Jambo La Msingi Kwenye Maisha Yako

Fanya vitu vyote lakini usiache kufanya vitu vya msingi kwenye maisha yako. Na kupambania lengo lako ndiyo jambo la msingi. Fanya uwezavyo lakini usiache kupambania lengo. Drama ni nyingi kwenye maisha. Kiki ni nyingi ambazo zinakukwamisha wewe kutokufikia kwenye malengo yako. Puuza vitu vyote lakini usipuuze kupambania lengo lako kuu.Kila unapoamka asubuhi, jikumbushe lengo lako …

Unajizima Data

Kujizima data ni pale ambapo unakuwa unaambiwa kitu au kupata maelekezo ya kitu fulani halafu unafanya tofauti na maelekezo uliyopewa. Unakuwa unajua unachopaswa kufanya lakini unajifanya kama hujui kwa kufanya kile ambacho siyo sahihi. Kama vile unapima hebu tuone itakuwaje kama nisipofanya hivi. Unakuwa unamjaribu mhusika je atasemaje? Mtu makini na kazi yake au yule …

Usiende Safari Ndefu Ukiwa Huna Mafuta Yakutosha

Dereva yoyote anayetaka kusafiri safari ndefu lazima lazima atahakikisha gari lake liko vizuri. Na kitu muhimu zaidi ni kuangalia kama mafuta yako ya kutosha. Kwa sababu, asije akaanza safari halafu katikati ya safari mafuta yameisha na kushindwa kuendelea na safari. Katika mafanikio makubwa, ni safari ya ndefu. Ni safari ambayo inahitaji uwe unajaza mafuta mara …

Unatakiwa Ufikie Kiwango Hiki

Kwenye maisha unatakiwa kujijengea sifa ambayo mtu anakuwa hana shaka yoyote ile juu yako. Kwa mfano, mtu akikuachia kazi, asiwe na wasiwasi aende akalale hata usingizi. Tunataka mtu akikupa kazi na anaenda kulala. Yaani mpe mtu kazi na ukalale usingizi. Je, umefikia viwango hivyo? Watu wengi ukiwapa kazi unakuwa na wasiwasi hata kulala utashindwa. Kwa …

Usiwape Watu Kiki Kirahisi

Hizi ndiyo zama ambazo watu wanaishi kwa drama sana. Watu wanaishi kwa kutafuta kiki ili maisha yao yaweze kwenda. Usiwashangae watu kufanya mambo ya kijinga, jua wanafanya hivyo kwa sababu ni kazi yao kufanya hivyo ya kutafuta kiki. Tunajua watu ambao wanatafuta kiki ni wasanii tu, lakini kwa sasa hata watu ambao siyo wasanii nao …

Vichocheo Viwili Vya Kukusaidia Kufanya Makubwa Kila Siku

Thamani na kusudi vitakupa kichocheo cha kufanya kila siku. Kuweza kufanya kitu kila siku kwa maisha yako yote siyo rahisi, wengi hukata tamaa na kuacha baada ya muda. Wengi wanaishia njiani, kukaa kwenye mchakato kila siku siyo kazi rahisi inahitaji kuwa na kitu ambacho kinakusukuma kufanya hivyo. Vipo vitu viwili ambavyo vinaweza kukupa kichocheo cha …

Tahadhari; Kuna Mtu Anaitamani Nafasi Yako

Bilionea Mark Cuban anasema kuwa, fanya kazi masaa 24 kama kuna mtu mwingine atakuja kukutoa hapo. Kila nafasi ambayo upo kuna mtu mwingine anaitaka sana hiyo nafasi hivyo usipoifanyia kazi watu wengine watakunyang'anya nafasi hiyo. Kwa mfano, mteja uliyenaye haumtamani kuwa naye peke yako, bali kuna watu wengine pia wanamtamani. Biashara unayofanya siyo kwamba wengine …

Hakuna Kitu Kitakachokuja Ukiwa Hivi

Iko wazi kwamba hakuna kitu kitakachotokea au kuja kwenye maisha yako ukiwa umekaa. Hii ina maana gani? Hii ina maana kwamba, kila kitu kwenye maisha yako utakipata kwa njia ya kupambania. Ni bora mtu ambaye anafanya kuliko mtu ambaye hafanyi. Mkaa bure si sawa na mtembea bure. Milango haifunguki pasipo kufunguliwa. Pata picha kama uko …

Sehemu Rahisi Ya Kuanzia Kujifunza

Mtu mmoja aliwahi kunukuliwa akisema, ninachotaka kujua ni wapi nikienda nitakufa na niepuke kwenda sehemu hiyo. Hii ina maana gani? Tunapaswa kujua ni vitu gani tukifanya tutaishia kupata maumivu na wapi tutapata matokeo mazuri. Hivyo basi, sehemu nzuri ya kujifunza ni kwenye makosa yako mwenyewe na makosa ya wengine. Angalia kwako wewe mwenyewe ulifanya makosa …

Design a site like this with WordPress.com
Get started