Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Niliyojifunza Katika Kitabu Cha The Total Money Makeover

Habari ya leo Mpendwa Rafiki na Msomaji wa mtandao wa Kessy Deo. Natumaini hujambo na unaendelea vizuri Rafiki hivyo basi, napenda kutumia nafasi hii kukualika katika makala yetu ya leo ambapo leo nitakushirikisha mambo ishirini niliyojifunza kupitia kitabu cha The Total money makeover.
Mambo muhimu niliyojifunza katika kitabu cha The Total money makeover kilichoandikwa na mwandishi Dave Ramsey.
Karibu, nikushirikishe Yale niliyojifunza kupitia uchambuzi huu wa kitabu.

Image result for the total money makeover

1. Dunia inaendeshwa na sheria ya asili huwezi kupata kitu bila kufanya kitu.
Siku zote unavuna kile ulichopanda kwa mfano kama ukipanda haba utavuna haba. Kama uliweka juhudi katika jambo lolote basi lazima utavuna juhudi ulizoweka awali na utapata matokeo kulingana juhudi ulizoweka.

2. Pale majanga yanapotokea yule aliyejianda katika kukabiliana na kuanguka kwa uchumi huwa anafaidika.
Yule mwenye uzoefu katika maisha ya kukabiliana na changamoto za kiuchumi huwa anafaidika sana. Uzoefu unalipa kwenye kila jambo katika maisha Yetu.

3. Matumizi mabaya ya fedha ni hatari katika uchumi. Huwezi kukua kiuchumi kama huna nidhamu nzuri ya pesa. Matumizi mabaya ya pesa ndio yanasababisha watu kuingia katika utumwa wa madeni kila siku.
Hivyo ni muhimu kuwa na matumizi mazuri ya pesa.

4. Elimu ambayo hatufundishwi mashuleni basi ni elimu ya fedha. Unatakiwa kujifunza zaidi kuhusu pesa na kuacha kuendelea kutumia fedha kimazoea.
Ni muhimu kujifunza elimu ya mambo ya fedha na kuitawala fedha na siyo fedha kukutawala.

SOMA;Njia Bora Ya Kumteka Na Kumfukuza Mteja Katika Biashara Yako

5. Unaweza kutawaliwa na ujinga kuhusu fedha na ukakufanya kuwa maskini.
Ujinga unaweza ukakufanya kutumia vibaya kile ambacho unapata bila hata ya kuweka akiba. Ujinga wa kutojua elimu ya hela na nini hela inahitaji ukishaipata ndio inafanya watu kuendelea kubaki katika hali duni.
Jifunze kuhusu pesa ili ufute ujinga.

6. Chochote unachopata katika kipato chako ishi chini ya kipato chako.
Kuishi juu ya kipato ni sawa sawa na kuwasha petrol sheli kwani muda wowote sheli italipuka na moto utakuunguza.
Hivyo, unatakiwa kuishi chini ya kipato chako haijalishi unapata au una ingiza kiasi gani.

7. Kama utakua na nidhamu katika maisha yako utafanikiwa kwenye mambo yote. Nidhamu ya kujisimamia binafsi katika mambo yako yote ikiwemo mambo ya fedha na mengine itakusaidia kupata Mali.
Kama huna hata nidhamu ya kujiwekea akiba usitegemee hata kupata utajiri hapa duniani. Maisha ya kupata na kutumia yote siyo maisha ya uchumi.

8. Watu wanafanya kazi na kupata hela na kulipa watu wengine lakini wanamsahau kumlipa mtu muhimu sana. Mtu unatakiwa kabla hujawalipa watu wengine jilipe kwanza wewe. Toa asilimia kumi ya kipato chako na jilipe kwanza wewe mwenyewe.
Na hii fedha iweke katika akaunti maalumu ambayo hutoitumia hovyo wala kuigusa. Hata ukiwa huna hela mfukoni usiingiwe na tamaa ya kwenda kuitoa.

9. Tabia moja wapo ya fedha inahitaji kuwekezwa na kuzungushwa. Wekeza pesa unayoipata katika maeneo mbalimbali.
Fedha haiwezi kukua kama haizalishi chochote hivyo, fedha inahitaji kufanyiwa uwekezaji na siyo kuiweka benki ikae.

SOMA ; Mambo Muhimu Niliyojifunza Katika Kitabu Cha Secrets Of The Richest Man Who Ever Lived

10. Adui wa ubora siyo ubaya Bali adui wa ubora ni kuridhika na kusema iko sawa tu.
Kwa mfano, ukimchukua chura na kumuweka katika maji ya moto atahisi maumivu na ataruka nje ya maji. Lakini ukimchukua chura na kumuweka katika maji ya joto la kawaida ataendelea kukaa na kufurahia. Wakati chura yuko katika joto la kawaida ukiwa unamwekea maji ya moto taratibu hatohisi chochote. Hivyo, mabadiliko huwa yanatokea kidogo kidogo katika maisha yetu na hatimaye yanakuja kutokea tayari kama ni kuzama umeshazama. Hivyo usidharau mabadiliko madogo madogo yanayotokea katika maisha yako.

11. Hakuna furaha nzuri katika maisha ya uchumi kama kuishi bila madeni
Madeni ni yananyima furaha.
Madeni yanafanya watu kuwa watumwa hapa duniani. Kama hujaingia kwenye madeni ni vema ukabaki hapo hapo ulipo kuliko kukopa.
Madeni yanakunyima kuwa na Uhuru wa kifedha.

12. Tabia ya uigizaji katika maisha haifai kabisa kwa mfano, Mtu ananunua kitu ambacho kipo nje ya uwezo wake kabisa ili mradi tu aonekane na rafiki kuwa yeye ni noma sana.
Habari mbaya ni kwamba huwezi kumfurahisha kila mtu hapa duniani. Kamwe usifanye mambo kwa kumfurahisha mtu au unafanya ili kujionesha kwa wengine kuwa wewe una kitu fulani kumbe hakuna.

13. Unatakiwa usiwe mtu wa kununua vitu vya gharama kubwa katika maisha yako. Tumia vitu vyenye gharama nafuu ili uweze kukuza uchumi wako.
Uchumi wa kifedha haukuzwi kwa nunua vitu vya kifahari kama vile magari na nk. Kwa mfano, hata ukinunua gari la kifahari leo asilimia 60 ya thamani ya gari hilo linapoteza thamani yake ndani ya miaka minne, na jinsi dunia na teknolojia inakua kila siku utafanikiwa kununua magari mangapi?
Hivyo, kama unataka kukua katika uchumi achana na mambo ya vitu vya starehe na vya kifahari.

14. Kama ukicheza na nyoka utapata kung’atwa tu. Hii ina maana ya kwamba kama ukifanya mchezo na kitu katika chochote katika maisha yako lazima kitakung’ata tu.
Usifanye masihara na maisha ukicheza nayo lazima yatakuumiza tu.

15. Kama una mtoto au watoto anza kuwafundisha mapema kuhusu mambo ya fedha tangu wakiwa wadogo. Wafundishe tabia kuhusu pesa na useme ukweli kuhusu pesa.
Kama mzazi na wewe hujui vizuri elimu ya pesa ni wakati wako sasa wa kujifunza. Soma vitabu mbalimbali,makala na jifunze hata kwa watu unaowajua wewe wako vizuri.

16. Kukopa hela benki ni njia ya kuifanya benki kuwa tajiri na siyo wewe. Usitegemee hata siku kuwa njia ya kukopa ndio njia ya kukupeleka kwenye utajiri. Benki wanahuburi na kuhamasisha watu waweze kwenda kukopa ili waweze kujiongezea utajiri.
Benki inakutegemea wewe ili iweze kuwa na utajiri na siyo kukufanya wewe kuwa tajiri.

17. Kuweka akiba na kuwekeza ndio njia inayoweza kusababisha utajiri kwa watu wengine.
Gepu kati ya walionacho na wasionacho litapunguwa kama kila mmoja akiweza kuwekeza na kuweka akiba.
Kupata fedha na kutumia ni njia nzuri ya kubaki kwenye umasikini.

SOMA; Mambo Muhimu Ya Mahusiano Niliyojifunza Katika Kitabu Cha Happier Marriage

18. Hadithi, mambo yatakuwa mazuri pale nitakapo staafu. Hata kama kwa sasa siweki akiba najua nipata kiinua mgongo changu.
Ukweli,
Mambo hayawezi kuwa mazuri hata pale utakapostaafu. Ukiwa na mawazo ya kutegemea kuwa na hela pale utakapo staafu ujuwe tayari umeshaenda na maji. Rafiki, muda mzuri wa kutengeneza maisha yako ni sasa na siyo kutegemea hela ya kustaafu. Huu ndio wakati mzuri kwako kutengeneza maisha yako wakati una nguvu.

19. Hadithi; nitapata utajiri haraka na kwa urahisi kama nikinununua DVD set ya mafanikio, kusoma vitabu,kuhudhuria semina, kujiunga na vikundi vya mafanikio na kujifungia ndani na kufanya kazi masaa matatu kwa wiki.
Ukweli; huwezi kufanikiwa kwa haraka na urahisi kwa kufanya kazi masaa matatu kwa wiki. Kufanikiwa ni mchakato siyo jambo la siku moja. Unatakiwa kufanya kazi zaidi ya masaa ya kawaida ya watu kufanya kazi. Unatakiwa kutumia masaa haya 24 vizuri kila siku ili uweze kufanikiwa.

20. Hadithi; nitakuwa tajiri kama nikicheza kamari,kubeti na aina nyingine za michezo ya bahati nasibu.
Ukweli; huwezi kuwa tajiri hata siku moja kwa ya kubeti, kamari na michezo ya kutegemea bahati nasibu. Kamari ni michezo inayowahakikishia watu kuwa watuma wa kubaki katika hali walizokua nazo.
Kwa mfano, watu wanaobeti wanatumika kama chombo cha kumwezesha mmiliki wa mchezo huo kuwa tajiri na ukiendelea kubaki na hali yako. Kama wewe ni mtu unayebeti jaribu kupiga mahesabu hela ulizoliwa tokea uanze kucheza mchezo ni shilingi ngapi? Je ungejiwekea akiba leo usingepata mtaji wa kuanzia kwenye biashara?

Nakutakia kila la heri katika haya niliyojifunza leo. Washirikishe na wengine maarifa haya mazuri uliyojifunza.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk @gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: