia nzuri ya kuwashawishi watu kwenye maisha yako ni kuwashawishi kwa matokeo. Matokeo yana nguvu kubwa ya kumfanya mtu akubaliane na wewe kirahisi. Kama wewe ni muuzaji, ukitaka kuwashawishi watu wakubaliane na wewe kwenye kile unachouza, waonyeshe matokeo wanayokwenda kuyapata. Watu wanaamini sana kwenye matokeo kuliko kitu chochote kile. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu …
Watu Hawapati Fedha Kwa Sababu Hii
Watu wanatafuta hela ndiyo maana hawapati hela. Ukiwa ni mtu wa kutafuta hela, utapata shida kupata hela kwa sababu, ili upate hela unatakiwa utoe HUDUMA. Watu wengi hawatoi huduma ndiyo maana hawapati hela. Kwa mfano, mtu mwingine akiwa ameshapata hela haendelei tena kutoa huduma kwa sababu ana hela ya kula. Kwenye kutoa huduma bora ndiyo …
Usiweke Matumaini Kwenye Kitu Hiki
Usiweke matumaini yako kwenye kitu hewa. Usiweke matumaini kwa kitu chochote ambacho hujakifanyia kazi kwani hayo ni matumaini hewa tu. Mtu akishakuonesha dalilli nyekundu kwenye kitu chochote kile, usiweke matumaini yako kwake badala yake msaidie kufanya maamuzi kupitia kile anachotaka kutokana na dalilli nyekundu alizokuonesha.Watu wengine wanakuonesha kabisa dalilli nyekundu kwamba hataki kitu fulani lakini …
Kuwa Na Chujio
Kwa dunia unayoishi sasa, mambo ambayo yanateka umakini yako ni mengi sana ukilinganisha na faida unazopata. Unatekwa umakini wako, tokea unaamka mpaka unaenda kulala. Lazima uchuje watu unaojijusisha nao kila siku, siyo kila mtu ni wa kumpa muda wako. Siyo kila mtandao wa kijamii unapaswa kuwepo. Siyo kila habari inayotoka unapaswa kuijua, ukitaka kuwa mtu …