Mahusiano Ni Kujali

Sisi binadamu ni viumbe vya hisia, huwa tunaongozwa na hisia. Na sisi binadamu tuko hapa duniani kwa sababu tunahusiana na wengine. Tuwapokee wale ambao tumepewa kama walivyo kwani sisi kazi yetu siyo kuwabadilisha watu bali kutumia yale mazuri ambayo yapo ndani ya watu.Jitahidi sana kupata UTULIVU kwenye ENEO la mahusiano, litakuongezea hamasa kwenye uzalishaji. Usitafute …

Dalili Za Mtu Aliyefanikiwa

Utaweza kujua kama mtu ana uelekeo kwenye maisha yake au la kwa kuangalia vitu vifuatavyo. Sina uhakika kama itakufaa lakini mtu aliyefanikiwa dalili yake ya kwanza iko kwenye matumizi ya muda. Kwa mfano, watu wengi ambao bado hawajafanikiwa na wana fikra za kimasikini huwa wanatumia muda kuokoa fedha. Hakuna kitu kibaya katika zama hizi kama …

Njia Pekee Ya Kufaulu Mitihani Ya Maisha

Ukiwa shuleni ili ufaulu lazima usome vitabu hata katika maisha, ili uendelee kufaulu mitihani ya maisha ni kuendelea kujifunza kupitia usomaji wa vitabu. Kwenye kusoma unapaswa kusoma vitabu unavyovipenda na kuvielewa lakini vile vitabu vigumu na usivyovipenda. Unaposoma vitabu vya aina mbalimbali unakua unaitanua akili yako na kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri. Hii itakusaidia …

Angalia Orodha Yako

Unapoianza siku yako unakutana na mengi, usipokuwa na orodha ya kufanya mambo yako yaani to do list ni rahisi kuhangaika na yale ambayo hata hukuyapangilia. Mambo ambayo hatujayaandika kuyafanya ndiyo mambo ambayo huwa yanatuondolea fokasi kubwa kwenye siku yetu. Unajikuta unatumia muda mwingi kwenye drama ambazo hazina maana kwako.Unatakiwa kuwa na mfumo wa kusema HAPANA …

Mtu Mwenye Maono Makubwa

Jana kuna kauli moja ambayo niliisikia kutoka katika mijadala ya watu, walikuwa wanaongea mengi ila kuna sentensi moja ilinitafakarisha sana. Kauli hiyo ni mtu mwenye maono makubwa huwa hali hovyo. Nikaitafakari na kuona ni kweli, huwezi kumkuta mtu mwenye maono makubwa amekaa vijiweni anakula na vyakula vya hovyo. Kwa sababu, kupitia chakula hata watu ambao …

Hakuna Mafanikio Bila Mateso

Kama kuna mtu anakuambia kwamba unaweza kufanikiwa kwenye jambo lolote lile bila mateso huyo anakudanganya. Pata picha kwa yale mafanikio ambayo unayo, ni mafanikio gani ambayo umeyapata kirahisi bila mateso? Njia ya mafanikio yoyote ile ni ngumu, ina mateso ndiyo maana wengi WANASHINDWA na kuishia njiani. Hakuna mafanikio utakayopata kwa njia ya imani tu, imani …

Njia Ya Kwenda Motoni Imepambwa Kwa Nia Njema

Vitu vingi vinavyoharibu hata afya na maisha yetu ni vile vitu vitamu, angalia sukari ni nzuri lakini ukiizidisha inavyokuletea shida. Kuishi bila mazoezi ni raha kwa sababu huusumbui mwili lakini matokeo yake yanakuja kukuumiza baadaye. Mtu anakuwa anaiba kwa nia njema kabisa, kwa mfano umemwajiri mtu siku akajisikia kuchukua elfu tano halafu ukimlipa mshahara atakuja …

Kinachowezekana Kufanyika, Kifanyike Sasa

Huwa tunajidanganya sana kwa kuahirisha mambo yetu ambayo tunaweza kufanya sasa hivi lakini tunajiambia baadaye. Sina uhakika kama itakufaa lakini, kile unachoweza kufanya sasa hivi, kifanye mara moja usisubiri baadaye. Pata picha wewe mwenyewe ulivyojikosesha au kujikwamisha mambo mengi kwa kujiambia kesho, baadaye au mwakani. Unajionea wewe mwenyewe jinsi ulivyoshindwa kwa kujiwekea vitu mbele?Kama kitu …

Unataka Nikusaidie Nini?

Ni moja ya swali ambalo Yesu alimuuliza kipofu, kipofu akamjibu, nataka kuona tena. Katika maisha ya kila siku hatuwezi kupewa kama tusiposema tunataka nini? Ili ufanikiwe kwenye kitu chochote kile, lazima kwanza ujue unataka nini, kama hujui unataka nini hakuna atakayeweza kukusaidia. Mungu aliyekuumba pasipo wewe kupenda, hawezi kukubadilisha pasipo wewe kupenda. Je, kuna kitu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started