Jinsi Ya Kujenga Mahusiano

Rafiki yangu mpendwa, Ushauri ninaotaka kukupa leo ni huu: wapigie simu marafiki zako bila sababu yoyote. Tumezoea kuwapigia watu wetu wa karibu tu pale tunapohitaji kitu fulani kutoka kwao. Mara nyingi, tunapopokea simu kutoka kwa mtu, wazo la kwanza linalotujia ni: "Anataka nini huyu?" Au "Labda ana shida na anahitaji msaada."Lakini hebu fikiria jambo hili …

Haifanyi Kazi? Tafakari Tena!

Rafiki yangu mpendwa, Watu wengi wanapojaribu jambo mara moja na halifanikiwi, hufikia hitimisho kwamba "haifanyi kazi." Lakini je, kweli jambo hilo halifanyi kazi, au ni sisi tunaokosa kulifanyia kazi ipasavyo? Katika jamii yetu ya sasa, tumekuwa na hulka ya kutaka mambo yatokee mara moja—bila kuchelewa, bila kujisumbua, bila kupitia changamoto. Tunataka mafanikio ya haraka, bila …

Kitu Muhimu Cha Kuwa Nacho Pale Unapopitia Magumu

Rafiki yangu mpendwa, Kuna nyakati katika maisha tunahisi tumeyapatia—kila kitu kinakwenda sawa, hakuna changamoto kubwa mbele yetu. Lakini asili ya maisha haiko hivyo. Hakuna hali inayodumu milele. Furaha unayoipata leo haitodumu milele, na vivyo hivyo, huzuni unayopitia sasa haitadumu milele. Kila kitu huja kwa muda wake. Mazuri na mabaya yote ni sehemu ya safari ya …

Hivi Ndivyo Ulivyo

Rafiki yangu mpendwa, Jinsi unavyofanya kitu chochote ndivyo unavyofanya kila kitu. Huwezi kujikimbia wala kujidanganya katika maisha haya. Kila unachofanya kwa jambo moja ndicho unachofanya kwa mambo mengine yote. Kwa mfano, kama ni mwaminifu katika kazi ya watu hata ya kwako itakuwa hivyo hivyo. Tabia yako katika eneo moja inaakisi tabia yako katika maisha kwa …

Leo ni Maandalizi ya Kesho

Rafiki yangu mpendwa,Kila unachofanya leo kina mchango mkubwa katika maisha yako ya kesho. Mazoea, maamuzi, na juhudi zako za leo zitaamua namna kesho yako itakavyokuwa. Ikiwa unafanya mambo yako kwa uzembe au bila mpango, basi tarajia kesho yenye matokeo yasiyoridhisha. Lakini ikiwa leo unajituma, unajifunza, na kujiboresha, basi unajitengenezea kesho yenye mafanikio. Matokeo mazuri ya …

Mazingira Yanashinda Mara Zote

Rafiki yangu mpendwa, Ili uweze kushinda vishawishi vya aina yoyote, epuka mazingira yanayokuvuta kwenye mazoea mabaya. Mazingira yana nguvu kubwa kuliko hata utashi wako (willpower). Kama hutaki kuwa mtumwa wa mitandao ya kijamii, epuka kuwa na simu janja au futa apps zinazokula muda wako. Tafiti zinaonyesha kuwa kwa sasa, TikTok ndiyo mtandao unaoongoza kwa kunasa …

Hakuna Kinachopotea

Rafiki yangu nikupendaye, Chochote kile ambacho unajifunza sasa hivi, jua unafanya uwekezaji na utakuja kukusaidia baadaye. Ni kama vile unavyokula, virutubisho vinabaki ndani yako. Na unaposoma, unawekeza. Vile unavyojifunza sasa unaweza kuviona siyo muhimu lakini siku ukiwa una changamoto fulani unajikuta unavitumia bila hata wewe mwenyewe kujua. Asikuambie mtu maarifa hayana maana, mwache aendelee kujaribu …

Huwezi Kukimbia Maumivu

Rafiki yangu mpendwa, Katika safari ya maisha, kuna kitu kimoja ambacho kila mtu anakutana nacho ambacho ni maumivu. Haijalishi unajaribu kwa kiasi gani, huwezi kuyakimbia kabisa. Ni aidha ukubali kuyakabili sasa au ukubali athari zake baadaye. Huwezi kujikimbia wewe mwenyewe. Kukimbia maumivu yako ni sawa na kujikimbia wewe mwenyewe kitu ambacho hakiwezekani. Kuna aina mbalimbali …

Umuhimu wa Kujua Namba Zako

Rafiki yangu nikupendaye, Kila kitu kilichokuzunguka ni hesabu. Kila kilichokuzunguka ni namba. Kwa kifupi, maisha ni mchezo wa namba. Hatuwezi kukwepa namba kwenye kila eneo la maisha yetu. Kuku analalia kwa siku kwa wiki tatu, na mama mjamzito anabeba mimba kwa miezi tisa. Hii inatuonesha kwamba maisha yetu ni mchezo wa namba. Hatuwezi kukwepa namba …

Design a site like this with WordPress.com
Get started