Mpendwa rafiki yangu,
Sidhani kama kuna mtu ambaye amekuja hapa duniani na kujiwekea ndoto ya kuwa masikini. Kila mmoja wetu anapenda maisha mazuri na vitu vizuri. Tunakuja kupata changamoto ya kuwa na maisha hayo tunayotaka pale katika utafuti wa kuwa na vile tunavyotaka.
Wote tunajua kabisa ili tufanikiwe tunahitaji kufanya nini lakini njia ya kufanikiwa ni nyembamba na haina foleni ila ni ngumu sana kupita ndiyo maana unaona watu wengi wanachagua kupitia njia kubwa ambayo kila mtu anapita.
Watu kwa asili hawapendi vitu vinavyowaumiza hivyo ndiyo maana wanachagua kupita njia rahisi. Siku zote kule kwenye urahisi mwisho wake kuna kuwa mbaya sana na kwenye magumu mwanzoni kuna kuwa pagumu ila mwishoni ni parahisi sana.

Kila mmoja wetu anachagua kuishi vile anavyotaka yeye. Na zifuatazo ni sababu tatu zinazo watofautisha tajiri na masikini.
- Tabia , unaweza kumfundisha mtu kazi lakini siyo tabia. Tunatengeneza tabia na kisha tabia zinatutengeneza sisi. Tabia ndiyo zinatutofautisha sisi, huwezi kumkuta mtu masikini amekaa chini hata anasoma kitabu kwa kujifunza lakini utamkuta analalamika juu ya hali ngumu ya maisha.
Unawezaje kubadilisha au kuacha tabia ambayo inakurudisha nyuma? Huenda ni ulevi wa kupindukia ndiyo unakurudisha nyuma, je huwezi kuiacha hiyo tabia? Jiulize tabia uliyonayo itaweza kukufikisha kwenye uhuru wa kifedha? Kama una tabia ambazo zinakupeleka sehemu ambazo siyo ni za kimasikini ziache mara moja.
Maisha ni tabia, angalia tabia nzuri za kitajiri na ziishi na achana na za kimasikini kwa kwani hazina faida.
SOMA; Jijengee Tabia Hii Muhimu Katika Mambo Ya Fedha
- Akili; masikini huwa wanafikiria kwenye uhaba sana lakini tajiri huwa anafikiria kwenye utele. Dunia ina utajiri wa kila aina, fursa za kila aina lakini tajiri anaziona ila masikini hazioni. Matajiri wanafanikiwa sababu wanaamini katika utele.
Hivyo basi, ukitaka kufanikiwa badili kwanza mtazamo wako wa akili, kama akili yako ni hasi huwezi kufanikiwa bali utaishia kwenye umasikini wa kutupwa.
Badili kwanza mtazamo wako wa akili kabla hujabadili uelekeo wako.
- Vitendo; matajiri ni watu wa kuchukua hatua kila siku, ila masikini ni watu wa kuahirisha mambo. Kulalamikia yale yanayoendelea kutokea katika maisha yao kiujumla.
Mafanikio yako kwa wale wanaochukua hatua, hata uwe mtu mwenye tabia nzuri kiasi gani lakini kama huchukui hatua utabakia hivyo hivyo ulivyo. Mafanikio yako kwenye kuchukua hatua na kadiri unavyochukua hatua ndivyo unavyozidi kufanikiwa.
Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kufanikiwa jenga tabia za kitajiri, badilisha mtazamo wa wa akili na fikiria kwenye utele na tatu fanya yote kwa vitendo na hapo utaweza kufanikiwa kwenye kile unachotaka.
Hivyo basi, hakuna kazi rahisi kila kitu kinahitaji kazi kama zilivyo kazi nyingine. Ukitaka kupata kitu chochote lazima uweke kazi na kama unataka utajiri lazima uweke kazi hali kadhalika umasikini. Jitoe kwenye kile unachotaka na acha mengine kwani ni usumbufu tu kwako.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.