Ili Kupata Unachotaka Lazima Ufanye Hiki

Rafiki, Wajibu wako mkubwa kwenye maisha yako ni kupata kile unachotaka hasa. Mafanikio ambayo tunayatafuta tutayapata kwa wengine.Kuna vitu ambavyo wewe unavitaka lakini mwingine anavyo.Hivyo basi, kupitia watu, ndipo malengo yetu yanaweza kutimia. Na ili kupata unachotaka, lazima uwasukume wengi wapandishe viwango vyao ili kufikia viwango vyako wewe.Kwa mfano hapa, kama una wateja ambao wanafanya …

Huhitaji Kila Mteja

Kwenye biashara huhitaji kila mteja anunue kwako. Watu wanafikiri kwamba kila mtu anaweza kuwa mteja wako. Lakini, kwenye biashara siyo kila mtu anaweza kuwa mteja wako.Kwenye biashara huhitaji kila mteja bali unahitaji mteja ambaye anajua thamani yako.Mteja anayeijua thamani yako, hawezi kujiuliza mara mbili kwako anunue au asinunue. Mteja anayeijua thamani yako huwa ananunua. Mauzo …

Fanya Kitu Hiki Kila Mahali Unapoenda

Rafiki, Fanya angalau kitu kimoja kuwa bora kila mahali unapoenda. Yaani unapoenda sehemu, uwaachie baraka au habari njema itakayowafanya watu hao waneemeke kupitia wewe. Usiende sehemu yoyote ile, ukaondoka hujabadili kitu chochote kikawa bora. Itakua haina maana yoyote ya wewe kuwepo eneo hilo. Kama umekutana na mtu hakikisha unamwacha akiwa bora kuliko alivyokuwa. Kazi yetu …

Ushindani Ni Mkali

Kama ushindani ni mkali jifunze kujitofautisha na wengine.Ukiwa chini huwezi kujua uhasilia ukoje. Ni mpaka pale utakapokua ndiyo utajua uhalisia ukoje. Hata mamlaka ya mapato ukiwa chini kwenye biashara, hawahangaiki na wewe.Ila pale utakapokua, ndiyo wataanza kukufuatilia. Ukiwa chini, watu wanakuwa hawana mpango na wewe.Unapokua sasa, ushindani unakuwa ni mkubwa sana kwako. Ukianza kukua, watu …

Jinsi Ya Kuwa Mbele Ya Wengine

Hakuna zama ambazo ni rahisi kufanikiwa kama zama hizi tunazoishi.Zama tunazoishi zina kila aina ya fursa za kukuwezesha wewe kufanikiwa. Ukitaka kuwa mbele ya wengine, basi kuwa mtu wa kujifunza.Ukishakuwa mtu wa kujifunza lazima utakua unajua vitu vingi kuliko wengine. Anguko linaanza pale unapokuwa mjuaji na kujiona wewe unajua zaidi na kuacha kujifunza zaidi. Hakikisha …

Mambo Matano Muhimu Ya Kuzingatia Kwenye Maisha Yako

Rafiki yangu,Kwenye kitabu cha 12 Rules for Life mwandishi Jordan Peterson anatushirikisha mambo muhimu ya kuzingatia katika maisha yetu. Na baadhi ya mambo ambayo mwandishi anatushirikisha ni kama ifuatavyo; Sema ukweli. Nafikiri hili halina haja ya maelezo marefu, sema ukweli mara zote, usidanganye hata kama ni kitu kidogo kiasi gani, sema kweli na kweli itakuweka …

Huhitaji Kuwa Na Anasa

Kama bado hujafanikiwa kwenye maisha yako, huhitaji kuwa na anasa kwenye maisha yako. Kama huna fedha, huhitaji kuwa na anasa ya kuchagua kazi ya kufanya.Unapata wapi UJASIRI wa kuwa na maisha ya anasa wakati maisha yako bado hujayajenga? Kama bado hujafanikiwa huhitaji kuwa na demokrasia kwenye maisha yako.Nini ufanye na nini usifanye.Huhitaji kuwa na anasa …

Matatizo Mengi Ya Kifedha Yanaanzia Hapa

Ukiangalia matatizo mengi ya kifedha ambayo watu wengi wanakutana nayo, mengi yako chini ya milioni moja. Dharura za fedha nyingi katika jamii zetu huwa ni chini ya milioni moja. Hata watu wengi wanaingia kwenye madeni madogo madogo ni kwa sababu ya kukosa kiasi cha fedha cha milioni moja. Hivyo basi, ili kuepukana na mikopo midogo …

Usipofanya Hiki, Kuna Mtu Atakuja Kuchukua Nafasi Yako

Bilionea Mark Cuban aliwahi kunukuliwa akisema, fanya kazi kama vile kuna mtu atakuja kuchukua nafasi yako.Maisha ni vita. Nafasi yoyote uliyonayo, kuna mtu anaitamani. Usipoipambania, kuna mtu ataichukua. Biashara uliyonayo, kuna mtu anaitamani. Wateja ulionao kuna mtu anawatamani.Usiwahudumie vizuri, wataenda kwa mwingine.Kazi unayofanya, nafasi uliyopewa kuna mtu anaitamani. Anakusubiria tu wewe uzingue halafu achukue nafasi …

Ni Bora Kufanya Kuliko Kutokufanya

Makosa mabaya sana kwenye maisha yetu ni yale ambayo unajua nini cha kufanya lakini hufanyi. Ni mangapi ambayo unayajua kwenye maisha yako lakini huyafanyi? Ni bora kufanya hata kama utapata matokeo ya tofauti, kuliko kujua lakini hufanyi kile unachopaswa kufanya. Unapaswa kufanya kila unachojua ili uweze kupata matokeo mazuri. Ni dhambi kujua kitu halafu hufanyi. …

Design a site like this with WordPress.com
Get started